Polisi wasumbuka na mishahara yao

mataka

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
286
61
Ndg zangu wanajf jana niliona polisi wanaponda utaratibu mpya wa kuingiza salary zao kupitia bank ya NMB. Eti wengine wamepata kitambo na wengine mpaka leo hakieleweki na kutrace kujua mshahara uko wapi eti ni ngumu. Walikuwa wamenuna kweli mpaka nikaogopa nikaondoka wasije kunipa kesi!
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa! na jinsi walivyo wagumu wa kufikiri, lazima wangekutafutia kesi kweli!
 
Taratibu wataelewa kuwa sisi tunaolia daily na kupigwa virungu sio wajinga, tuna sababu za kufanya hivyo
 
Nidhamu ya woga na inferiority complex ndiyo tatito kubwa sana kwa hawa askari polisi wetu, yaani wanatakiwa kuingia barabarani tuu kudai haki yao ni si vinginevyo
 
Siyo polisi tu, kwani hali hii ni kwa wafanyakazi wengi, hata walimu wengine wamepata, wengine bado. Kazi ipo. Bora imewagusa na wao wajue maana ya 'maandamano" ya kudai haki.
 
Taratibu wataelewa kuwa sisi tunaolia daily na kupigwa virungu sio wajinga, tuna sababu za kufanya hivyo
Hatimaye kisu kinakaribia kufika kwenye mfupa. Walipwe baada ya tarehe 12/11/2011 ili kisu kiwe kimefika mfupani. Wapi washawasha..
 
Hata wasipopewa hao hamna hasara,c huwa wanawasuport hao magamba.
 
Acheni uzushi askari wote tushalipwa mishahara jamaa zangu askari wengi tumeshalipwa nyie cjui vp mbna mnazusha hivyo!!
 
Ndg zangu wanajf jana niliona polisi wanaponda utaratibu mpya wa kuingiza salary zao kupitia bank ya NMB. Eti wengine wamepata kitambo na wengine mpaka leo hakieleweki na kutrace kujua mshahara uko wapi eti ni ngumu. Walikuwa wamenuna kweli mpaka nikaogopa nikaondoka wasije kunipa kesi!
Matatizo kama haya siyo tu polisi yanaweza kutokea bali idara yoyote ile ambayo watumishi wake walikuwa wanapata kwenye payroll na kisha kuingizwa bank kwa sababu zifuatazo;
  1. Kukosewa kwa aidha check number au akaunti.
  2. Kuwasilisha domant akaunt n.k
Kwa kuwa polisi walikuwa wanapokelea kwenye payroll basi matatizo hayo ni ya kawaida kabisa. Hoja ya msingi niliyofikiri kwangu ni kuwa serikali hadi saizi haijalipa jeshi la polisi mshahara hapo ningesema kidogo ngoja waonje joto ya jiwe lakini kumbe ni makosa ya idara yenyewe hiyo siyo issue sana.
 
Acheni uzushi askari wote tushalipwa mishahara jamaa zangu askari wengi tumeshalipwa nyie cjui vp mbna mnazusha hivyo!!
Mshikaji mjeda nini? Nitashangaa ukiruka kimanga wakati statement yako sehemu niliyo bold inajieleza!
 
Back
Top Bottom