Polisi waua tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waua tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Oct 4, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi la Polisi limeendelea kuandamwa na matukio ya kuua raia baada ya askari wake wanne, akiwamo Mkuu wa Kituo (OCS) kukamatwa kwa tuhuma za kuvamia nyumba ya kulala wageni, kujeruhi, kupora mali na kumuua mchimbaji wa madini.

  Tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Chato, mkoani Geita baada ya askari hao kutuhumiwa kuwavamia wafanyabiashara wawili waliokuwa kwenye nyumba hiyo, kuwapora fedha, mawe yanayosadikiwa kuwa dhahabu na kuwajeruhi kwa vipigo ambavyo vilisababisha kifo cha mmoja wao.

  Askari wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo ni wa kituo cha polisi cha Buziku wilayani Chato ambao waliwavamia David Gilles Vyamana na Gilbert Ntabonwa, wakazi wa kijiji cha Kakeneno wilayani humo na wazaliwa wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

  Tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 30, mwaka huu wakati watu hao wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Buziku Inn.

  Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni wachimbaji wadogo wa dhahabu, kabla ya kukumbwa na mkasa huo, walitokea kijijini kwao Kakeneno na kuelekea kijiji cha Buziku kwa ajili ya kuburudika na kwamba baada ya kupanga vyumba katika nyumba hiyo mmoja akiwa chumba namba mbili na mwingine namba tatu, walimuomba mhudumu kuendelea kuwahudumia vinywaji wakiwa vyumbani.

  Habari zinasema kuwa saa 5:30 usiku, polisi walivamia eneo hilo na kuwaamuru wachimbaji hao kufungua milango ya vyumba vyao.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya watu hao kukataa kutii amri hiyo huku wakihoji uhalali wa kuwaamuru kufungua milango wakati wamelala, askari hao walitumia nguvu kubwa na kufanikiwa kuvunja milango kisha kuanza kuwaadhibu kwa vipigo vikali.

  Habari zinadai kuwa katika chumba cha kwanza askari hao walichukua kiasi cha Sh. 500,000 na mawe yanayosadikiwa kuwa ni dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye mfuko mdogo katika chumba cha pili.

  Baada ya kuwapa kichapo, waliwachukua na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi na kushikiliwa kwa muda na baadaye baada ya kubaini kuwa hali zao zinaendelea kuwa mbaya kutokana na majeraha, walilazimika kuwaondoa haraka na kuwapeleka kwenye Kituo cha Afya cha Bwanga kabla ya kuwahamishia Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu zaidi.

  Shuhuda mwingine, alidai kuwa baada ya wachimbaji hao kukaidi kufungua milango licha ya mhudumu wa nyumba hiyo, Godesiliva Paulo, kuwataarifu kuwa wanaowahitaji ni askari polisi, polisi walilazimika kutumia nguvu kuingia ndani, lakini katika hali ya kushangaza wachimbaji hao walikutwa ndani ya chumba kimoja wakiendelea kunywa pombe na ghafla mmoja wao alimkwida koo PC Mwidin, hali iliyowalazimu kutumia nguvu kubwa kuwaondoa vyumbani vyao kwa lengo la kuwapeleka kituo cha polisi.

  Aliongeza kuwa baada ya askari hao kufanikiwa kuwatoa ndani ya chumba wachimbaji hao walikaidi kwenda kituo cha polisi na kuanza kupiga yowe wakiomba msaada kwa wananchi na baada ya muda mfupi, watu wengi walikusanyika eneo hilo na kuanza kuwashambulia na kuwajeruhi.

  Alisema kuwa baada ya kutambua hali zao siyo nzuri walilazimika kuwapeleka kupata matibabu, lakini wakati wakiendela kuhudumiwa, mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Gilbert Ntabonwa (40) alifariki dunia akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chato.

  KAULI YA KAIMU RPC

  Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Paulo Kasabago, mbali na kuthibitisha kuwapo kwa tukio hilo, alisema kuwa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa askari wake walienda kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaohofiwa kuwa ni wahalifu kutokana na mazungumzo yao wakati wakinywa pombe kabla ya kuingia ndani ya vyumba vyao.

  “Askari wetu walikwenda eneo hilo baada ya kupigiwa simu na raia mwema kuwa watu waliokuwa wakinywa pombe kwenye gesti hiyo siyo wema kutokana na mazungumzo mbalimbali waliyokuwa wakiyazungumza kabla ya kuhama nje na kuingia ndani ya vyumba vyao,” alisema Kasabago.

  Kufuatia hali hiyo jeshi hilo linawashikilia askari wake wanne akiwemo mkuu wa kituo hicho, Sajenti Raulens Bendera, kwa ajili ya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo la mauaji na kwamba itakapothibitika kuhusika, hatua za kisheria zitashika mkondo wake.

  ASKARI WANAOSHIKILIWA

  Kamanda Kasabago aliowataja wengine wanaoshikiliwa kuwa ni PC Mwidini, PC abdallah na PC Yusuph, wote wakiwa ni askari wa kituo kidogo cha Buziku wilayani Chato.

  Kamanda Kasabago aliongeza kuwa baada ya upekuzi uliofanywa na askari hao, waliwakuta wachimbaji hao wakiwa na fedha taslimu Sh. 500,500, kiroba cha mfuko unaosadikiwa kuwa na mawe ya dhahabu na chupa moja ya bia.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chato, Dk. Pius Buchukundi, alithibitisha kupokea majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo kutoka Kituo cha Afya cha Bwanga na kwamba wakati wakiendelea kuwatibu, mmoja wao alifariki dunia na kwamba Vyamana anaendelea vizuri.

  Dk. Buchukundi alisema kuwa uchunguzi wao ulibaini kuwa marehemu alijeruhiwa kutokana na kipigo kilichosababisha damu kuvujia ndani ya mwili.

  Kwa mujibu wa Dk. Buchukundi, tayari ndugu na jamaa wa marehemu huyo wamefika na kuchukua mwili wake kwa ajili ya kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Kibondo, mkoani Kigoma kwa ya maziko.

  Septemba 2, mwaka huu, polisi walimuua aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakifungua tawi la chama chao.

  Askari mmoja, Pacificus Cleophace Simon (23), alifikishwa mahakamni mjini Iringa akikabiliwa na kosa la kumua Mwangosi.

  Jumapili iliyopita Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa Septemba pamoja na mambo mengine aliwataka polisi kuacha kutumia nguvu kupita kiasi wanapokabilina na vikundi na raia.  Ila ukweli kua wameshazowea kuua hao au hamukumbuki mwaka 2001 kule Zanzibar walivofanya?.....
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Chonde Chonde serikali mkichelewesha mishaara huku mtaani inakua vurugu,maaskari wanaua kisa hamjawapa mishaara! Hala mlivyochelewesha mishaara ya mwezi wa 7 askari wengi waliuwawa kwenye vitendo vya wizi.
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sikia hadithi zao.....tulipata taarifa kutoka kwa raia juu ua mazungumzo yaoooo, wanajua hatuwezi kuthibitisha hayo!
   
 4. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Hivi viongozi wetu wanadhani kuwa raia watakubali kundelea kuuwawa tu? Hawajui kuwa raia nao kwa kuchoka uonevu au kwa kutaka kulipiza kisasi au kutaka kujilinda wanaweza nao kuanza mauaji ya kijinga kama haya ya hawa polisi? Watz tunalalamika sana sasa ila naamini kama hali itaendelea hivi kutatokea raia ambao watakuwa wanawaonyesha polisi kuwa wamechoka. Sidhani kama ni sahihi na busara kwa viongozi wetu kukubali baadhi ya askari kuendelea kuuwa raia. ITAFIKA MAHALI RAIA WATAAMUA NAO KUUA TU KWA SABABU WASIPOUA ASKARI, ASKARI WATAWAUA. Ni upu.u.zi watu wanaouwa kila siku na wengine wanawalinda. Shame on you canibalists
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kuna siku kibao kitageuka na hakutakuwa na amani tena
   
 6. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inaonekana hawa jamaa walikua majambazi kwa mujibu wa muhudumu wa gesti...Tena hata majina yao ni kama watu wa kigoma hawa..hakika ni majambazi wakutupwa hao wanatokea burundi na kuua watu Geita hongera raia wema kwa kuwapa kichapo manyangau hayo...Wamwambie zitto aanzishe jamhuri yao si walisema wanataka jamhuri ya wachawi wa kigoma...
   
 7. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hata jambazi ana haki ya kuishi ajitetee na km ana hatia apewe haki ya kifungo
   
 8. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  bila shaka utakuwa ni kichaa tena umetoroka milembe, na km sio kichaa nakushauri uache bangi
   
 9. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  umenena mkuu maana mi Raia bana huwa haielewielewi imekaa kimajungu majungu 2 hv sisi watanzania ndo maana hatuendelei sababu ya MAJUNGU.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  Tanzanian Police were born to be NATURAL KILLERS
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  polisi njaa nendeni mkapore nyumbani kwa nchimbi,chagonja na mwema
   
 12. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  jambz hana hak ya kuish hv ebu ulizia lile pori la kosovo pale kasulu ndo utajua kama hawa wa2 ni wa aina gan.? Hawana huruma
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  Tanzania kisiwa cha amani na utulivu nani kakwambia?
  Tunao majambazi ambao ni wahalifu,
  Pia polisi nao ni majambazi na wauaji wakubwa.
  Je i wapi amani yetu? Uko wapi usalama wetu?
   
 14. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  hawana njaa labda njaa unayo wewe..
   
 15. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  mkuu usimlaumu sanaaa kabla ya yote ungejua ni gamba lililo kakamaa?? Kamwe usinge mlaamu yaani akili yake imeganda hiv hapo kajikakamua na kutumia busara mpaka mwisho.
   
 16. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Very bad! real bad
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,530
  Likes Received: 10,442
  Trophy Points: 280
  Hii habari ukisoma kwa umakini unajichanyanya,kama hao washukiwa walishambuliwa na wananchi wenye hasira, hao askari wanashikiliwa kwa kosa gani.? hao raia tunaambiwa walikua wamejifungia wanakunywa pombe badae tunaambiwa ilikutwa chupa moja tu ya pombe.inamaana wote walikua wanakunya pombe moja.?
   
 18. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  Kwa uzoefu unapokwenda kukagua guest house lazima iende kamati ya ulinzi na usalama nikiwa na maana si lazima kamati yote but at least mwakilishi mmoja ambae ni raia na lazima awe mtumishi wa serikali, polisi si wa kuwaachia kufanya mambo wenyewe inapokuja suala la kwenda kufanya searching kwa watu na ndio maana ukienda mtaani wanatakiwa kwenda na kiongozi wa serikali za mtaa
   
 19. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  nimekugusa riafande..nyuma geuka,mbere tembea
   
 20. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  JAMANI HEBU SOMENI TENA HUU USANII WA POLISI "Aliongeza kuwa baada ya askari hao kufanikiwa kuwatoa ndani ya chumba wachimbaji hao walikaidi kwenda kituo cha polisi na kuanza kupiga yowe wakiomba msaada kwa wananchi na baada ya muda mfupi, watu wengi walikusanyika eneo hilo na kuanza kuwashambulia na kuwajeruhi".

  This reminds me kauli ya ACP Paulo Changonja "Daud Mwangoshi aliuawa na kitu kizito kichotupwa kwake na wafuasi wa CDM"

  Halafu watu hawa (read Polisi) ndiyo JK anataka tuwaheshimu na kutii amri zao. Jeshi la Polisi linahitaji kufumuliwa lote.

  Haiwezekani mtu apige mayowe ya kuomba msaada, halafu watu wakusanyike waanze kumushambulia tena huyo mtu aliyepiga mayowe ya kuomba msaada tena eti mbele ya POLISI.

  These kind of stetments is ONLY POSSIBLE IN TANZANIA, Very unfortunately hata Amri jeshi mkuu ana buy those kind of stetments!
   
Loading...