Polisi wamtaka Sheikh Ponda ajitokeze kusema nani alimpiga risasi

Polisi wamtaka Sheikh Ponda ajitokeze kusema nani alimpiga risasi

Umeelewa vibaya muktadha wa niliyo maanisha. Hii ni mtiririko wa matukio wala siyo kuwa nani ni mtu wa Mungu. Wote ni watu wa Mungu. Walianza kuwaua wapinzani ambao ni pamoja na wa kisiasa na kimaslahi, wakasogea kwa viongozi wa dini ambo nilisema watu wa Mungu pamoja na tunasubiri siku wao kwa wao wakianzana, siyo muda mrefu tusubiri.

Nadhani nimefafanua nilikuwa na maana gani


Mkuu soma bandiko lako la awali vizuri.
 
duh, hawa jamaa waliokuwa wanataka muua wameshindwa muua kwa namna ingine hadi wampige risasi jukwaani..sijui huu mchezo wa paka na panya utaishaje?
 
aise inatisha, kuna siku watatubuthu kumpiga risasi kiongozi wetu wa chadema
 
Kama ashakamatwa tungoje nini kinafata. Ni kweli jeshi la polisi lina mapungufu mengi lakini tuwaache wafanye kazi yao.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwa upande wangu nawapongeza polisi kwa kiasi fulani. Busara waliyotumia kumsubiri Shekhe Ponda ashuke jukwaani ilikuwa kubwa kwani kama wangetaka kumkamata pale jukwaani maafa yangekuwa makubwa na leo hii tungekuwa tunazungumza mengine. Haingekuwa rahisi kwa wafuasi wake kukubali akamatwe kirahisi na pia polisi wasingeacha kutumia nguvu ili kumkamata. Swali la kujiuliza ni kwa nini Shekhe Ponda alivyoona polisi wanamzingira akaamua kushuka kwenye gari na kutaka kukimbia? Nadhani kwa jibu la haraka ni wazi kuwa alitambua kosa lake na ndio maana akataka kuwakwepa polisi.
 
St.Apolinary na wote wenye mawazo Kama yako,

Ushabiki na au utani una nafasi yake. Lakini kufanya utani katika jambo lolote linalohusu maisha ya mtanzania ni ujinga. Msingi hapa ni kuwa kazi za polisi hazifanywi kwa matakwa ya polisi, awe ngazi yeyote ile. Polisi wanaongozwa na Sheria ya nchi. Hata pale Polisi wanapolazimika kutumia Risasi au mabomu ya machozi kuna utaratibu wa kisheria. Hii haijalishi mtu amefanya kosa kweli au la. Uhai wa mtu na usalama wake ni haki yake ya msingi, na haki hiyo inaweza kuondolewa tu na mamlaka iliyokubalika kisheria yaani mahakama. Polisi jukumu Lao ni kumkamata, bila kutumia nguvu zilizodi kiwango isipokuwa katika mazingira yaliyowekwa na sheria. Narudia, hakuna mtanzania, awe mhalifu asiwe mhalifu, wa itikadi yeyote ile au dini yeyote ile anayepaswa kuhatarishiwa uhai wake na vyombo vyenye jukumu la kulinda usalama wake na wa Mali zake. Tujifunze kwa wenzetu wa nje wanavyolinda watu wao, tazama Uingereza inavyoshughulikia wale Mabinti 2( Mungu awape Faraja na ustahimivu katika kipindi chao kigumu). Nimalizie tu kwa kusema angalau sasa tunaweza kusema with authority baada ya Taarifa mbili za Tume ya Haki za Binadamu ambayo ni chombo cha Serikali kuwa Nyololo Polisi ( Kamanda RPC) na Tendwa Msajili walivunja Sheria, nab kwa mauaji ya Arusha IGP Mwema na RPC Andengenye walivunja Sheria ambapo katika matukio hayo yote mauaji ya raia wema yalitokea, na mpaka Leo Serikali imepata kigugumizi. Kama Shekhe Ponda alimaliza mkutano wake ni kwanini hawakumkamata Mara tu alipokuwa anashuka jukwaani? Polisi wetu hawakufundishwa Mob psychology na Crowd Control? Kama ndivyo basi kuna dosari kubwa sana katika mfumo wetu ( it must be a systemic problem). Tuache ushabiki kwenye mambo ya msingi. Namwomba Mungu ampe mjoli wake ahueni.





UOTE=St.Apolinary;7051181]Anajulishwa kama mbowe kwa sababu gani? Kwani yeye ni mwanasiasa? Serikali imesema haitaki mihadhara yake full stop.[/QUOTE]
 
Ukweli ulio wazi, Polisi hawa ndio chanzo cha kuvuruga Amani Yetu

Kama nikweli walikua wanamtafuta shekh ponda walishindwa nini kumuambia Shekh ponda Popote pale alipo ajisalimishe kituo chochote cha polisi kama walivyo fanya kwa Mh. Mbowe, Nasari n.k

Kodi yetu tunayo lipa Ndio inayo geuka kua ni fimbo kwetu. Kuna haja Gani ya Kutumia Magari zaidi Ya kumi na Asakari zaidi ya 89 kwenda kumkamata mtu ambaye sio jambazi na wala hana siraha.

Watanzania wenzangu Wote kwa pamoja tuondoe itkadi zetu za kisiasa na kuangalia kwa kina kuhusu Jeshi letu la polisi.

Polisi wamekua ni chanzo cha kuvuruga Amani yetu. Nakuandaa ushahidi wa uwongo kuwahadaa Watanzania.
tukio la ponda ni ajali katika eneo la kazi tu
 
form four and failures...bogus ndio hao polis..ndio maaana na cfa ya polis uwe huna akil na elimu
 
duh, hawa jamaa waliokuwa wanataka muua wameshindwa muua kwa namna ingine hadi wampige risasi jukwaani..sijui huu mchezo wa paka na panya utaishaje?


Iwe real suspect au kafara,ilikuwa strategical ifanyike kama ilivyofanyika ili ionekane machoni pa wazungu serikali ya ccm ilichukizwa na imechukua hatua tukio la acid z'bar
 
Sunday, August 11, 2013 | 7:57 PM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA - DAR ES SALAAM

​


1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.

2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.

3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.

4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.

5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.

6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
 
Shekhe Ponda ameombwa ajitokeze ili kuthibitisha kuwa amepigwa risasi na jeshi la polisi.

Source: ITV
 
Msemaji wa jeshi la polisi kadai kuwa sheick Ponda alikuwa anatafutwa na polisi na alipotaka kukamatwa kulitokea wafuasi wake wakawa wanarusha mawe na katika kurusha mawe ndo sheikh Ponda akajeruhiwa na polisi haihusiki

Source TBC 1 HABARI
 
Finally, now we have the official report. Than you fhis. But your haven't told us if he under arrest or not.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Waongo....hata kwa mwangosi walisema ni ktu kizito kilirushwa
 
Majeruhi wengine zaidi ya sh. Ponda ni kina nani? Na wamelazwa hosp. Gani?
 
Back
Top Bottom