DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Barabara zote kuu zinazoelekea jijini Nairobi zimefungwa leo huku hali ya usalama ikimarishwa katika maeneo mbalimbali ya mji, kufuatia maandamano yanayotarajiwa katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Saba Saba.
Kulingana na BBC, polisi wameweka vizuizi katika maeneo muhimu, wakizuia magari ya umma na binafsi kuingia katikati ya jiji. Hali hiyo imewalazimu abiria kushuka mbali na jiji na kutembea kwa miguu kufika makazini au nyumbani.
Katika daraja la Kangemi, mashuhuda wanasema mabasi kutoka maeneo ya mbali—hata yale yaliyoingia kutoka nchi jirani—yamezuiwa kupita. Abiria wamelazimika kushuka na kutafuta njia mbadala kufika mjini.
Usafiri wa magari ya umma umepungua sana, na wengi wanategemea pikipiki kama njia mbadala. Biashara nyingi katika barabara kama Moi Avenue zimefungwa huku wamiliki wakihofia usalama wao na wa mali zao.
"Tangu asubuhi hakuna mabasi yanayoruhusiwa kuingia CBD (Katikati ya mji). Watu wanatembea kwa miguu kwa makumi ya kilomita. Ni kama jiji limefungwa rasmi," amesema mmoja wa wananchi katika eneo la Westlands.
Serikali kupitia Wizara ya Usalama imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha maandamano yanayofanyika hayapelekei uharibifu wa mali wala kuhatarisha maisha ya wananchi, kufuatia matukio ya vurugu yaliyoshuhudiwa kwenye maandamano yaliyopita.