Polisi waonya wachochezi wamponda mbowe

baraka boki

Senior Member
Sep 20, 2010
181
80
SOURCE;HABARI LEO
Imeandikwa na Hellen Mlacky; T

JESHI la Polisi nchini limewataka watu wenye uchu wa madaraka kusubiri uchaguzi wa mwaka 2015 na si kupotosha umma kwa kufanya uchochezi.

Aidha, limewaonya wananchi kutokubali shinikizo la kwenda kufanya makosa au vurugu na badala yake waheshimu utawala wa sheria.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano uliolenga kutoa taarifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya nchini.

Akijibu swali kuhusu hatua zilizochukuliwa na Polisi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, alisema lazima utawala wa sheria uheshimiwe na kuwataka wananchi waepuke upotoshaji wa makusudi wa mambo kwa maslahi ya kisiasa.

“Nawaambia Watanzania wasikubali kutumiwa na mtu mwenye uchu wa madaraka kwa sababu sisi tumepewa madaraka na yeyote atakayeleta uchochezi hatutamwonea aibu.

“Mtu anayetaka madaraka tungojeane mwaka 2015 kinyume cha hapo ni uchochezi na Polisi itakapochukua hatua, na mtu asiseme ameonewa maana amechimba shimo mwenyewe na ataliingia mwenyewe”.

Alisema, kitendo alichokifanya Mbowe kinauonesha umma wa Watanzania udhaifu alionao na kueleza kuwa, kiongozi wa aina hiyo ni wa kuogopwa, kwa sababu atakuwa analea wananchi wake katika misingi ya kuvunja sheria.

Akifafanua kuhusu sheria inayomkinga mbunge dhidi ya kukamatwa, akiwa katika shughuli za Bunge, Chagonja alisema inamaanisha kwamba Mbunge huyo anatakiwa awe ndani ya viwanja vya Bunge na awe ametenda kosa hilo ndani ya Bunge na si nje.

Arnold Swai, anaripoti kutoka Moshi kwamba vyama vya siasa vimetakiwa kuheshimu na kutii maagizo yanayotolewa na Serikali ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani.

Rai hiyo ilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati akizindua Mfuko wa Tamasha la maombi ya kumshukuru Mungu kwa amani ya Tanzania lililofanyika mjini humo.

Balozi Idd alisema, baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikijichukulia uamuzi bila kufuata maagizo ya viongozi wa Serikali hali inayowachonganisha wananchi na Serikali.

“Sheria na taratibu za nchi zipo ili zifuatwe, pia viongozi walioko madarakani wanapaswa kuheshimiwa na kusikilizwa … suala la kujichukulia uamuzi wako tofauti na agizo la Serikali ni kukiuka taratibu za nchi,” alisema Balozi Idd.

Katika hatua nyingine alisema nchi imwekwa doa kutokana na watu wachache kudai kuwa haitatawalika na kuapa kwamba watamwaga damu hadi haki ipatikane, hali ambayo inawafanya wananchi wakose amani.

Alisema viongozi wanaochochea maandamano wamekuwa chanzo cha kuvunja amani ya Watanzania na hivyo Serikali kwa kushirikiana na dini zote nchini, itahakikisha inaimarisha amani ili kujenga Taifa adilifu.

Hellen Mlacky anaripoti kutoka Dar es Salaam, kwamba Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amewahadharisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kutotumia vijana kama chambo cha uchochezi hata kuvunja amani ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kova alisema baadhi ya viongozi wa vyama wamekuwa wakichochea vijana kuingia mitaani kufanya fujo kwa madai kuwa wanadai haki yao ya kikatiba.

“Kutokana na hilo, Jeshi la Polisi haliko tayari kuvumilia tabia hii na tutachukua hatua kali kwa yeyote atakayehusika kuhamasisha au kuchochea vijana kuleta machafuko nchini,” alisema Kova.

Akitolea mfano wa fujo za juzi zilizochochewa na viongozi wa juu wa Chadema kuhamasisha vijana kuingia mitaani wakiwa wamevaa fulana na mabango yenye ujumbe unaochochea nchi kuingia katika machafuko ya umwagaji damu, ambapo alisema Polisi haitavumilia vitendo hivyo.
 
SOURCE;HABARI LEO
Imeandikwa na Hellen Mlacky; T

JESHI la Polisi nchini limewataka watu wenye uchu wa madaraka kusubiri uchaguzi wa mwaka 2015 na si kupotosha umma kwa kufanya uchochezi.

Aidha, limewaonya wananchi kutokubali shinikizo la kwenda kufanya makosa au vurugu na badala yake waheshimu utawala wa sheria.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano uliolenga kutoa taarifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya nchini.

Akijibu swali kuhusu hatua zilizochukuliwa na Polisi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, alisema lazima utawala wa sheria uheshimiwe na kuwataka wananchi waepuke upotoshaji wa makusudi wa mambo kwa maslahi ya kisiasa.

"Nawaambia Watanzania wasikubali kutumiwa na mtu mwenye uchu wa madaraka kwa sababu sisi tumepewa madaraka na yeyote atakayeleta uchochezi hatutamwonea aibu.

"Mtu anayetaka madaraka tungojeane mwaka 2015 kinyume cha hapo ni uchochezi na Polisi itakapochukua hatua, na mtu asiseme ameonewa maana amechimba shimo mwenyewe na ataliingia mwenyewe".

Alisema, kitendo alichokifanya Mbowe kinauonesha umma wa Watanzania udhaifu alionao na kueleza kuwa, kiongozi wa aina hiyo ni wa kuogopwa, kwa sababu atakuwa analea wananchi wake katika misingi ya kuvunja sheria.

Akifafanua kuhusu sheria inayomkinga mbunge dhidi ya kukamatwa, akiwa katika shughuli za Bunge, Chagonja alisema inamaanisha kwamba Mbunge huyo anatakiwa awe ndani ya viwanja vya Bunge na awe ametenda kosa hilo ndani ya Bunge na si nje.

Arnold Swai, anaripoti kutoka Moshi kwamba vyama vya siasa vimetakiwa kuheshimu na kutii maagizo yanayotolewa na Serikali ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani.

Rai hiyo ilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati akizindua Mfuko wa Tamasha la maombi ya kumshukuru Mungu kwa amani ya Tanzania lililofanyika mjini humo.

Balozi Idd alisema, baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikijichukulia uamuzi bila kufuata maagizo ya viongozi wa Serikali hali inayowachonganisha wananchi na Serikali.

"Sheria na taratibu za nchi zipo ili zifuatwe, pia viongozi walioko madarakani wanapaswa kuheshimiwa na kusikilizwa … suala la kujichukulia uamuzi wako tofauti na agizo la Serikali ni kukiuka taratibu za nchi," alisema Balozi Idd.

Katika hatua nyingine alisema nchi imwekwa doa kutokana na watu wachache kudai kuwa haitatawalika na kuapa kwamba watamwaga damu hadi haki ipatikane, hali ambayo inawafanya wananchi wakose amani.

Alisema viongozi wanaochochea maandamano wamekuwa chanzo cha kuvunja amani ya Watanzania na hivyo Serikali kwa kushirikiana na dini zote nchini, itahakikisha inaimarisha amani ili kujenga Taifa adilifu.

Hellen Mlacky anaripoti kutoka Dar es Salaam, kwamba Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amewahadharisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kutotumia vijana kama chambo cha uchochezi hata kuvunja amani ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kova alisema baadhi ya viongozi wa vyama wamekuwa wakichochea vijana kuingia mitaani kufanya fujo kwa madai kuwa wanadai haki yao ya kikatiba.

"Kutokana na hilo, Jeshi la Polisi haliko tayari kuvumilia tabia hii na tutachukua hatua kali kwa yeyote atakayehusika kuhamasisha au kuchochea vijana kuleta machafuko nchini," alisema Kova.

Akitolea mfano wa fujo za juzi zilizochochewa na viongozi wa juu wa Chadema kuhamasisha vijana kuingia mitaani wakiwa wamevaa fulana na mabango yenye ujumbe unaochochea nchi kuingia katika machafuko ya umwagaji damu, ambapo alisema Polisi haitavumilia vitendo hivyo.

Tamko kama hilo definetely mwenye akili aliyekwenda shule analitegemea kutoka Jeshi la polisi. We know Police etc are the instruments of oppression, here to sustain a state (Is a LEAD instrument of oppression), the ruling class to exploit the mass
 
Back
Top Bottom