...Polisi wetu wameonyesha ukilaza wao kumkamata Lulu ambaye alikwenda kuwaarifu ya kuwa mpenzi wake amedondoka na kufa mwenyewe. Polisi wenye mafunzo stahiki walipaswa kutoa PF, kurekodi kauli za wahusika na kuchukua contacts zao na kuwaruhusu waondoke wakisubiria taarifa ya ukaguzi wa mwili wa mwendazake...................i na za kikatiba za kuwa hana kosa hadi pale atakaposhitakiwa na kosa..................polisi wamemkamata huku hawana ushahidi wowote kuwa kanumba aliuawa na kuwa hiyo ni kesi ya murder na kauli ya kamanda wa polisi aliedai kuwa Lulu atashitakiwa kwa mauaji inathibitisha jinsi jeshi la polisi lisivyojua wajibu wake ndani ya polisi jamii................
katika mazingira ya namna hii nani atatoa taarifa kwa polisi wakati akijua ataanza kubughudhiwa..............na kushukiwa kuwa anahusika na mauaji wakati hakuna ushahidi wowote hadi sasa wa kufanya hivyo.........mtoto wa watu kakoseshwa kula Easter yake kwa sababu ya uzembe na umbumbu wa polisi wetu................kweli tunakazi ya kuwalisha hawa vilaza polisi na familia zao kwa kutubughudhi tu!
Pili, hakuna maelezo kwa nini mdogo wake wa Kanumba - Seth - naye hakukamatwa pia kutokana na maelezo yake mwenyewe kuwa siku nzima alikuwa na kaka yake kabla ya Lulu kuja...................mashaka kama yanaweza kutiliwa kwa Lulu kwa nini watu wote waliokuwapo wakati marehemu yupo hai wasichukuliwe kama ni watuhumiwa bali mdogo wake aonekane hana hatia kama siyo ubaguzi wa kijinsia? kauli ya polisi kuwa ni ugomvi wa kimapenzi ndiyo uliomwuuwa unazidi kulidhalilisha jeshi la polisi kwa kufikia hatma ya swala lenyewe hata kabla ya kusubiri maelekezo ya taarifa za kitabibu..............