Polisi wanaswa na meno ya tembo

Polisi wanaswa na meno ya tembo

smigon

Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
8
Reaction score
0
WATU tisa wakiwamo askari polisi wawili wa Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam wametiwa mbaroni wakiwa na meno 70 ya tembo (sawa na tembo 35).


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, watuhumiwa hao walikamatwa Julai 28, mwaka huu usiku saa nne katika kizuizi cha Kauzeni, Kata ya Vikumbulu, wilayani Kisarawe wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 357 ABK aina ya Toyota Surf.


Aliwataja askari hao kuwa ni Senga Idd Nyembo na Issa Mtama.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na askari hao ni Hamidu Hamadi na Prosper Maleto wakazi wa Tandika, jijini Dar es Salaam, Mussa Mohamed Ali mkazi wa Kinondoni, Amir Bakari mkazi wa Mbagala, Seif Kadro Mdumuka mkazi wa Kisarawe, Said Kadro Mdumuka na Ramadhani Athuman wakazi wa Chanika.
Kamanda Matei alifafanua kuwa meno hayo yana uzito wa kilo 305, yakiwa na thamani ya sh 850,500,000, huku akitoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili ili wachukuliwe hatua bila kujali nyadhifa zao.


Katika hatua nyingine, mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, Ibrahim Mnyanga (58) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na vipande 16 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 24.5 kinyume cha sheria.


Mnyanga alikamatwa Julai 22, mwaka huu, saa tisa alasiri eneo la Msimbazi Centre akiwa na masanduku mawili yenye nyara hizo za serikali.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na askari polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam waliokuwa kwenye doria ya kawaida kumtilia shaka.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa atafikishwa mahakamani muda wowote baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda Kova aliongeza kuwa ameunda jopo la uchunguzi wa kifo cha mtuhumiwa Seleman Mwinyi (46) mkazi wa Kurasini Shimo la Udongo.


Kwa mujibu wa kamanda huyo, jopo la uchunguzi linaundwa na Jeshi la Polisi, vyombo vya ulinzi na usalama wakishirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).
Marehemu Mwinyi alikutwa na mauti akiwa ndani ya chumba cha mahabusu Kituo cha Polisi Oysterbay huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akidai kwamba kifo cha mtuhumiwa huyo kilitokana na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.
 
Kwa serikali hii hayo ni ya kawaida sana
Hakuna hata Kiongozi anaweza sema
maana hao ni wachafu pia huwatuma hao
wadogo kila uchao.
 
Mtu yeyote akitaka kufa uangalia ukuta au juu, hii ni dalili ya wizi kuchokana na kausema tuu sasa.... wameiba siku nyingi tu ila sasa wanatazama ukuta.
 
mkiambiwa kuwa serikali na mamlaka zake ni LEGE LEGE NA DHAIFU (IMPOTENT) mnalia lia tu, hakika natamani ningeishi kipindi cha utawala wa Chief Mangungo wa Msovelo.
 
Vigogo wameona ni dili kuwatumia polisi kusafirisha nyara.

Hao polisi ni BANGUSILO tu.......... kuna wakubwa hapo nyuma....
 
dah , Haya sasa Majanga ,

wanasiasa WANAIBA Nyara ( Kinana) , polisi WANAIBA nyara za serikali , Wanajeshi nao wanaiba nyara ,
viongozi ndo waiba walio Hai kabisa ( REF. wale twiga waliotoroshwa kwa ustadi mkubwa)

But kubwa kuliko ZOTE wametugeuka na sisi wananchi wao wanasachi vyote vilivyopo mfuko (Kodi ya kichwa imerudi kwa style ya kodi ya Kadi ya simu .


HAYA MAJANGA
 
Duuh...sijui dili gani ambalo polisi hawapigi......inawezekana kabisa kuwa rekodi yao haivunjwi na wasio polisi....
 
polisi polisi polisi
Kuua Binadamu - polisi
Kutesa watu - polisi
Kurusha mabomu - polisi
Kuua tembo - polisi
Kuua na kubambikiza mtu kichwa cha binadamu - polisi
Kuficha/kushirikiana na wauza mihadarati - polisi

And yet, waziri mwenye dhamana nao yupo ofisini anadunda!!!!!!!!!!!!!
 
Duh sasa labda uwe na moyo kama wa mwendawazimu kuwatetea polisi.
 
Kamanda Kova aliongeza kuwa ameunda jopo la uchunguzi wa kifo cha mtuhumiwaSeleman Mwinyi (46) mkazi wa Kurasini Shimo la Udongo.


Kwa mujibu wa kamanda huyo, jopo la uchunguzi linaundwa na Jeshi la Polisi, vyombo vya ulinzi na usalama wakishirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).
Marehemu Mwinyi alikutwa na mauti akiwa ndani ya chumba cha mahabusu Kituo cha Polisi Oysterbay huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akidai kwamba kifo cha mtuhumiwa huyo kilitokana na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.

Hebu nikumbusheni vizuri hii habari ilipotoka mara ya kwanza Kituo cha Polisi Osterbay cha Polisi Mkoa wa Kinondoni si walikataa hakuna kitu kama hiki...
 
Hao polisi watafunwe sawa sawa iwe ni mfano kwa wengine wenye tabia km hiyo ya kishenzi.
 
Nalipongeza jeshi la polisi kwa kuwatia mkononi mwa dola wahalifu hao
 
polisi polisi polisi
Kuua Binadamu - polisi
Kutesa watu - polisi
Kurusha mabomu - polisi
Kuua tembo - polisi
Kuua na kubambikiza mtu kichwa cha binadamu - polisi
Kuficha/kushirikiana na wauza mihadarati - polisi

And yet, waziri mwenye dhamana nao yupo ofisini anadunda!!!!!!!!!!!!!
Kukamata wahalifu - polisi
 
polisi polisi polisi
Kuua Binadamu - polisi
Kutesa watu - polisi
Kurusha mabomu - polisi
Kuua tembo - polisi
Kuua na kubambikiza mtu kichwa cha binadamu - polisi
Kuficha/kushirikiana na wauza mihadarati - polisi

And yet, waziri mwenye dhamana nao yupo ofisini anadunda!!!!!!!!!!!!!

MKUU KAMA UNATA NCHIMBI AKUTUMIE WANG'OA KUCHA NA MENO BILA GANZI ENDELEA KUKISAKAMA CHEO CHAKE AACHIE KITI HALAFU AANZE KUZUNGUSHA CV MAOFISINI WAKATI MIJIHELA YA BILA JASHO IPO TELE WIZARANI?? ....bongo dhana ya uwajibikaji BONGOLAND bado ni ndoto.
 
Kama kungekuwa na kuwajibishana Tanzania Mawaziri husika sikunyigi wangesha jiuzuru, lakini hilo haliwezekani sababu Executives wote ni wapiga dili chafu.
 
Haya sasa! Wabunge wa CCM mlipoambiwa na Mch Msigwa kwamba huu mtandao unahusisha watumishi wengi wa serikai ya CCM kama kawaida yenu mlimzomea,

Leo hii nani anastahili kuzomewa kati yenu na Msigwa? Wabunge wa CCM ni janga la Taifa
 
huu ndio mradi wa viongozi wa ccm n kutapanya mali za umma, na kufilisi nchi, tatizo kwa wakubwa wao serikalini huu ndio mradi kuanzia kikwete hadi wenye viti wa vijiji.
SHAME UPON THEM, WTZ TUSIPO WAONDO HAO WAHARAMIA CCM MJUE MMESHA DAIMA.
 
Raia kazi tunayo kwa kweli!!!!!

Watafikishwa mahakamani baada ya USHAHIDI/UPELELEZI! !!!!!!

Si ni suala la kuweka sheria tu kuwa ukikamatwa nayo unahasiwa na kufungwa maisha au???? Mbona ya simu imewezekana???????
 
Back
Top Bottom