Polisi wameugeuza mlima kutonga kuwa chanzo kipya cha mapato.

Huyo polisi amekushinda sehemu moja tu. Kuovateki sehemu isiyoruhusiwa. Hayo maelezo mengine unayotoa inafaa yawafikie tanroads. Polisi yuko pale kusimamia sheria.
kitonga yote ni kona tupu kali,kwa dereva aliyepita chuo asingekuja kulalamika hapa kwa ujinga aliofanya.

anataka kuhalalisha uhuni wake double standard waliyofanya polisi kwenye fuso,kitu ambacho hatuna uhakika nacho pia.
 
Sijaelewa uchotetea mtoa mada,
Binafs UJASIRI wa kuovertake kitonga Sina kabisa.

Bora TU nichelewe, ila sio kurisk maisha kwa haraka zisizo na maana.

Ukiovertake, ukapigwa konga Moja tu pembeni tayari Ni ahera iyo.

Kama kweli ulienda driving school, ile mistari kabisa inajieleza kua mahali pale sio pa kuovertake.

Pia hata Kama Hakuna mistari, bado kuovertake mlimani na kwenye Kona Kali Kama za kitonga bado sio salama hata kidogo.

Jifunze Defensive Driving,
Makosa ya dreva mpumbavu yasigharimu maisha yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
humo barabarani isingekuwa nafsi za wasio na hatia pangeachwa kama palivyo,ili kila mtu ajifunze kwa vitendo.

kuna bango la barabarani nililiona nchi za mbele limeandikwa kwa kiingereza tafsiri yake ni hii.
"maisha yako yanaweza yasiwe na thamani kwako na kwetu pia,ila usitupe kazi ya kusafisha lami yetu"

huyu ni ile aina ya watu anayetakiwa kuchangia serikali hata kwa makosa 7 au 9,ili kabla hajafa na buyu, serikali iwe imenufaika naye
Upo sahihi kabisa, na nimeona kuna watu wanasema kwamba siujui vizuri mlima kitonga wana sababu zao ni sawa kwa fikra zao.
Jiulize kwa nini makampuni ya kimataifa hapa tanzania, mtu akipewa gari la ofisi linakuwa na tracking kwamba hautakiwi kuzidi spidi 80.ukizidisha unafukuzwa kazi.
Huo mlima sijaupanda kitambo ila niliupanda sana wakati wa kutafuta maisha kwenda sauzi kununua ndinga kuja kuuza huku. Marafiki wengi niliwapoteza njiani sababu ya hizo spidi. Gari ina spidi 240 hadi 300 mtu anataka azimalize zote matokeo yake inammaliza na yeye.
Natumia pesa nyingi every 2 years kuwapa Training wafanya kazi wangu kuhusi safe driving. Si vema kukatisha uhai wako kwa ajali za barabarani.
 
Habari zenu wapendwa ,naamini bado mpo na hangover ya furaha ya did.Kuna Jambo ningependa kuliweka hapa nikiamini mamlaka husika wanaweza kulipitia na kuliangalia upya.
Last week nilikuwa na safari ya kuelekea nyanda za juu kusini . Bahati nzuri nilifankiwa kupata lifti kwa jamaa yangu mmoja alikuwa na safari ya uelekeo huo. Kufika pale kitonga kama kawaida unakutatana na mabango mbali mbali ya tahadhari ukitahadharishwa juu ya hatari ya mlima na kwa bahati mbaya mlima mzima huruhusiwi ku overtake. Basi tulipoanza kuupanda mbele kidogo tukakutana na malori manne yamesheheni mzigo tukayafwata kwa taratibu kwa dk kadhaa kufika mbele kidogo akaona upenyo (kwenye mlima kuna sehemu wamepanua barabara kwenda kushoto) jamaa akatanua kwenda kushoto kabisa akapata upenyo wa kupita..kwenda mbele kidogo tukakutana na malori mengine.tukayafwata na tulipofika kona iliyo vikzuri tukachomoka kama kawaida .kazi ikawa ni kuangalia usalama na kuchomoka ..kufika kat Kati ya mlima tukakutana na trafki akatupiga mkono tukae pembeni..tuliposhuka akatuita na kutuonyesha kwamba mmeanza kucheza rafu kuanzia kuleee.kumbe bwana waliposimama wanauwezo wa kuona barabara kuanzia mwanzo wa mlima ..
Tukamsikiliza kisha nikamuuliiza kwa hiyo huu mlima wote haturuhusiwi ku overtake ?
Akanijibu kwa hasira hujui Alama za barabarani ? Umesona uderava kweli?
Nikamjibu mbona hujajibu swali langu?
Nikamwomgezea swali lingine..kwa hiyo mimi mwenye gari dogo Natakiwa niwe nyuma ya malori haya hadi mwisho..hamuoni kwamba ni hatari na upotevu wa muda?
Nikaona anazidi kuwa mkali..yaani wewe badala ya kuomba msamaha unajifanya kuhoji na kujifanya mjuaji?
Nikamjibu sioni sababu ya kuomba msamaha kwa sababu kiuhalisia huu mlima hakuna gari dogo litakalofwata hiyo sheria yenu hata ninyi wenyewe hamuwezi kuifwata..huu niuonevu wa wazi yaani haina tofauti na vibaka wa usiku..mzee akawaka na kusema huyu lazima aandikiwe maana anajifanya mjuaji..nikamwambia jamaa yangu wacha waandike nitakulipia..hakuna kuwapa hela ni bora niichangie serikali yangu.
Mara ghafla wakalisimamisha gari lingine dogo kwa kosa lile ..alipofungua kilo kumbe wanafahamiana wakaanza kuchekena na kupigishana story kisha akamtakia safari njema.nikamuliza huyu jamaa alikuwa nyuma yangu na malori niliyoanza nayo mimi bado nayaona yaleee kwenye kona ya pili ya mlima..ina maana huyu Nae aliyapita ..mbona mmemwachia?
Wakajibu usitufundishe kazi wewee..sisi ndio wenye mlima..nikabaki nashangaa huku nikimwomba amalizie kutuandikia tuendelee na safari..wakati anandika yakapita malori matatu na fuso nyuma yake. Akamwambia dereva wa fuso acha kulal overtake weweee.jamaa akaovertake..nikamuuliiza na hii tunaiitaje ? Akajibu mm ndio mtu wa usalama nimemruhusu ....nikabaki nashangaa.
Kabla sijaondoka nikaliona gari walilopaki pembeni..nikacheka Sana wakaniuliza wacheka nini.
Nikawambia mwaka huu January nilisafiri toka makambako nikapita hapa..kufika ilula huwa hamruhusu ku overtake kabisa ingawa pako vizuri.ghafla nikapitwa kwa kazi na hii gari na mbele kulikuwa na malori kadhaa akayapita tena. Kuna jamaa akaamua kuwaiga hakufika hata mbali akadakwa akaandikiwa ..bahati nzuri mi napafahamu nikawa mpole..kufika kabla ya mlima nikalikuta hili gari lenu mmepaki ..ndio nikagundua kumbe ni trafki ndio maana hamkusimamishwa..wakati nashuka mlima mkaja tena mkanipita kwa kasi na malori kadhaa mbele nikaja nikawakuta hapa ..sasa hizi sheria nyie haziwahusu au?
Wakanijibu kwa hasira tumeshakuandia naomba uondoke..nikawauliza kama mnasena huu mlima ni hatari ina maana hiyo hatari iko kwetu tu? Ila kwa maaskari na jmaa zao Wana kinga.? Nikaona wamekuwa wakali na kurudi kwenye ofisi yao..
Naomba serikali wauangalie huu mlima vizuri..wasitugeuze raia kama chanzo cha mapato.Ni kwa nn mtunge sheria ambayo hta ninyi hamuwezi kuifwata?
Umenikumbusha Sekenke.
Ukiwa unatokea Misigiri kona ya kwanza barabara imenyooka unaweza kuona mbele zaidi ya mita 600. Lakini alama (mstari wa katikati) hairuhusu ku overtake. Speed iliyowekwa hapo mwisho ni 30kph. Sasa fikiria mwenye lorry atembee na 30 pia mwenye gari ndogo atembee na 30.
Hiyo sehemu ndio traffic police hukaa. Yaani ulifika pale either u overtake au uzidishe speed. Hakuna mwenye gari ndogo anaweza kukwepa hilo na ukikwepa ujue hawapo au gari yako ni ya Serikali labda wanaweza kupunguza makali. Police hapo wamepageuza pa kujipatia fedha.

Watu wengi humu wanajua kufuata sheria kwa 100% ndio usalama wenyewe la hasha. Unaweza kusababishiwa ajali huku wewe ukiwa kwenye haki.
 
Sidhani kama umesoma driving school ama ndio kama sisi wa kununua leseni.
Brother mlima kitonga unaovertake? Kweli?
Halafu unasimamishwa unaanza kulalamika kweli brother?
Una familia brother? Una mke na watoto?
Magari yanaua brother, ajali za barabarani zinaua. Usicheze na maisha yako.
Huyaoni Magari yaliyoanguka chini pale kitonga?
Muulize kigwangala, ajali haziangalii wewe ni kiongozi ama raia wa kawaida.
Jifunze defensive driving hii course hata online unaipiga utajua nini maana ya kuendesha gari kwa usalama wako
Kuna makosa yanafanywa na Tanroad katika alama za barabarani na usalama wake
Mlima kitonga una km 9 , huwezi ukaweka katika foleni magari yote kwa km nyingi hivo.
Ni hatari pia kulifata nyuma gari la mzigo kwa umbali.mrefu,
Kitonga palitakiwa pawe na sehemu za ku overtake , Askari wanaishi na udhaifu wa Tanroad.
 
Kinachosikitisha wao wenyewe hawafwati
 
Kuna makosa yanafanywa na Tanroad katika alama za barabarani na usalama wake
Mlima kitonga una km 9 , huwezi ukaweka katika foleni magari yote kwa km nyingi hivo.
Ni hatari pia kulifata nyuma gari la mzigo kwa umbali.mrefu,
Kitonga palitakiwa pawe na sehemu za ku overtake , Askari wanaishi na udhaifu wa Tanroad.
Upo sahihi sana na ndio maana nimetoa mfano wa Sekenke. Huwezi fika sehemu ambayo unaweza kuona mbele zaidi ya mita 600 then usi overtake wakati mbele hakuna kinachokuja na bado eti utembee speed ya 30kph. Hiyo speed ingewekwa kwa malori na gari ndogo iwe hata 50 sio mbaya.
 
Nimepita mara nyingi Kitonga na basi na ma Dereva wanaovertake kama kawaida
 
Sidhani kama umesoma driving school ama ndio kama sisi wa kununua leseni.
Brother mlima kitonga unaovertake? Kweli?
Halafu unasimamishwa unaanza kulalamika kweli brother?
Una familia brother? Una mke na watoto?
Magari yanaua brother, ajali za barabarani zinaua. Usicheze na maisha yako.
Huyaoni Magari yaliyoanguka chini pale kitonga?
Muulize kigwangala, ajali haziangalii wewe ni kiongozi ama raia wa kawaida.
Jifunze defensive driving hii course hata online unaipiga utajua nini maana ya kuendesha gari kwa usalama wako
Point
 
Habari zenu wapendwa ,naamini bado mpo na hangover ya furaha ya did.Kuna Jambo ningependa kuliweka hapa nikiamini mamlaka husika wanaweza kulipitia na kuliangalia upya.
Last week nilikuwa na safari ya kuelekea nyanda za juu kusini . Bahati nzuri nilifankiwa kupata lifti kwa jamaa yangu mmoja alikuwa na safari ya uelekeo huo. Kufika pale kitonga kama kawaida unakutatana na mabango mbali mbali ya tahadhari ukitahadharishwa juu ya hatari ya mlima na kwa bahati mbaya mlima mzima huruhusiwi ku overtake. Basi tulipoanza kuupanda mbele kidogo tukakutana na malori manne yamesheheni mzigo tukayafwata kwa taratibu kwa dk kadhaa kufika mbele kidogo akaona upenyo (kwenye mlima kuna sehemu wamepanua barabara kwenda kushoto) jamaa akatanua kwenda kushoto kabisa akapata upenyo wa kupita..kwenda mbele kidogo tukakutana na malori mengine.tukayafwata na tulipofika kona iliyo vikzuri tukachomoka kama kawaida .kazi ikawa ni kuangalia usalama na kuchomoka ..kufika kat Kati ya mlima tukakutana na trafki akatupiga mkono tukae pembeni..tuliposhuka akatuita na kutuonyesha kwamba mmeanza kucheza rafu kuanzia kuleee.kumbe bwana waliposimama wanauwezo wa kuona barabara kuanzia mwanzo wa mlima ..
Tukamsikiliza kisha nikamuuliiza kwa hiyo huu mlima wote haturuhusiwi ku overtake ?
Akanijibu kwa hasira hujui Alama za barabarani ? Umesona uderava kweli?
Nikamjibu mbona hujajibu swali langu?
Nikamwomgezea swali lingine..kwa hiyo mimi mwenye gari dogo Natakiwa niwe nyuma ya malori haya hadi mwisho..hamuoni kwamba ni hatari na upotevu wa muda?
Nikaona anazidi kuwa mkali..yaani wewe badala ya kuomba msamaha unajifanya kuhoji na kujifanya mjuaji?
Nikamjibu sioni sababu ya kuomba msamaha kwa sababu kiuhalisia huu mlima hakuna gari dogo litakalofwata hiyo sheria yenu hata ninyi wenyewe hamuwezi kuifwata..huu niuonevu wa wazi yaani haina tofauti na vibaka wa usiku..mzee akawaka na kusema huyu lazima aandikiwe maana anajifanya mjuaji..nikamwambia jamaa yangu wacha waandike nitakulipia..hakuna kuwapa hela ni bora niichangie serikali yangu.
Mara ghafla wakalisimamisha gari lingine dogo kwa kosa lile ..alipofungua kilo kumbe wanafahamiana wakaanza kuchekena na kupigishana story kisha akamtakia safari njema.nikamuliza huyu jamaa alikuwa nyuma yangu na malori niliyoanza nayo mimi bado nayaona yaleee kwenye kona ya pili ya mlima..ina maana huyu Nae aliyapita ..mbona mmemwachia?
Wakajibu usitufundishe kazi wewee..sisi ndio wenye mlima..nikabaki nashangaa huku nikimwomba amalizie kutuandikia tuendelee na safari..wakati anandika yakapita malori matatu na fuso nyuma yake. Akamwambia dereva wa fuso acha kulal overtake weweee.jamaa akaovertake..nikamuuliiza na hii tunaiitaje ? Akajibu mm ndio mtu wa usalama nimemruhusu ....nikabaki nashangaa.
Kabla sijaondoka nikaliona gari walilopaki pembeni..nikacheka Sana wakaniuliza wacheka nini.
Nikawambia mwaka huu January nilisafiri toka makambako nikapita hapa..kufika ilula huwa hamruhusu ku overtake kabisa ingawa pako vizuri.ghafla nikapitwa kwa kazi na hii gari na mbele kulikuwa na malori kadhaa akayapita tena. Kuna jamaa akaamua kuwaiga hakufika hata mbali akadakwa akaandikiwa ..bahati nzuri mi napafahamu nikawa mpole..kufika kabla ya mlima nikalikuta hili gari lenu mmepaki ..ndio nikagundua kumbe ni trafki ndio maana hamkusimamishwa..wakati nashuka mlima mkaja tena mkanipita kwa kasi na malori kadhaa mbele nikaja nikawakuta hapa ..sasa hizi sheria nyie haziwahusu au?
Wakanijibu kwa hasira tumeshakuandia naomba uondoke..nikawauliza kama mnasena huu mlima ni hatari ina maana hiyo hatari iko kwetu tu? Ila kwa maaskari na jmaa zao Wana kinga.? Nikaona wamekuwa wakali na kurudi kwenye ofisi yao..
Naomba serikali wauangalie huu mlima vizuri..wasitugeuze raia kama chanzo cha mapato.Ni kwa nn mtunge sheria ambayo hta ninyi hamuwezi kuifwata?
Wameelekezwa kutotumia vibaya hizo sheria. Sheria zina nia ya kurekebisha, siyo kuumiza wananchi. Pia zisitumike kama Chanzo cha mapato ya Serikali.
 
Sidhani kama umesoma driving school ama ndio kama sisi wa kununua leseni.
Brother mlima kitonga unaovertake? Kweli?
Halafu unasimamishwa unaanza kulalamika kweli brother?
Una familia brother? Una mke na watoto?
Magari yanaua brother, ajali za barabarani zinaua. Usicheze na maisha yako.
Huyaoni Magari yaliyoanguka chini pale kitonga?
Muulize kigwangala, ajali haziangalii wewe ni kiongozi ama raia wa kawaida.
Jifunze defensive driving hii course hata online unaipiga utajua nini maana ya kuendesha gari kwa usalama wako
Yaani wewe ni boya kabisa kwenye barabara, kaa kimya. Ulishawahi kuona jinsi yale malori yanavyonyata kupandisha ule mlima, Unajua ni hatari kiasi gani kulifuata hilo lory kwa nyuma, Je unaelewa foleni itakayosababishwa kwa magari yote Kuamua kufuata hiyo sheria ulihofundishwa na hicho chuo chako ngumbalu?. Je wajua watunga hizo sheria za barabara huwa wanakosea.Au hujui wale Trafick wanajua kabisa kwamba pale huwezi kufuata Sheria zilizowekwa kutoka na Mazingira hatalishi ya ule mlima, na wapo pale kwa ajili ya kutumia udhaifu wa sheria na wanaamua ndiyo Eneo lao la kupigia pesa. Jifunze kukaa kimya kwa usichokijua ili uelimike
 
Upo sahihi kabisa. Maisha yako hayana maana yoyote kwangu.
Ovateki nenda hata 180km/h
 
Binafsi nilikuwa siujui mlima kitonga na vyanzo vya ajali. Nimeangalia video zake wala hautishi tatizo ni kona nyingi wala sio mlima. Najaribu kulinganisha na milima ya uluguru kuanzia Maeneo ya Lolo, mgeta, nyandira mpaka masalawe. Kitonga ni cha mtoto sana tena ni kichanga nina Ndugu yangu ni dereva wa Toyota Dyna engine 14B anabeba abiria kutoka Moro mpaka mgeta huwa kwa kawaida dereva wa njia hiyo lazima uwe mzoefu na gari usizidishe mizigo kuofia kushindwa kupanda milima. Kitonga ni kona tu mlima cha mtoto. Siku nilenda tembea naye akawaambia abilia "Leo mizigo mingi sana sishushimzigo wa mtu ila gari ukishindwa kypanda mlima basi" waluguru walikuwa kimya kwenye gari mpaka wameimaliza milima ya uluguru. Gari inatumia masaa 2 kuimaliza milima hiyo. Kitonga ni kona tu
 
Uzi umesaidia kukimbiza mwizi, leo nimepita hakuna Askari trafiki kitonga , nadhani wameusoma huu uzi.
 
Back
Top Bottom