Polisi wamtaka Sheikh Ponda ajitokeze kusema nani alimpiga risasi

Polisi wamtaka Sheikh Ponda ajitokeze kusema nani alimpiga risasi

shaabani

Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
64
Reaction score
17
Sunday, August 11, 2013 | 7:57 PM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA - DAR ES SALAAM

​


1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.

2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.

3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.

4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.

5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.

6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Ukweli ulio wazi, Polisi hawa ndio chanzo cha kuvuruga Amani Yetu

Kama nikweli walikua wanamtafuta shekh ponda walishindwa nini kumuambia Shekh Ponda Popote pale alipo ajisalimishe kituo chochote cha polisi kama walivyo fanya kwa Mh. Mbowe, Nasari n.k

Kodi yetu tunayo lipa Ndio inayo geuka kua ni fimbo kwetu. Kuna haja Gani ya Kutumia Magari zaidi Ya kumi na Asakari zaidi ya 89 kwenda kumkamata mtu ambaye sio jambazi na wala hana siraha.

Watanzania wenzangu Wote kwa pamoja tuondoe itkadi zetu za kisiasa na kuangalia kwa kina kuhusu Jeshi letu la polisi.

Polisi wamekua ni chanzo cha kuvuruga Amani yetu. Nakuandaa ushahidi wa uwongo kuwahadaa Watanzania.
 
Ni upepo tuu utapita yamepita mangapi?

"Nchi ngumu hii"
 
mimi pia nashangaa polisi kila siku wanasema wanamtafuta ponda cha ajabu ponda mwenyewe wala ajifichi yuko huru tena adi anaweza kutembea kutoka sehemu moja adi nyingine hivi kweli wanamtafuta au usaniiiii tu
 
Ustadh Ricco, mwenye miwani, akimtambulisha Sheikh ponda jana mjini MorogoroFFU uwanjani
Shekh+Ponda+akiwaameduwaa+na+kusimama+ili+kujua+hatima+yake+baada+ya+kuona+gari+la+Polisi+wa+FFU+likiwa+eneo+la+viwanja+hivyo..JPG
Sheikh Ponda baada ya kuhutubia. Alipanda kwenye gari dogo na polisi wakaanza kulifuata. Baada ya waumini kulisindikiza ndipo mabomu ya machozi yakaanza kupigwa. Ponda alishuka ili atumie angalau usafiri wa pikipiki na hapo ndipo alipigwa risasi la begani na polisi. zilikua gari 5 za polisi. baada ya kupigwa risasi aliwahishwa ktk hospitali ya morogoro lkn walipokosa huduma akapelekwa kutibiwa sehemu ya siri aliko hadoi muda huu
​
 
Anajulishwa kama mbowe kwa sababu gani? Kwani yeye ni mwanasiasa? Serikali imesema haitaki mihadhara yake full stop.
 
Kwan yeye sio raia watanzania had azuiliwe asitoe maon yake...
 
Kwani hawana number yake?
Hivi ukiukumiwa kifungo cha Nje si kila baada ya Muda unaripoti Polisi/mahakamani ?

By the way hata mimi wangeniambia niwaletee ningemleta mbona tena kwa Amani tu.
 
Matukio haya na yale sambamba na habari/picha za ziada za Globu ya Jamii matukio-michuzi matukio-michuzi

› Home

View web version

SUNDAY, AUGUST 11, 2013

MUHIDIN MICHUZI at Sunday, August 11, 2013

SHEKHE PONDA ATIWA MSUKUSUKO KATIKA JARIBIO YA KUTIWA MBARONI NA POLISI MORO.

Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro. KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu. Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro. Shekhe Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo. Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali. Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifayuliwa risasi iliyompiga begani. Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja. Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi. Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu. Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini. Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo. Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki kusikojulikana. Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa kupatiwa huduma. Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda. “ Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili” alisema Kamanda huyo. Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota a wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega . “ Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema. Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea kufuatulia kwa ukaribu.

Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika.

Kutambulishwa jukwaani Shekh Ponda.

Kikosi cha FFU uwanjani

Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro

Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara nchini, Ustaadhi Abubakari

Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Kongamano , Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro

Shekh Ponda akiteta jambo na baadhi ya Viongozi wa umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Morogoro

Shekhe Ponda akiwa meza kuu kwenye kongamano hilo

Shekhe Ponda akiwa amezingirwa na waumini

Umati wa waumini wa Kiislamu wakimsikiliza Shekh Pond

Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda

Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya muda wa kongamano kufikia tamati,

Share 3

Create a Link

No comments:

Post a Comment

Links to this post

MK

MUHIDIN MICHUZI

ABOUT MATUKIO-MICHUZI

Powered by Blogger
 
some times ni bora mchochezi mmoja kadhibitiwa mapema kuliko kumwacha hadi akaleta mdhara sasa huyu ponda wamemlea hadi amekuwa na wafusi wengi hata wakimuua sio solution wangemdhibiti mapema tu
 
Nia na madhumuni ilikuwa ni kuondoka na uhai wa Ponda! Nchi hii kwa sasa haina viongozi kuna kundi la wasanii tu.
 
Nyerere alisema ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha. Serikali ya sisemu ilianza kula nyama ya wapinzani wao, sasa wameanza kula ya watu wa Mungu tusubiri kidogo wataanza kulana wao kwa wao, tena sasa imekuwa bila kificho.
 
Nyerere alisema ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha. Serikali ya sisemu ilianza kula nyama ya wapinzani wao, sasa wameanza kula ya watu wa Mungu tusubiri kidogo wataanza kulana wao kwa wao, tena sasa imekuwa bila kificho.


Hivi kumbe wapinzani sio watu wa Mungu!!!!!!?,ndio maana mnawashangilia police wanapowaua wapinzani !!!!?.Wanafiki leo tumewajua,mmesahau sisi sote ni binaadamu sababu ya dini za kuletewa!!!! shame on you.
 
Hivi kumbe wapinzani sio watu wa Mungu!!!!!!?,ndio maana mnawashangilia police wanapowaua wapinzani !!!!?.Wanafiki leo tumewajua,mmesahau sisi sote ni binaadamu sababu ya dini za kuletewa!!!! shame on you.

Umeelewa vibaya muktadha wa niliyo maanisha. Hii ni mtiririko wa matukio wala siyo kuwa nani ni mtu wa Mungu. Wote ni watu wa Mungu. Walianza kuwaua wapinzani ambao ni pamoja na wa kisiasa na kimaslahi, wakasogea kwa viongozi wa dini ambo nilisema watu wa Mungu pamoja na tunasubiri siku wao kwa wao wakianzana, siyo muda mrefu tusubiri.

Nadhani nimefafanua nilikuwa na maana gani
 
Back
Top Bottom