Polisi waua na kuuawa huko Sumbawanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waua na kuuawa huko Sumbawanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lifeofmshaba, May 28, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MFUGAJI aliyeua polisi kwa mkuki wa kichwa, Hango Masanja (19) amefariki dunia usiku wa kuamkia jana, baada ya kuvuja damu nyingi kutokana na majeraha ya risasi sehemu zake za siri.

  Masanja anadaiwa alimpiga mkuki wa kichwa Sajenti Elikana Jumatano wiki hii, wakati polisi huyo na wenzake watatu walipokwenda kukutana na wafugaji waliokuwa wakituhumiwa kuvamia Kijiji cha Mfinga wakiambatana na maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutafuta suluhu kati ya wafugaji hao na wanakijiji.

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Sadun Kabuma alisema kuwa Masanja aliyekuwa amelazwa wodi namba tatu katika hospitali hiyo, alifariki saa saba usiku wa kuamkia jana kutokana na majerahamakubwa aliyopata mwilini mwake.

  Inadaiwa Sajenti Elikana baada ya kupigwa mkuki , polisi wanzake watatu waliokuwa wameambata naye katika kujihami walifyatua risasi na kujeruhi baadhi ya wananchi, akiwemo Masanja.

  Dk. Kabuma alisema, Masanja alipata majeraha makubwa sehemu ya makalio upande wa kushoto na sehemu zake za siri ziliharibika vibaya baada risasi kupiga maeneo hayo.

  “Ni kweli tulimpokea mgonjwa huyo akiwa amepigwa risasi makalio ya kushoto na kusambaza kabisa sehemu za siri… kitabibu nathibitisha kuwa kifo chake kimesababishwa na kuvuja kwa damu nyingi mwilini,” alisema Dk. Kabuma.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alisema Masanja ni miongoni mwa watuhumiwa wanne waliokamatwa katika msakounaendelea katika Kijiji cha Mfinga wilayani Sumbawanga ili kubainiwaliohusika katika mauaji ya polisi huyo.

  Kamanda Mantage alisema watuhumiwa wengine watatu, mmoja kati yao anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo huku wengine wakihojiwa, watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

  maoni yangu:
  hapo kwenye RED uwa siwaelewi polisi wa tanzania kwa nini wanaingia kwenye matukio yenye kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia , kwa nini viongozi wa vijiji wasitumike kuamanisha watu ili polisi wapate ushirikiano wakutosha kutoka kwa wananchi wao wenyewe hawawezi
   
 2. Banzi

  Banzi Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nitarudi rasmi
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,313
  Likes Received: 14,582
  Trophy Points: 280
  na mimi
   
 4. N

  Nguto JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kwa hapa sioni kama polisi tu ni wa kulaumiwa. Kosa liko pande zote mbili. Kwanini wafugaji walirusha mkuki? Hatuambiwi kama polisi ndio walioanza kuwapiga. Kama polisi ndio walioanza basi lawama zitupiwe kwao. Kama wafugaji ndio walianza kama tulivyosoma magazetini basi wafugaji na polisi wote wana makosa. Polisi hawakutakiwa kufyatua risai ovyo kwani aliyerusha mkuki ni mmoja tu kwanini wafyatue risasi kwa wananchi wasio na hatia???
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ...kabisa unaamini taarifa za kiintelijensia kuwa polisi walipofika tu kwenye hilo eneo hao wafugaji wakaanza kutupa mkuki na polisi ndio wakajibu mashambulizi?? Havent we heard all this many times before??
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  maoni yangu:
  hapo kwenye RED uwa siwaelewi polisi wa tanzania kwa nini wanaingia kwenye matukio yenye kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia , kwa nini viongozi wa vijiji wasitumike kuamanisha watu ili polisi wapate ushirikiano wakutosha kutoka kwa wananchi wao wenyewe hawawezi[/QUOTE]

  Kweli LM,
  Marazote ninashaka sana na mafunzo wanayopewa polisi wetu,
  Japo jeshi linachangamoto nyingi, lakini hapo ukiangalia utajiuliza lini Polisi wameanza "conflict resolution program"??
  Ni vigumu hilo jeshi kukwepa lawama.
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,932
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  RAIA kupiga polisi SAWAAAAAAAA......! polisi kujihami WANAKIUKA HAKI ZA BINADAMU....!
  YES! polisi wana madhaifu yao mengi tu.....tuyaite (CALL SPADE A SPADE) na pale ambapo wanafanyiwa visivyo napo tuite SPADE SPADE...!
   
 8. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,084
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  hii nchi imeharibika sasa, Polisi wawe makini, mbinu za zamani za vitisho kwa raia itaendelea kuwagharimu maisha yao
   
Loading...