Polisi wapambana na wananchi, waua mmoja

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
MWANAUME mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika vurugu za wananchi zilizotokea katika Kijiji cha Wegero, Musoma Vijijini.

Vuguru hizo zilitokana na wananchi kuwashtumu polisi kwamba wamemwachia mmoja wa watuhumiwa wa mauaji mwananchi mwenzao aliyemchomwa kisu.

Kamanda wa polisi mkoani Mara, Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni katika Kijiji cha Wegero na kwamba aliyeuawa kwa kupigwa risasi ni Mgoyo Mgoyo, mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda Boaz alisema a mtu huyo aliuawa kwa bahati mbaya katika jitihada za askari polisi kujihamini dhidi ya kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakishambulia kwa mawe.

Alisema katika tukio hilo askari polisi walipofyatua risasi hewani na kwa bahati mbaya moja ilimpata mtu huyo na kupoteza maisha.

“Mtu huyo ameuawa kwa bahati mbaya katika jitihada za polisi kujihami kwa kufyatua risasi hewani. Zilikuwa vurugu kubwa maana wananchi walikuwa na jazba sana na walikuwa na silaha za jadi kama mawe ambayo waliyatumia kuwashambulia askari," alidai.

Alisema kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya uvumi kwamba mwananchi mmoja anayeshikiliwa na polisi kwa tuhuma ya mauaji ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, aliyeuawa Desemba 26 mwaka jana kwa kumchoma na kisu ameachiwa huru, baada ya ndugu zao kuwaonga polisi.

Alisema kufuatia uvumi huo wananchi walikwenda nyumbani kwa ndugu wa mtuhumiwa na kubomoa nyumba zipatazo 12, na kuteketeza maghala ya chakula na mabanda ya mifugo kwa madai kuwa wao ndio walioonga pesa polisi ili kuwezesha ndugu yao kuachiwa.

Kamanda huyo alisema kufuatia vurugu hizo, uongozi wa Wilaya ya Musoma ulimtuma Ofisa Tarafa kwenda katika eneo la tukio, lakini alipofika wananchi walimfukuza, hatua iliyomlazisha kutoa taarifa polisi.

Alisema hata hivyo polisi walipokwenda katika kijiji hicho nao walishambuliwa kwa mawe na kusababisha gari moja ya polisi kuvunjwa tata na vioo huku skari mmoja aiwa amejeruhiwa.

“Kutokana na vurugu hizo polisi walilazimika kuondoka katika katika eneo wakiwa wamewachukuwa baadhi ya viongozi hao na kuwapeleka mahabusu," alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuteketeza nyumba za wananchi wenzao katika kipindi kisichozidi wiki moja.

Hivi karibuni wananachi wa Kijiji cha Mwibagi, Musoma Vijijini, waliziteketeza nyumba zaidi ya 15 za familia sita tofauti, wakazi wa kijiji hicho, wakiwatuhumu kuwa ni washirikina na majambazi.
Chanzo.
Polisi wapambana na wananchi, waua mmoja
 
Tatizo polisi wetu hawaaminiki, ni kweli wapo watuhumiwa wanaachiwa kwa mlungula japo inawezekana huyu hakuachiwa kiivo bali hali ya kutoaminiana tu, na polisi jamii eneo hilo zero
 
Hicho ndicho tunachopata kwa kuwa na system iliyooza juu mpaka chini. Apumzike salama huyo aliyepoteza maisha yake.
 
Sasa kama polisi nao wanafanya kazi zao kwa mtindo wa kiharamia utawasaidiaje? Ulinzi shirikishi hauwezekani TZ kama polisi wenyewe hawashirikishi raia katika kazi zao kwa dhati. Ni sawa na dereva wa daladala anayegombania abiria kwa kuwakanyaga waliopo kituoni ajaze kipanya chake. Nani atapanda kipanya hicho?
 
Risasi zilipigwa juu kwa hiyo marehemu alikuwa juu ya mti? Anyways mimi napita tu!
 
Risasi za siku hizi ni korofi sana,zinapigwa juu halafu zenyewe zinaua chini....
 
Back
Top Bottom