Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 202
- 1,588
Nalipongeza jeshi la Polisi Dar kwa kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi kada wa chama cha ACT Bw.Habib Mchange, ili kuisaidia jeshi hilo juu ya tuhuma alizozitoa kwa CHADEMA.
Pamoja na mambo mengine, Mchange aulizwe maswali yafuatayo:
1.Kwa kuwa amekiri kutumiwa na CHADEMA kutekeleza mauaji mbalimbali, aseme kwa sasa huko alipo wamemtumia kufanya mauaji ya nani?
2.Kama CHADEMA walimtumia, kwanini tusiamini kuwa hata sasa anatumika kwa kuwa ameshakuwa mtu wa "kutumikatumika"?
3.Kama anakubali CHADEMA walimtumia kupanga mipango ya mauaji, mbona anakataa kuhusika na njama za kumuua Dr.Slaa zilizotolewa na madiwani wa Shinyanga?
4.Aeleze kwa kina nani alimuua Mwangosi na atoe na ushahidi wa kutosha.
5.Aeleze ni kivipi CHADEMA walivaa sare za Polisi na kutekeleza mauaji ya Mwangosi.
6.Aeleze ni Afisa gani wa Polisi aliyewapa CHADEMA hizo sare na silaha za kumuua Mwangosi, na kwanini Afisa huyo hakuchukuliwa hatua.
7.Na kama Polisi wanafanya dili ya kuwaazima CHADEMA sare zao pamoja na Silaha ili kufanya uhalifu, kwanini hakuripoti muda wote hadi alipokuja kusema leo? Miaka mitatu aliyokaa kimya haoni alichangia watanzania wengi wasio na hatia kuuawa na CHADEMA kwa kupewa sare na Polisi?
8.Kwanini hakumshauri Rais Kikwete amfukuze kazi RPC Kamuhanda? maana kwa mujibu wa maelezo yake ndiye aliyesimamia mauaji ya Mwangosi kwa kushirikiana na CHADEMA.
9.Kwa kuwa amekiri yeye ni mtu wa dili za "mauaji" aeleze alishiriki nafasi gani kutekeleza mauaji ya Mwangosi? Alisambaza silaha kwa CHADEMA? Aliwabebea CHADEMA sare za Polisi? Au mchango wake ulikua upi?
10.Mwisho, ASIPEWE DHAMANA kwa kuwa anatuhumiwa kwa kupanga mauaji ( Conspiracy to Commit Murder).
(Pichani ni Habib Mchange enzi za ujana wake).