Polisi waua tena

Inasikitisha sana kuona jinsi polisi wanavyotumia nguvu kubwa katika kudhiru/kuuwa raia wema na kuwaacha mafisadi wakipeta.

Pia hili la wakuu wao kutoa matamshi a utetezi kwamba "walipata taarifa kutoka kwa raia wema" ili kuhalalisha uhalifu wa polisi halitavumilika.

Tunaamini polisi ni watu waliopata mafunzo ya kuhoji, kuchunguza na kubaini kuwepo kwa uhalifu ama lah. Inakuwaje hawa watu wapoteze pesa na madini yao chini ya mikono ya polisi ambao ndiyo wanadhamana ya kulinda usalama wao?

Hata kama mtu amelewa, polisi bado inajukumu la kuangalia usalama wake na siyo kuitia watu wawauwe ili wafiche uhalifu wao.
 
inashangaza kuona washukiwa wa ujambazi wanakamatwa hata silaha moja hawana.!
 
Acha ujinga, unawahukumu vipi? ilipaswa wakamatwe wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na siyo kuwaua kwa kisingizio cha taarifa ya raia wema
Inaonekana hawa jamaa walikua majambazi kwa mujibu wa muhudumu wa gesti...Tena hata majina yao ni kama watu wa kigoma hawa..hakika ni majambazi wakutupwa hao wanatokea burundi na kuua watu Geita hongera raia wema kwa kuwapa kichapo manyangau hayo...Wamwambie zitto aanzishe jamhuri yao si walisema wanataka jamhuri ya wachawi wa kigoma...
 
sikia hadithi zao.....tulipata taarifa kutoka kwa raia juu ua mazungumzo yaoooo, wanajua hatuwezi kuthibitisha hayo!

Huu mchezo wa askari kuvamia guest usiku kwa kisingizi cha kupata taarifa kwa raia mwema niliwahi kuushuhudia Muheza. Waliingia saa 8 usiku wanaamsha watu wote na kuwasearch. Utaratibu huu unaweza kutumiwa na majambazi kuvamia guest kwa kujifanya polisi.

Kabla ya kufungua mlango wa chumba nitaaminije kuwa hao ni polisi na si mahambazi. Kwa kesi ya Muheza, walimuona mama mmoja wa kizungu jioni hiyo akipata kinywa ji na kijana mmoja na inaonekana uwalikuwa wanamfuatili huyo mama. Walidai nyaraka zake baada ya kwaamsha na rafiki yake.

mama wa kizungu akawaoutsmart. aliwaambia hawana mamlaka ya kumuhoji kwa njia waliyotumia. alikuwa na namba ya kiongozi wa Serikali na aliwaomba polisi wampe majina yao ili awaripot kwa kumnyanyasa.

Walikataa kutoa majina yao. Baada ya wapangaji wote wa guest kullamikia unyayansaji huo, polisi waliondoka. Nilikereka saana maana polisi hawakuwa na hata chembe ya ustaarabu.

Kuuliza wazoefu, wakaniambia wana mazoea ya kuwatisha wageni kwa lengo la kupata chochote, hivyo taarifa za uhalifu zilikuwa feki. Police mnajidhalilisha.
 
Kwamba mazungumzo yao yalionyesha (kwa mujibu wa bar maid) kuwa ni wahalifu. Halafu mlipovunja mlango mliwakuta na Bia moja moja walizokuwa wakinywa, mfuko wa mawe ya dhahabu na fedha taslimu Tshs. 500,000/=.

Ebo! Hawa ndio majambazi sugu? Hivyo "vifaa" mlivyowakuta navyo ndio vinatumika kufanyia ujambazi? Washitakiwe tu kwakuwa wao polisi ndio waligeuka majambazi kwenye tukio hili.

Na ili ujue hilo nenda kawaambie wakuonyeshe huo mfuko wa madini na hizo pesa kama bado wanavyo manake ni vielelezo. Wameshachakachua.
 
Amiri Jeshi Mkuu Dr Dr Dr Kikwete kawaamuru waue ,ameyasema hayo bila kumung,unya maneno kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwamba hawakuwa na kosa kumrarua mwangosi ,sasa unategemea message gani ametuma kwa polisi manake ni endelea kuua kwa kadri mupendavyo
 
Kwa uzoefu unapokwenda kukagua guest house lazima iende kamati ya ulinzi na usalama nikiwa na maana si lazima kamati yote but at least mwakilishi mmoja ambae ni raia na lazima awe mtumishi wa serikali, polisi si wa kuwaachia kufanya mambo wenyewe inapokuja suala la kwenda kufanya searching kwa watu na ndio maana ukienda mtaani wanatakiwa kwenda na kiongozi wa serikali za mtaa

hujui lolote kaa kimya kamat ya ulinz ndio,.!
 
Achen ukuda mbna polisi akiuawa hampigi kelele......jamii hamng'ak achen hzo.
 
Kuna siku kibao kitageuka na hakutakuwa na amani tena

Tusiendelee kusubiri hiyo siku huku tunamalizika inatakiwa na wewe ukikutana na police mtaani kwenye vichochoro tandika nondo au jiwe akipona bahati akifa halali yake!
 
Inaonekana hawa jamaa walikua majambazi kwa mujibu wa muhudumu wa gesti...Tena hata majina yao ni kama watu wa kigoma hawa..hakika ni majambazi wakutupwa hao wanatokea burundi na kuua watu Geita hongera raia wema kwa kuwapa kichapo manyangau hayo...Wamwambie zitto aanzishe jamhuri yao si walisema wanataka jamhuri ya wachawi wa kigoma...

Kwa hiyo,mtu kutokea Kigoma ndio tiketi ya kuwa jambazi na kustahili kifo?
My Take:Wewe ni kilaza.
Eliah G Kamwela says sorry for this very kilazaful post.
 
Tatizo ni kuto tii amri halali ya polisi. Kama wangeamriwa kufungua na wakafungua, pengine mambo yasingekuwa hayo. Pole kwa wote waliofikwa na msiba huo, na aliyetangulia kwenye haki, basi apumzike kwa amani. kwa sisi tuliobaki, let we learn to obey.
 
J

KAULI YA KAIMU RPC

Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Paulo Kasabago, mbali na kuthibitisha kuwapo kwa tukio hilo, alisema kuwa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa askari wake walienda kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaohofiwa kuwa ni wahalifu kutokana na mazungumzo yao wakati wakinywa pombe kabla ya kuingia ndani ya vyumba vyao.

“Askari wetu walikwenda eneo hilo baada ya kupigiwa simu na raia mwema kuwa watu waliokuwa wakinywa pombe kwenye gesti hiyo siyo wema kutokana na mazungumzo mbalimbali waliyokuwa wakiyazungumza kabla ya kuhama nje na kuingia ndani ya vyumba vyao,” alisema Kasabago.

Kufuatia hali hiyo jeshi hilo linawashikilia askari wake wanne akiwemo mkuu wa kituo hicho, Sajenti Raulens Bendera, kwa ajili ya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo la mauaji na kwamba itakapothibitika kuhusika, hatua za kisheria zitashika mkondo wake.
.

Kaimu kamanda tuambiae kama hawa mliodhani ni wahalifu waliwahi kufikishwa mahakamani? Tunajua sheria inawataka msimshikilie mtu bila kumfikisha mahakamani kwa zaidi ya saa 24.
 
hujui lolote kaa kimya kamat ya ulinz ndio,.!

Nielimishe mkuu si unajua kazi nyingi zinafanywa kwa mazoea, unaposema kaa kimya maana yake hauko tayari kumuelisha mtanzania mwenzako maana wengine huwa tunasafiri sana na huwa mara chache huwa tunakutana na hizi operation za misako guest house though wao hulenga zaidi wale ambao wanakuwa hawajafanya registration kwenye kitabu cha wageni ndio huanza nao kwanza wengine ni just kufanya verification. Kusema hujui kaa kimya sidhani kama ni hoja ulichotakiwa kuniulisha itanisaidia kufahamu haki yangu pindi nitapovamiwa na askari police napokuwa room. Kama wote wangekuwa wanajua nadhani tusingekuwa na bunge, baraza la madiwani, pia kusingekuwa na mikutano, makongamano pia kusingekuwa na JF maana mmoja akifikiria kwa niaba yetu inatosha lakini MIKUTANO, MAKONGAMANO na mitandao ya jamii mfano JF ipo kwa ajili ya ku-share uzoefu ili mawazo na uzoefu wa watu mbalimbali mkikaa pamoja mnatoka na kitu kizuri na ndio maana kuna JF ambayo ni HOME OF GREAT THINKER (sio lazima uwe na PHD hata STD 7 bado na wewe ni great thinker the way unavyo react kwenye issue mbalimbali). Kwa waliobahatika kuelimika katika kiwango cha kawaida huwa wanaamini kwenye uhuru wa kutofautiana hoja na ndio maana hata unapokuwa katika kusaka elimu unasoma idea za watu tofauti tofauti (philosophers) kuhusu mada flani kisha unakuja na hoja productive, unachotakiwa ni KUTIRIRIKA ili yule ambae HAJUI KITU afahamu.
 
Polisi njaa zinawasumbua sasa tutakuja kuwafundisha vipi S inavyoandikwa nyama hao na CCM wao
 
Nani atalinda raia wa nchi hii? Hawa askari kweli sio raia ndiyo maana wanaitwa asili kali . Mimi naona tuanze kujilinda kwa mbinu mpya. Kwanza, askari waende kwenye nchi yao iitwayo kambini. Waondoke uraiani.Kisha wakijitokeza uraiani tupige kelele. Wananchi tuwarushie mabomu ya mawe mpaka watupe silaha zao. Lakini bado ni raia tu,hawa jamaa!!! kIWETE USICHEKE NA HAWA ASILIKALI WAOVU!!!
 
Back
Top Bottom