Polisi waua tena mtuhumiwa mara

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa mara robert boaz alipoulizwa alisema marehemu alitoka na panga na kumshambulia PC sixbert kwa kukamata magazine na kumuangusha chini.Alisema PC rajabu alimpiga risasi mkononi,lakini marehemu aliendelea kutaka kumshambulia na kwamba ndipo PC huyo akampiga risasi ya mgongoni iliyo tokea kifuani na kumuua.
Huyu jambazi alikuwa anamshambulia polisi kwa style ya kimgongomgongo? Nilitaraji anayeshambulia apigwe kifuani lo!
 
Kwa hii habari, inanikumbusha hoja ya Mb wa zamani wa Shy mjini aliyesema Jeshi la Plosi livunjwe na kuundwa upya. Wengi hatukumwelewa lakini kwa vitendo vinavyoendelea sasa ni wazi kuwa hoja ya Mh DEREFA ilikuwa na mashiko.

Sasa kwa hili la Mara, RPC anasema mtuhumiwa, "jambazi" alitoka na panga na kumshambulia askari, Askari kuona hivyo akampiga risasi ya mkono. Anasema eti aliendelea kumfuata na ndipo akampiga risasi ya mgongoni ikatokea kifuani.

Kwa haraka haraka inaonyesha wazi kuwa huyo wanayemwita jambazi baada ya kupigwa hiyo risasi ya mkono aliamua kuondoka yaani aligeuka ili aondoke, na ndipo askari akamtwanga risasi tokea nyuma. Kwa sababu kama alikuwa anakabiriana naye angempiga risasi tokea kifuani na kutokea mgongoni.

Jamani vitu vingine vinasononesha sana. Lakini kama kawaida ya utendaji kazi wa serikali yetu, utasikia imeundwa tume kuchunguza kitu kama hicho, wakati maelezo ya RPC yako wazi, kwamba mtuhumiwa alipigwa risasi mgongoni, maana yake alikuwa anakimbia na wala alikuwa hakabiriani na askari wakati akipigwa risasi.
 
Nadhani kwa staili hii ya kuuwauwa tunatengeneza watu wenye chuki ambao kila siku watakuwa wanabuni namna ya kulipiza mwishoni watakuwa wengi tutapata kundi zuri tu la waasi na sio chama kama chadema nafikiri serikali inataka waasi,
 
Back
Top Bottom