Polisi wamezingira nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima

siasa imetokea kwenye DINI. Huwezi kuvitenganisha.
kiongozi wa dini kujihusisha ktk siasa ni jambo linalopelekea uvunjifu wa amani na umwagaji wa damu... ona sasa mpk mda huu wafuasi wa gwajima wanajua anachosema mchungaji wao ni ufunuo kutoka kwa bwana kumbe ni hila zake tu...nashauri seikali ipige marufuku viongozi wote wa dini kujihusisha ktk siasa ili kuepuka vitendo vya uvunjifu wa Amana ikiwemo ugaidi
 
Taarifa toka East Afrika Radio kama inavyoonekana kwenye Accouny yao ya Facebook pichani inasema nyumbani kwa Gwajima kumezingirwa na Polisi.
Je lengo ni kumlinda au kumzuia asitoke? Kuna nini kinaendelea?
 

Attachments

  • Screenshot_2016-06-17-08-38-10.png
    Screenshot_2016-06-17-08-38-10.png
    135.5 KB · Views: 37
Dini ya kikwete si tatizo maana hata mimi ni dini yake. Tatizo ni mambo aliyoyafanya. Mbona jeneral ulimwengu naye aliyasema na hawajamkamata? Mbona Dr Magufuli alisema kikwete kamwachia kazi kubwa sana. Wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa na mita za kupimia mafuta bandarini hewa?watu wameiba sana. Dini yake msiitumie kama kava ya kuficha maovu yake. Na mtu asiye na hoja hukimbilia dini,rangi au kabila. Utawala uliopita ulikuwa wa wezi


Gwajima alitaka kutumia madhabahu kujipendekeza kwa Magufuli, mjinga sana!
 
Badala ya kukamata majizi ya nchi hii, kazi kuhangaika na viongozi wa dini,
Hata baadhi ya viongozi wa dini ni mijizi pia huoni wanavyotukamua halafu wao wanaisha kama wapo mbinguni wakati hata yesu hakuwahi kuishi maisha ya kina gwajima kwa utajiri walionao
 
Tatizo lada ni hivyo tulivyoambiwa kuwa siku hizi demokrasia imerudi nyuma miaka 50 , watu hawataki kukosolewa, kulaumiwa, kusahihishwa, kushauriwan watu hawataki kufuata taratibu sheria na wajibu baadhi ya watu wanaamini mawazo na hisia zao bila kujali au kutoa nafasi kusikiliza hoja na hisia za wengine!!!
 
Tutaendelea kuwapa yanayojiri.

Mchezo huu hautaki hasira

=> Polisi 6 ndani ya Landcruiser wako nje ya nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wamezingira nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima huko Salasala, jijini Dar muda huu.

Wasema wamegonga geti bila kufunguliwa.
View attachment 357102

=======

Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo linamuhitaji Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa kuwa kuna mkanda wameupata unaosemekana ni wake ambao unazungumza maneno ya kichochezi.

Kamanda Sirro alisema: “Tumepata clip (mkanda) inayosemekama ni ya kwake. Tunamtaka athibitishe kama hayo maneno ni ya kwake. Na kama ni yeye ameyasema, anaelewa nini kuhusu kile alichokizungumza kwa sababu hayo maneno ni kichochezi. Tupo kwenye uchunguzi mama yangu.”

Jana, polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.

Chanzo: Mwananchi
Kanisa vs Siasa. Tanzania!!!
 
Tatizo lada ni hivyo tulivyoambiwa kuwa siku hizi demokrasia imerudi nyuma miaka 50 , watu hawataki kukosolewa, kulaumiwa, kusahihishwa, kushauriwan watu hawataki kufuata taratibu sheria na wajibu baadhi ya watu wanaamini mawazo na hisia zao bila kujali au kutoa nafasi kusikiliza hoja na hisia za wengine!!!
Hapa kweli umenena,, Democrasia iliopo hamna mwenye kuielewa vizuri hususani sisi wananchi wa kawaida, ila viongozi ndio wanaoelewa, mm naomba viongozi wazidi kutusaidia ufafanuzi wa democrasia yetu inapo elekea kwa maana, Sijui out of this, kitafuata nini,,?? Nikilinganisha na ile speech ya Mh Zitto kable, alio mpoint Mh Raisi.
 
Naishauri serikali na vyombo vyake,wamuite na wala wasiwe na mipango yoyote itakayoleta mapokeo tofauti kwa jamii.

Gwajima ni kiongozi wa dini,anajulikana,anafahamika,haitaji kuzingirwa wala kukamatwa kwa staili hiyo. Tuwe na uvumilivu
 
Kama kweli polisi wanataka tuwaone wanafanya kazi ,waimalishe ulinzi maeneo yote yanayoitwa soweto ambyo ni hataro kwa wakazi wa maeneo hayo.
 
Ya Mungu MPE Mungu. Ya Kaisali MPE Kaisali.iweje uko . kanisani. Uingize siasa..wewe ombea serikali.basi. ishauli. Siyo kujiingiza.na kutoa kauli kama msemaji.wewe shugulika kiroho.ombea watu.hatari kweli.
 
Back
Top Bottom