Polisi wasaka mchawi sakata la Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wasaka mchawi sakata la Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe


  Baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kusema ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, hautokani na kulishwa sumu, Jeshi la Polisi limeanza kumsaka mchawi aliyeibua madai hayo ili ashtakiwe mahakamani.

  Kati ya wanaohofiwa kwamba wanaweza kukumbwa kushtakiwa kwa tuhuma hiyo, ni ama Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, au Dk. Mwakyembe mwenyewe.
  Mchakato wa kumtafuta mchawi katika suala hilo unatokana na uamuzi uliochukuliwa na

  Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi wa suala hilo na kupeleka jalada la mashtaka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).
  DPP amepelekewa jalada hilo ili aamue kama wanaotoa taarifa kwamba Dk. Mwakyembe alilishwa sumu washtakiwe mahakamani au la.Hatua hiyo imechukuliwa na Jeshi hilo zikiwa zimepita siku chache tangu DCI Manumba, kueleza kuwa ugonjwa unaomsumbua Dk.

  Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu.
  Msemaji wa Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo (ASP), Advera Senso, akizungumza na NIPASHE jana ofisini kwake, alithibitisha kupelekwa kwa jalada hilo kwa DPP.Hata hivyo, Senso hakuwa tayari kueleza kwa kina

  wanaotuhumiwa katika jalada hilo kutoa taarifa kuhusu Dk. Mwakyembe kulishwa sumu.
  Wakati Senso akisita kutaja wanaotuhumiwa katika jalada hilo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekuwa akitamka hadharani kuwa ugonjwa unaomsumbua

  Dk. Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu.
  Kutokana na kauli hiyo ya Waziri Sitta, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, pamoja Jeshi la Polisi mara kadhaa wamekuwa wakinukuliwa na vyombo vya habari wakimtaka Sitta kupeleka ushahidi

  unaoonyesha kuwa Dk. Mwakyembe amelishwa sumu.
  Sitta amekuwa akieleza hivyo katika mikutano yake kadhaa ikiwemo anayoalikwa makanisani. Siku moja baada ya Manumba kukanusha madai juu ya Dk. Mwakyembe kulishwa sumu, Naibu Waziri huyo alilishambulia Jeshi la Polisi kwa kueleza kuwa lina ufinyu wa uelewa.Dk. Mwakyembe alisema kulishwa sumu si lazima mtu anyweshwe ili imdhuru

  wakati inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.
  Alisema Jeshi la Polisi limejiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.


  CHANZO: NIPASHE

   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nothing is new in this same story, same same!
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hili Jeshi la polisi linafurahisha sana, hivi Dr. Mwakyembe aliishutumu serikali au anatuhumu kikundi cha watu kumlisha sumu? Inakuwaje linashupalia kufungua kesi kwa nini watuhumiwa wasifungue wao kesi ya madai? Kama ni hoja ya watu kuwatuhumu wengine zipo tuhuma nyingi tu mitaani na wafikirie kufungua kesi pia.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 4. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  As I have been always telling my JF members there is strong commitment of these two police speakers they both aim at maintaining some status ahead of the time. I could call it as corruptiob of office responsibilies. Both deserved persecution in serious government but not this corrupt country.
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inshu ya Dr mwakyembe imekuwa ndo ya kuuzia magazeti sasa. Hakuna kipya ktk habari hii. shame on you Nipashe ktk hili! matokeo ya waandishi wavivu
   
 6. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unatujazia post zisizo na mbele wa nyuma
   
 7. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Polisi wa Tanzania nyambafu kabisa.
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndo akome kuwa na nyumba ndogo tabata.....network search.....
   
 9. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wachawi wao wenyewe!! Kutuletea statement za uongo....washazoea kuburuzwa watu na mambo yao Yale ya kubambikia kesi....sasa wakaonelea waje na uzushi Huu. Timing imekataa safari hii
   
 10. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna polisi majambazi - Samuel Sitta ..... Nakubaliana nawe,kwa kubambikia kesi jamaha awajambo
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Yeaaah! The source is reliable, but why the investigation do not start from the source too?
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Tunajua Mwema na jeshi lake wanamtumikia nani!
   
 13. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kinachofurahisha mpaka hapa ni ukweli kuwa mchezo huu sasa unawarudi waliouasisi. Dr. Mwakyembe alipoongoza kamati teule ya bunge kuandaa ripoti ya nusu-ukweli alidhani anaisaidia serikali. Lakini sasa imemgeuka.
  Aliyekuwa spika wa bunge. Samwel sitta alipozima mjadala wa richmond kwa rungu lake kuu alhdhani anaisaidia serikali. Kumbe sivyo leo inamwona mwongo na mzushi. Naona sasa yanatimia.
   
Loading...