Polisi watanda kwa Mo Dewji

Polisi watanda kwa Mo Dewji

Baada ya sakata la kutekwa kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemuongezea ulinzi mfanyabiashara huyo
View attachment 910312
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa katika mahojiano yake na www.eatv.tv amesema kuwa wamemwongezea ulinzi mfanyabiashara huyo katika kipindi hiki ambacho bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio.

"Katika kipindi hiki ambacho bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwake, tumemuongezea ulinzi", amesema Mambosasa.

Mo Dewji alitekwa Alfajiri ya Oktoba 11, katika hoteli ya Colosseum iliyopo Osterbay jijini Dar es salaam na kupatikana baada ya siku tisa katika maeneo ya Gymkhana alikotelekezwa na watekaji, huku pia wakitelekeza gari aina ya Toyota Surf walilolitumia likiwa na silaha kadhaa za moto.
Huu ni unafiki wa kichawi
 
Hapa utakuta jamaa hata passport kanyanganya na hatakiwi kutoka nje ya nchi. Huu ulinzi wanaosema ni wakumbana asiseme wala asiongee na vyombo vya habar kile kilichomkuta.
YAN TUNANEEMEKA KULIPA KODI ILA ZINATUMIKA KUTUNEENESHA PIA.
 
Hivi Mo aliokolewa na polisi au alirudishwa na walewale watekaji wenye huruma, waliokuwa wakipa misosi yote aliyokuwa akihitaji?

Huu ulinzi hauna maana yoyote na ni matumizi mabaya ya rasilimali zetu.
 
wanamlinda asiseme anayoyajua kuhusu kukamatwa kwake
 
Naye Mo kaona isiwe noma, kaamuwa kujifungia na kupiga tizi home tu! isije ikawa yale yale mwaya...🙂😀😎

Hivi kweli na kijifua kwote huku Bw. Mo alishindwa kabisa kuwapa vitasa vya Kisingida wale wahuni?!
 
kama hamkuweza kumuokoa mtawezaje kumlinda?
Maana katekwa wiki nzima.mpaka wakaamua kumrudisha wenyewe.
Inachekesha.
 
wanamlinda asiseme anayoyajua kuhusu kukamatwa kwake

Ulinzi gani huo? kwa kutumia kodi zetu kumlinda Bilionea? je mabilionea wengine kama Bakhresa, Mengi, Sabodo, Manji, Subash Patel, Nauresh etc nao watalindwa kama Mo kwa kutumia kodi zetu?
 
Ukitema nchale na ukimeza ni nchale..

MTU kati
 
Back
Top Bottom