Polisi watanda kwa Mo Dewji

Polisi watanda kwa Mo Dewji

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,492
Baada ya sakata la kutekwa kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemuongezea ulinzi mfanyabiashara huyo
DqWA3ZsWkAAnKnf.jpg

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa katika mahojiano yake na www.eatv.tv amesema kuwa wamemwongezea ulinzi mfanyabiashara huyo katika kipindi hiki ambacho bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio.

"Katika kipindi hiki ambacho bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwake, tumemuongezea ulinzi", amesema Mambosasa.

Mo Dewji alitekwa Alfajiri ya Oktoba 11, katika hoteli ya Colosseum iliyopo Osterbay jijini Dar es salaam na kupatikana baada ya siku tisa katika maeneo ya Gymkhana alikotelekezwa na watekaji, huku pia wakitelekeza gari aina ya Toyota Surf walilolitumia likiwa na silaha kadhaa za moto.
 
Baada ya sakata la kutekwa kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemuongezea ulinzi mfanyabiashara huyo
View attachment 910312
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa katika mahojiano yake na www.eatv.tv amesema kuwa wamemwongezea ulinzi mfanyabiashara huyo katika kipindi hiki ambacho bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio.

"Katika kipindi hiki ambacho bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwake, tumemuongezea ulinzi", amesema Mambosasa.

Mo Dewji alitekwa Alfajiri ya Oktoba 11, katika hoteli ya Colosseum iliyopo Osterbay jijini Dar es salaam na kupatikana baada ya siku tisa katika maeneo ya Gymkhana alikotelekezwa na watekaji, huku pia wakitelekeza gari aina ya Toyota Surf walilolitumia likiwa na silaha kadhaa za moto.

Watasema wanamlinda, lakini mimi nafikiri wanamlinda ili hasitoe siri za waliomteka na si vinginevyo.
wanazidi kumtia mawazo maana hana uhuru wa kufanya anayotaka.

TANZANIA UKITAKA KUPEWA ULINZI NA SERIKALI, BASI KUBALI UTEKWE
 
Back
Top Bottom