Chadema yashuku mauaji majambazi Serengeti

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
572
2,549
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshuku mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya majambazi wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, kikitoa hoja nne kuthibitisha mashaka yake.

Mashaka hayo yanaibuka ikiwa ni karibu wiki moja tangu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Longinus Tibishuana aliporipoti kuwauwa watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi na mmoja kutokomea kusikojulikana.

Leo Jumanne Septemba 27, 2022, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, idadi ya watu wanaodaiwa kukamatwa katika oparesheni ya Polisi iliyohusisha mauaji hayo ni zaidi ya wanne.

"Tumefanya uchunguzi wetu kwa kuwahoji wanakijiji na uongozi wa Kijiji na tumepata taarifa kwamba waliokamatwa hawakuwa wanne kama inavyosema Polisi ni zaidi ya hao," amesema.

Amefafanua watu wengine waliachiwa baada ya kulipa fedha kati ya Sh1 milioni hadi Sh2.5 milioni walizotozwa na jeshi hilo baada ya kuwekwa kuzuizini.

Hata hivyo, amesema inatia shaka mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha kuachwa bila kufungwa pingu.
"Wanasema waliwajeruhi baada ya kutaka kukimbia walipofika porini kuonyesha walipokuwa majambazi wenzao na silaha, ina maana hawakuwa na Pingu," amehoji.

Hata mauaji, Kigaila amesema Mwenyekiti wa Kijiji (David Mugendi) ameeleza yamefanyika saa 9 alfajiri eneo lilipo rambo la kunyweshea mifugo, sio porini kama inavyoelezwa na Polisi.

Kutokana na mashaka hayo, Kigaila ametaka Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Massauni.

Wengine aliotaka wafutwe kazi ni uongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mara, ili kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo.

Pia, amemtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kufanya uchunguzi wa tukio hilo, akisema wanakijiji wapo tayari kutoa ushahidi.

Chanzo: Mwananchi
 
Eti amemtaka Rais Samia 😠😠.... Nyambaf kabisa. Acheni kuingiza siasa kwenye maswala nyeti ya ulinzi na USALAMA. Wahubirini Wananchi wafuate Sheria waache uhalifu. Hii maneno ya kuvizia matukio hamuwezi kupata umaarufu tena.
 
Eti amemtaka Rais Samia .... Nyambaf kabisa. Acheni kuingiza siasa kwenye maswala nyeti ya ulinzi na USALAMA. Wahubirini Wananchi wafuate Sheria waache uhalifu. Hii maneno ya kuvizia matukio hamuwezi kupata umaarufu tena.
Inasikitisha sana ccm mnavyokosa utu kiasi hicho.

Haki huinua taifa, kama jambazi amekamatwa si apelekwe kunakostahili?
Kwanini umkamate mtu na umuue?

Ikiwa ni eneo la tukio na jambazi ana silaha hilo la askari kujihami kwa kumpiga risasi inaruhusiwa kisheria na sio kumkamata na kuua
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshuku mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya majambazi wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, kikitoa hoja nne kuthibitisha mashaka yake.

Mashaka hayo yanaibuka ikiwa ni karibu wiki moja tangu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Longinus Tibishuana aliporipoti kuwauwa watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi na mmoja kutokomea kusikojulikana.

Leo Jumanne Septemba 27, 2022, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, idadi ya watu wanaodaiwa kukamatwa katika oparesheni ya Polisi iliyohusisha mauaji hayo ni zaidi ya wanne.

"Tumefanya uchunguzi wetu kwa kuwahoji wanakijiji na uongozi wa Kijiji na tumepata taarifa kwamba waliokamatwa hawakuwa wanne kama inavyosema Polisi ni zaidi ya hao," amesema.

Amefafanua watu wengine waliachiwa baada ya kulipa fedha kati ya Sh1 milioni hadi Sh2.5 milioni walizotozwa na jeshi hilo baada ya kuwekwa kuzuizini.

Hata hivyo, amesema inatia shaka mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha kuachwa bila kufungwa pingu.
"Wanasema waliwajeruhi baada ya kutaka kukimbia walipofika porini kuonyesha walipokuwa majambazi wenzao na silaha, ina maana hawakuwa na Pingu," amehoji.

Hata mauaji, Kigaila amesema Mwenyekiti wa Kijiji (David Mugendi) ameeleza yamefanyika saa 9 alfajiri eneo lilipo rambo la kunyweshea mifugo, sio porini kama inavyoelezwa na Polisi.

Kutokana na mashaka hayo, Kigaila ametaka Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Massauni.

Wengine aliotaka wafutwe kazi ni uongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mara, ili kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo.

Pia, amemtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kufanya uchunguzi wa tukio hilo, akisema wanakijiji wapo tayari kutoa ushahidi.

Chanzo: Mwananchi
Nakubaliana na Kigaila mara Milioni moja. Huyo binti Mwese aliyebakwa na Polisi hadharani jamani inakuwaje tena. Najisikia uchungu sana kwa uonevu wa aibu. Mhe. Samia Suluhu Hassan, nakuomba sana chukua hatua madhubuti sasa. Hii ni aibu kwa nchi yetu, laana kuu mbele ya Mwenyezi Mungu Muumba wetu. Tafadhalini tuchukue hatua stahiki sasa. Hatuwezi kuwa wapole mpaka tunaltiwa vidole puani. Polisi wa aina hii ni zaidi ya Panya Road. Ujambazi haukubaliki, hali kadhalika mauaji kiholela hayakubaliki. Nao ubakaji haukubaliki.
 
Hoja ya Polisi ya ''.... majambazi yalijeruhiwa wakati wa kuonyesha walipo wenzao au silaha' imetumika miaka mingi sana. Kama ndivyo inavyotokea basi tuna jeshi la Polisi la ajabu sana kwasababu hizi;

1. Mtuhumiwa yoyote huwekwa chini ya ulinzi na PINGU ili kuepuka kutoroka au kuleta madhara

2. Hivi inakuwaje Polisi watembee na Mtuhumiwa wa UJAMBAZI kama vile wanakwenda sokoni?

Kauli ya kwamba walijaribu kutoroka au walikimbia ina maana walijaribu wakiwa na PINGU.

Huyo jambazi sijui atakuwa na akilini gani kuweza kukimbia na pingu mkononi na hakika hatakiwi kupigwa risasi bali kufanyiwa uchunguzi wa akili.

Haiingiii akilini hata kwa mtoto wa darasa la kwanza kwamba mtu anapingu halafu anajaribu kukimbia!!!.

Kauli hii ambayo imekuwa kama ''kauli mbiu' kila wanapotaka 'kuhalalisha matumizi ya silaha

Si kwamba inawadhalilisha katika weledi lakini pia inaacha jeshi letu la Polisi lichekwe duniani na kuwa kituko.

Polisi wanaotembea na mtuhumiwa tena wa Ujambazi bila PINGU hawafai kuvaa Uniform hata kwa dakika moja

JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla MALCOM LUMUMBA
 
Jeshi letu la police ni majambazi in uniforms, suspect anapokimbia away from crime scene huruhusiwi kumpiga risasi bcs sio threat kwa mtu yeyote,police kisheria anaruhusiwa kutumia deadly force once maisha ya raia au yake yanapokua hatarini sio vinginevyo, police ni dept iliyogubikwa na rushwa kuliko zote serikalini na trust ya wananchi towards them its at lowest level, prove me wrong
 
Eti amemtaka Rais Samia 😠😠.... Nyambaf kabisa. Acheni kuingiza siasa kwenye maswala nyeti ya ulinzi na USALAMA. Wahubirini Wananchi wafuate Sheria waache uhalifu. Hii maneno ya kuvizia matukio hamuwezi kupata umaarufu tena.
stupid burger!
 
Samia kama Magufuli, kumwaga damu ndio mafanikio yao
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshuku mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya majambazi wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, kikitoa hoja nne kuthibitisha mashaka yake.

Mashaka hayo yanaibuka ikiwa ni karibu wiki moja tangu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Longinus Tibishuana aliporipoti kuwauwa watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi na mmoja kutokomea kusikojulikana.

Leo Jumanne Septemba 27, 2022, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, idadi ya watu wanaodaiwa kukamatwa katika oparesheni ya Polisi iliyohusisha mauaji hayo ni zaidi ya wanne.

"Tumefanya uchunguzi wetu kwa kuwahoji wanakijiji na uongozi wa Kijiji na tumepata taarifa kwamba waliokamatwa hawakuwa wanne kama inavyosema Polisi ni zaidi ya hao," amesema.

Amefafanua watu wengine waliachiwa baada ya kulipa fedha kati ya Sh1 milioni hadi Sh2.5 milioni walizotozwa na jeshi hilo baada ya kuwekwa kuzuizini.

Hata hivyo, amesema inatia shaka mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha kuachwa bila kufungwa pingu.
"Wanasema waliwajeruhi baada ya kutaka kukimbia walipofika porini kuonyesha walipokuwa majambazi wenzao na silaha, ina maana hawakuwa na Pingu," amehoji.

Hata mauaji, Kigaila amesema Mwenyekiti wa Kijiji (David Mugendi) ameeleza yamefanyika saa 9 alfajiri eneo lilipo rambo la kunyweshea mifugo, sio porini kama inavyoelezwa na Polisi.

Kutokana na mashaka hayo, Kigaila ametaka Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Massauni.

Wengine aliotaka wafutwe kazi ni uongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mara, ili kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo.

Pia, amemtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kufanya uchunguzi wa tukio hilo, akisema wanakijiji wapo tayari kutoa ushahidi.

Chanzo: Mwananchi
CHADEMA wanatumia nguvu kubwa kujinasua kwa sababu baadhi ya majambazi hawo ni ndugu wa wajumbe wa Kamati Kuu walioshiriki kuwafikisha huko kwa ufadhili wao.
 
Polisi ni majambazi yaani wao kazi ya mahakama wanafanya wao, Ivi kweli kama walikuwa na ushahidi wa kutosha kwa nini wasipelekwe mahakamani yaani uchukuwe polisi bila hata balozi, majirani au mwenyekiti wa eneo husika eti mwende polini na watuhumiwa halafu mnawaua then mnakuja kusema walitaka kukimbia? Mbona isiwe kuvunjwa miguu ili mtuhumiwa abakie hai na kesi yake iwepo au huko CCP Moshi ndo wanafundisha mauaji tu kwa vijana wao wa polisi ? yaani option ya mwisho kabisa kwa polisi ni kuua kisa ana SMG
 
Eti amemtaka Rais Samia .... Nyambaf kabisa. Acheni kuingiza siasa kwenye maswala nyeti ya ulinzi na USALAMA. Wahubirini Wananchi wafuate Sheria waache uhalifu. Hii maneno ya kuvizia matukio hamuwezi kupata umaarufu tena.
Acha ujinga.watu wenye akili wanaongelea mambo ya msingi ya nchi wewe unawaza siasa.siasa zina maana gani wakati silaha zinatumiwa ovyo na taasisi zenye mamlaka zakuheshimu sheria.Siasa zinakuaga na mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom