Polisi wanaswa na meno ya tembo

Polisi wanaswa na meno ya tembo

Kinana at work!

Hivi kesi aliyofungua bado haijaisha tu?
 
polisi polisi polisi
Kuua Binadamu - polisi
Kutesa watu - polisi
Kurusha mabomu - polisi
Kuua tembo - polisi
Kuua na kubambikiza mtu kichwa cha binadamu - polisi
Kuficha/kushirikiana na wauza mihadarati - polisi

And yet, waziri mwenye dhamana nao yupo ofisini anadunda!!!!!!!!!!!!!

Halafu waziri huyo huyo anadiriki kusema hadharani kuwa amani nchini itakuja kwa KUSALI!!! Kwa hujuma mnayofanya nchini haki haiwezi kupatikana na amani lazima itatoweka!!!
 
Huu si mwezi wa ramadhani? Wahusika wengi ni watanzania wa dini ya ....(siyo udini) but for the sake of connecting the dots with knana na their sism!
 
Raia kazi tunayo kwa kweli!!!!!

Watafikishwa mahakamani baada ya USHAHIDI/UPELELEZI! !!!!!!

Si ni suala la kuweka sheria tu kuwa ukikamatwa nayo unahasiwa na kufungwa maisha au???? Mbona ya simu imewezekana???????

Jamani mimi sio mdini lakini mbona najiuliza katika tuhuma nyingi za madawa ya kulevya, Meno ya tembo nk. majina ya kiislamu yanaonekana zaidi? Je ni mbinu ya kuonyesha kua uislamu ni adui wa maendeleo na ustawi wa taifa au watuhumiwa wnaficha majina yao halisi?
Naulizatu jamani.
 
...

......kwa nini hii kasi inaongezeka?

......nahisi wamehisi 2015 milango ITAFUNGWA!!!

.....TAFAKARI!!!!!!!!!!
 
Hebu nikumbusheni vizuri hii habari ilipotoka mara ya kwanza Kituo cha Polisi Osterbay cha Polisi Mkoa wa Kinondoni si walikataa hakuna kitu kama hiki...

mkuu hali ni mbaya jeshi la polisi linatia aibu nchi
 
Maiti kukutwa rumande mtuhumiwa alipigwa na wananchi wenye hasira (ahahahaha) walimfunga mtu mahututi badala ya kumpeleka hospitali ?Hivi Kova utaacha lini uwongo ? kama mnaushahidi alipigwa na wananchi je kuna upelelezi wowote mlioufanya kuwabaini waliompiga na hatua zipi mmezichukua kwa hao wahusika (wananchi) ?

Upelelezi haujakamilika mtu kakutwa na mabegi ?ama na nyie mmepunguza mzigo mnasikilizia kama watu wataropoka mkauze ?Polisi mnahitaji kujisafisha.
 
Watu watafikiri labda hii issue ya tembo ni mchezo sio mchezo hata kidogo hawa mashetani wanafyeka bila huruma hii picha moja tu. Kwa bahati mbaya ninaona visa na picha kama hizi karibu kila siku na sijui ni lini this "very serious government" of URT will take action against these cruel,selfish, unscruplous, ill mannered washenzi wapuuzi wasiojua kesho yaani inakasirsha na kuuma sana. Hebu kaone hako katembo kalikua kazaliwa wakati wowote hawa mafisadi wakaona bora wajishindie mapema. ------- zao wote.
 

Attachments

  • tembo mtoto 030.jpg
    tembo mtoto 030.jpg
    1.4 MB · Views: 64
just kuwasaidia polisi .. Huyo Polisi Issa Mtama (aka Bonge/Chinga) ndo sterling wa hiyo biashara na kwao ni huko huko Mtwara ameifanya kwa mda wa kutosha ..
 
Polisi wameshaamulishwa kuwa juu ya sheria. kwa hiyo pinda aamue kufuta ile kauli yake au iendelee kuwa vilevile.

Hii ni kama una familia ya watoto nyumbani nawe baba ukatoa madaraka kwa mmoja wa watoto kufanya apendavyo kwa wengine. utaona mengi tu juu ya upuuzi huyo mtoto!!

Kama polisi anaua raia halafu wanaambiwa waendelee kupiga. na kama polisi anaua raia halafu mkuu wa polisi mkoa anapandishwa cheo kwa hiyo wako juu ya sheria kimamlaka ya nchi!!! kuua raia, kuwinda nyara za nchi, kuvuna na kusafirisha bangi na mirungi na takataka zingine!!

Hakuna watu wachafu kama polisi na hasa wanapodekezwa kwa maelekezo ya kimabavu!! tutaona mengi!!
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akidai kwamba kifo cha mtuhumiwa huyo kilitokana na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, agizo la PM liliwahusu polisi kwa raia sio raia kwa raia. Kazi kwelikweli, maana hata maneno ya bosi wao pale UDSM kuwa polisi wana kawaida ya kusingizia/kubambikia kesi raia hajatoweka kwenye meza za magazeti
 
Mkiuu Simigon - siku nyingine katika habari kama hizi za manjagu haya kukamatwa na tuhuma mbali mbali uwe unataja 'POLICCM' katika headline yako badala ya 'polisi' tu. Hii ni kwa sababu wao hufanya kazi kwa niaba ya chama chao, na sasa nao wameanza kuiga mambo yao ya kila aina ya uchafu.
 
Waliokamatwa sio wahusika wa PEMBE ZA NDOVU (SIYO MENO) maana wao kwa vyovyote walitumwa na BOSI wao watekeleza kazi hiyo kwa vyovyote huwa wanapewa kitu kidogo.
Kamanda husika wa askari hao anahusika maana anajua ni eneo gani askari wake walipopangwa siku husika, ahojiwe kwa mapana, pia gari husika na wale watu tisa wataje nani kawatuma.
Kiasi cha milioni 15 walizotaka kuhonga walizitoa kwenye akaunti gani kama ni askari wacheki akaunti zao au wale tisa akaunti zao zichekiwe kujua pesa zinavyoingia na kutoka.
Jeshi la Polisi halina tena WELEDI ni muda muafaka sasa kuanzia IGP, KANDA MAALUM DSM, KANDA ZA MIKOA makamanda wajiuzulu kwa ushiriki wao wa moja kwa moja kwenye ujambazi.
Aidha tumpongeze kamanda wa Mkoa wa Pwani kwa kukataa kupokea Rushwa ya hayo majangili.
Tunasubiri Waziri NCHIMBI,akishirikiana na CHAGONJA, KAMUHANDA kutupatia majibu
 
Mch. Msigwa alisema siku nyingi kuwa mtandao wa majangili uko ndani ya CCM na serikali yake!! Leo nani asimame kumkejeli tena Msigwa. Huu ni uthibitisho POLICCM, JWTZ, JKT, MAGEREZA, Kinana wote ndi wahusika wakuu

CCM MAJANGA, MAJANGA, MAJANGA!!
 
Kama wanaona na kujua rais anauza drugs, kinana anaua tembo na kuondoka na meno yao, madawa ya kulevya yakikamatwa, kesho unasikia kuwa ulikua ni "unga wa sembe" SIO madawa ya kulevya je, unategemea hao "dagaa" wafanye nini........
 
Kwenye hili suala la meno ya tembo kuna movie tunachezewa nini? hii sasa too much,tukiandamana kuna tatizo?! Napata hasira sana. Yani na wingu lote hili bado kuna raia wa nchi hii wanaendelea kuua tembo?! No way tumechoka! Tupazeni sauti hata kwa kuandamana serikali ijue wanatukera,hatuwezi kuwa na serikali dhaifu kiasi,aibu! aibu! Madawa nayo!!
 
Nianze kukosoa namna ya mwandishi wa habari alivyoripoti.
1. Mwandishi hajatuelwza ni nani mmiliki wa toyota surf?
2. Pili ili kutoa uzito wa janga hili la biashara haramu ya meno ye tembo kwanini waandishi wa habari wasioneshe pia hasara iliyoletwa na wizi huo. Mathalani, itajwe thamani halisi (kwa shilingi) ya tembo mzima na si meno yake. Mfano kama ni shilingi milioni 100 mara tembo 35. Hiyo ndiyo thamani ya tembo. Thamani hiyo isiwe determined by market principles.
3. Waandishi wa habari hawana tabia ya kufuatilia habari mpaka tujue hitimisho lake
 
Back
Top Bottom