Polisi waua majambazi 4 kati ya saba kahama

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
900
Polisi wilayani kahama wameua majambazi wanne kati ya saba waliokuwa wanijiandaa kufanya uvamizi. Habari zilizopatikana hapa kahama zinasema polisi walipigiwa simu na raia wema na walipofika eneo majambazi walipokuwa waliaanza kufyatuliana risasi na kufanikiwa kuwatoa uhai raia hao. Watu hao wameuwaa katikati ya barabara inayotoka kahama kueleke Kakola (bulyahyulu).
 
Kuna ushahidi gani kama watu hao ni majambazi na walikusudia kwenda kufanya uhalifu? Kwa nini hao polisi wasifanye subira kumshika mhalifu wakati akifanya uhalifu? Hii ya kushambulia na kuua watu barabarani kwa kuambiwa au kuchongewa na watu au mtu fulani haiakisi ukweli, inawezekana ni uhasama wa watu hao na hivyo kufikisha hatua za kuhasiniana. Polisi fanye kazi kwa kadiri ya maarifa yao na kutumia njia sahihi za kujengo hoja ya uhalifu wa mhusika. Shauri hili lilivyo halina ushahidi kama wahusika ni wahalifu.
 
Bila shaka source ni Chitambikwa mwenyewe.
Hongereni polisisiem kwa jitihada hiyo.
Lakini nataka kusema hawa police kwa mafunzo walionao hawana shabaha hata punje kwnn wale wengine wakimbie bila hata ya kujeruhiwa na wakati mmesomea kbs mambo ya silaha na hata shabaha!

Mi kwa hili la majambazi wengine kukimbia sijaridhika nao ingetakiwa wawe wamekimbia na majeraha hata ya kuacha ya mikono pale.

Lakini hongereni kidogo tu. 50%
 
Polisisiem haiaminiki
saaaana wanauwa raia
wanasema majambazi
pia wanaua majambazi
zen na wao wanakwapua
kilichokwapuliwa
na majambazi
sa sijui kwanini wanawauwa wenzaooo???
 
Polisisiem haiaminiki
saaaana wanauwa raia
wanasema majambazi
pia wanaua majambazi
zen na wao wanakwapua
kilichokwapuliwa
na majambazi
sa sijui kwanini wanawauwa wenzaooo???

kweli kabisa na ndio zao hizo kila siku watu wanapotea ghafla tu kumbe jamaa wamewaua..

RIP Eddy clux
 
Kuna ushahidi gani kama watu hao ni majambazi na walikusudia kwenda kufanya uhalifu? Kwa nini hao polisi wasifanye subira kumshika mhalifu wakati akifanya uhalifu? Hii ya kushambulia na kuua watu barabarani kwa kuambiwa au kuchongewa na watu au mtu fulani haiakisi ukweli, inawezekana ni uhasama wa watu hao na hivyo kufikisha hatua za kuhasiniana. Polisi fanye kazi kwa kadiri ya maarifa yao na kutumia njia sahihi za kujengo hoja ya uhalifu wa mhusika. Shauri hili lilivyo halina ushahidi kama wahusika ni wahalifu.

we una2mia nn kufikilia? Unadhan kazi ya polisi ni kubofya keyboard,unataka waulize nn? Wangekua raia wema wangewafyatulia polisi risasi? Try 2 be reasonable
 
Polisisiem haiaminiki
saaaana wanauwa raia
wanasema majambazi
pia wanaua majambazi
zen na wao wanakwapua
kilichokwapuliwa
na majambazi
sa sijui kwanini wanawauwa wenzaooo???

acha kuropoka! Unadhan risasi ni mbege?
 
Kuna ushahidi gani kama watu hao ni majambazi na walikusudia kwenda kufanya uhalifu? Kwa nini hao polisi wasifanye subira kumshika mhalifu wakati akifanya uhalifu? Hii ya kushambulia na kuua watu barabarani kwa kuambiwa au kuchongewa na watu au mtu fulani haiakisi ukweli, inawezekana ni uhasama wa watu hao na hivyo kufikisha hatua za kuhasiniana. Polisi fanye kazi kwa kadiri ya maarifa yao na kutumia njia sahihi za kujengo hoja ya uhalifu wa mhusika. Shauri hili lilivyo halina ushahidi kama wahusika ni wahalifu.

Soma habari kwa makini kabla ya kutoa hoja!!!! kwa faida yako habari inasema 1. raia wema walitoa taarifa polisi baada ya kuwabaini majambazi 2. Polisi walifika eneo lengwa 3. Polisi na majambazi walirushiana risasi - mwandishi hakubainisha nani alifyatua risasi ya kwanza lakini pande zote zilirusha risasi.

Hitimisho: Raia wema ambao wanamilki bunduki kihalali hawawezi kuwarushia polisi risasi. Polisi wanawajibu wa kuwakamata watuhumiwa bila ya kuhatarisha maisha yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom