Polisi wakorogana

Kama jeshi limefikia hatua ya kuvisha wahuni uniforms ili tu kuidhibiti chadema basi kazi ipo.
Dada Mwajei, usiamini kila kinachoandikwa na waandishi kuwa ni kweli, ningekuwa mimi ndio mhariri wa Tanzania Daima, nisingeruhusu kauli hiyo kwenye gazeti langu bila uthibitisho!. Ukisikia habari za uzushi ndizo hizo!. Hakuna mtu mwenye akili timamu, anaweza kuamini uzushi huo, eti Jeshi la polisi, limewachukua vijana wahuni wa mitaani na kuwavisha sare za polisi na kuwapa silaha ili waidhibiti Chadema!, that is too cheap!. Ni vitu vido vidogo kama hivi, vinaiweka credibility ya Tanzania Daima kwenye mizani!.

Pasco.
 
Someone in Tanzania please put on the lights
By CHARLES ONYANGO-OBBO

Posted Saturday, September 8 2012 at 20:56

In Summary

•Several policemen set upon Mwangosi, and one of them fired a teargas canister at close range at his torso. It ripped the journalist apart, and he collapsed with his intestines and everything else scattered about in a heap.
•While journalists have been killed in several countries in Africa, none of them had been murdered in this bizarre fashion.
•There was always the hope that the violent demons that have convulsed all of Tanzania's neighbours, would spare it so that we could all argue that it was actually possible for a country in our region to be peaceful.
•The beating and killing of Mwangosi, though, was captured on camera. In this case, the police were probably emboldened because they expected they would get away with it.
•It is this combination of rogue forces and impunity that should worry Tanzanians – and East Africa. You are actually better off when a government orders the police to beat and kill citizens.
•Rogue forces, shadowy militias, or state operatives who are above the law, are a different type of nightmare. They behave like the vampires in the movies.

The killing of Tanzanian TV journalist Daudi Mwangosi last week shocked the country as well as people in East Africa and around the world who still have a view of it as a gentle land.


Several policemen set upon Mwangosi, and one of them fired a teargas canister at close range at his torso. It ripped the journalist apart, and he collapsed with his intestines and everything else scattered about in a heap.


While journalists have been killed in several countries in Africa, none of them had been murdered in this bizarre fashion.


Mwangosi, who was covering skirmishes between the police and the opposition Chadema, was the first journalist to be killed in the line of work in Tanzania, but you don't need 20 dead scribes to worry about the direction a country is taking.


There was always the hope that the violent demons that have convulsed all of Tanzania's neighbours, would spare it so that we could all argue that it was actually possible for a country in our region to be peaceful.


That is turning out to be a misplaced hope. In an incident not too dissimilar, two months ago, Dr Steven Ulimboka, leader of a group of striking doctors, was kidnapped, tortured and dumped in a forest outside Dar es Salaam.


His tormentors left him for dead. He was lucky. A local man noticed a bound and battered man twitching, and saved him.

President Jakaya Kikwete denied reports that his government was behind the kidnap and torture of Ulimboka.


It probably wasn't, in the sense that orders were not given from the top. But that does not mean rogue security elements cannot take matters into their own hands.


The beating and killing of Mwangosi, though, was captured on camera. In this case, the police were probably emboldened because they expected they would get away with it.


It is this combination of rogue forces and impunity that should worry Tanzanians – and East Africa. You are actually better off when a government orders the police to beat and kill citizens.


That is because such a government can be shamed into changing its ways, compensating victims' families, and the offending officer can be privately sued. And, in a country where you have free elections, a murderous government can always be voted out of office.


Rogue forces, shadowy militias, or state operatives who are above the law, are a different type of nightmare. They behave like the vampires in the movies.


They get a taste of blood today, and tomorrow they want two sips, and next week they want three sips of blood. As they suck more blood, they grow stronger, multiply their kind, and before you know it they take over the town.


Before long, they take over the government, and own the president.


Which raises the question. If indeed Tanzania has a growing vampire problem, what will they do if in the future the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) that they feed off, loses an election?


Will they allow the opposition to take power? You can bet your left hand they won't.


Hopefully someone in Tanzania will turn on the lights and scare the vampires away before it is too late.


Charles Onyango-Obbo is Nation Media Group's executive editor for Africa & Digital Media. E-mail: cobbo@ke.nationmedia.com. Twitter: @cobbo3
 
Pasco,

..kuna vijana[ Mkeshaji, marejesho] wanataka kujua "MLINZI WA AMANI" ni nani.

..tunaomba msaada wako wa kisheria.

..natanguliza shukurani.

NB:

..mimi jina "mlinzi wa amani" nilisikia miaka ile ya kesi ya uhaini, na sijakutana nalo tena.
 
Last edited by a moderator:
Dada Mwajei, usiamini kila kinachoandikwa na waandishi kuwa ni kweli, ningekuwa mimi ndio mhariri wa Tanzania Daima, nisingeruhusu kauli hiyo kwenye gazeti langu bila uthibitisho!. Ukisikia habari za uzushi ndizo hizo!. Hakuna mtu mwenye akili timamu, anaweza kuamini uzushi huo, eti Jeshi la polisi, limewachukua vijana wahuni wa mitaani na kuwavisha sare za polisi na kuwapa silaha ili waidhibiti Chadema!, that is too cheap!. Ni vitu vido vidogo kama hivi, vinaiweka credibility ya Tanzania Daima kwenye mizani!.

Pasco.
Pasco, nani angeamini kwamba polisi mlinda amani alimwelekezea marehemu Mwangosi mtutu wa tear gas cannister louncher kwenye tumbo na kisha kumlipua? Kama kusingekuwa na picha zile?
I bet hata wewe Pasco ungekataa kwamba tear gas canister lilitumika, labda hata mimi ningesema polisi aliyefunzwa asingeweza kufanya kitu kama hicho.

Ni afadhali kuwa na maswali kuliko kujiaminisha kama ufanyavyo, hawaaminiki hawa.
 
Last edited by a moderator:
Pasco,

..kuna vijana[ Mkeshaji, marejesho] wanataka kujua "MLINZI WA AMANI" ni nani.

..tunaomba msaada wako wa kisheria.

..natanguliza shukurani.

NB:

..mimi jina "mlinzi wa amani" nilisikia miaka ile ya kesi ya uhaini, na sijakutana nalo tena.
Mkuu Joka Kuu, naomba kukujibu kama layman tuu, kwa sababu mimi sii mwanasheria per se, posession ya LL.B pekee hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria, hivyo jibu langu hapa sii la kisheria kwa sababu haliandamani na vifungu.

Mlinzi wa amani ni mtu anaetakiwa kuwepo, wakati mtuhumiwa anatoa statement kwa polisi itakayotumika kama ushahidi rasmi mahakamani katika kesi za jinai ambazo adhabu yake ni kifo (capital punishment). Mara nyingi mlinzi huyu wa amani sii lazima awe ni mwanasheria, bali lazima awe ni mtu wa integrity ili kuaminika na jamii husika na awe tayari kuja mahakani kutoa ushahidi kuhusu statement husika, mfano Ofisa wa serikali wa kuanzia ngazi ya mwandamizi mfano RC, DC, Jaji, Hakimu, Kiongozi wa dini, kiongozi wa kimila, Mzee wa Kijiji etc.

Lengo rasmi la kutumia mlinzi wa amani, ni kuithibitishia mahakama kuwa umetoa maelezo yako ukiwa huru bila shinikizo lolote, ili kuyapa maelezo hayo matakwa ya kisheria (force of law) kuweza kutumika mahakamani kama ushahidi (addmisability of evidence).

Miongoni mwa statements zinazotakiwa kutolewa mbele ya mlinzi wa amani ni za kesi za mauaji na uhaini.

Kunapotokea kifo, watuhumiwa hushikwa na polisi kuchukua maelezo yao, hao watuhumiwa huweza kukiri kuhusika moja kwa moja au kukanusha. Ili kuithibitishia mahakama kuwa mhusika ametoa maelezo akiwa huru na kwa ridhaa yake, mara baada ya polisi kuyapata maelezo yale, humtafuta mlinzi wa amani, mtu mwingine ambaye ni independent nje ya jeshi la polisi, awepo wakati mtuhumiwa akitoa maelezo ili asije baadae akayaruka mahakama, au akadai aliyatoa kwa shinikizo!.

Kwenye sheria yetu ya ushahidi (evidence act) ushahidi wowote utakaotolewa kwa shinikizo lolote, unakuwa batili (not addmisable), hivyo ili polisi kulinda haki zao na za mshatakiwa, ushahidi huu lazima urekodiwe mbele ya mlinzi wa amani ili kuupa nguvu ya kisheria!.

Ni ukweli isiofichika, polisi hutumia mbinu mbali kwa watuhumiwa ili kupata "confession", mbinu hizi ni pamoja na torture, polisi wakishapata maelezo hayo, hawawezi kuyatumia mahakamani mpaka yatolewe na mtuhumiwa akiwa huru bila shinikizo lolote, ndipo sasa humtongoza mtuhumiwa kuyatoa tena maelezo yake mbele ya mlinzi wa amani sometimes hata kwa kumwahidi, kuwa hata shitakiwa!.

Kwenye ile kesi ya uhaini, tulishuhudia mara kibao, washitakiwa wakiyakana maelezo yao waliyatoa mbele ya walinzi wa amani na kuipelekea mahakama ifanya "trial within trial" ili kuyadhibitisha kwanza hayo maelezo ndipo ifikie uamuzi wa kuyakataa, na kwenye kesi ile, maelezo ya washtakiwa wakuu wote yalikataliwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa watuhumiwa waliteswa sana na kulazimishwa kukiri, nao wakakubali kukiri na kutoa maelezo ya ushiriki wao mbele ya walinzi wa amani ili tuu kuepuka mateso na hatimaye kuja kuyakana mahakamani.

Kwa polisi wetu wa kifo cha Daudi Mwangosi, ukiona tuu kesi inapandishwa mahakamani basi ujue polisi hao watafanywa mbuzi wa kafara kwa kushitakiwa tuu ili kutuliza hasira za wananchi kwa kuonyeshea kuwa waliyatenda waliyoyatenda bila kupokea amri kutoka juu, ili kuwangikia kifua wauwaji halisi!.

Huyo polisi aliyefyatua bomu, yeye ni mtekelezaji tuu, muuaji halisi ni aliyetoa amri ya mabomu yavurumushwe!.

Pasco.

 
anafanya kitu kinachoitwa confession (kukiri) mara nyingi hufanywa mbele hakimu wa mahakama ya mwanzo.
 
CCM wamedhamiria kuleta vita na machafuko nchini ili kulinda himaya na maslahi yao tu.

Watawala hawa wamedhani nchi hii ni personal property yao. Kwa sasa wananchi tunajitahidi sana kuwavumilia huku tukiwaelimisha lakini kama itabidi kupigana, kwa kulazimishwa na CCM, tutapigana nao kwa silaha zote ktk umoja wetu na hakika yake tutawashinda.

Imagine kuwavalisha wahuni sare za jeshi na kuwapa silaha (zilizonunuliwa na kodi za wananchi) huku RPC na RCO (na pengine IGP) wakiwa na taarifa. Ni wazi zile kambi zao za kigaidi sasa zimekuwa sehemu ya jeshi la Polisi. Mambo ya Intarahamwe, mambo ya kuwa na vikundi vya wanamgambo wenye silaha ndio CCM wanakoelekea.

Jakaya Kikwete katulia tuli anaangalia kama mtazamaji.
 
Niwaombe wananchi wenzangu kuwa, pamoja na uozo na ukatili wa Police Tanzania lakini tukumbuke kuna nafasi ya kupata ushirikiano wao (polisi) katika wakati huu jeshi linapopita kwenye chekeche la umma.

Hivyo tuwatie moyo askari polisi wachache ambao ni wazalendo wa ukweli, kuja mbele na kutoa taarifa zenye ushahidi za uharamia na umafia wa CCM kwa jeshi lao.
 
Ndugu yangu viongozi wa nchi hii wanadhani wanamarefu yenye ncha,kamanda kamuhanda anajiandaa kugombea ubunge baada ya kustaafu polisi,STEVEN WASIRA anaona bila kufuta CDM inachukua dola kiulaini 2015,KATIKA HALI YA KUTUMIA POLISI DHIDI YA CHADEMA,CCM IMEKOSA VIONGOZI WENYE WELEDI KWA NYAKATI HIZI.MBINU ILIYOBAKI DHIDI YA CDM NI KUFUTA TU,SASA WAJARIBU KUFANYA HIVYO KAMA WAMEICHOKA AMANI YA NCHI HII,WENYE UKIMWI NDANI YA CCM WASIWASABABISHIE WENZAO WDNYE AFYA SINTOFAHAMU.

Sidhani kama hilo wazo la kuifuta chadema wamelitafakari vya kutosha. Sipati picha pale vijana katika kila mkoa watakapo lianzisha kupinga hiyo hatua. Bora walifutilie mbali wazo la kuifuta chadema.
 
Dada Mwajei, usiamini kila kinachoandikwa na waandishi kuwa ni kweli, ningekuwa mimi ndio mhariri wa Tanzania Daima, nisingeruhusu kauli hiyo kwenye gazeti langu bila uthibitisho!. Ukisikia habari za uzushi ndizo hizo!. Hakuna mtu mwenye akili timamu, anaweza kuamini uzushi huo, eti Jeshi la polisi, limewachukua vijana wahuni wa mitaani na kuwavisha sare za polisi na kuwapa silaha ili waidhibiti Chadema!, that is too cheap!. Ni vitu vido vidogo kama hivi, vinaiweka credibility ya Tanzania Daima kwenye mizani!.

Pasco.
Pasco hiyo statement imenishangaza sana na ndio sababu nikasema kama jeshi limefikia hatua hiyo basi kazi ipo. Maana ni ngumu kuamini kama kitu kama hicho kinaweza kufanyika. Mtu anayekabidhiwa silaha za jeshi iwe polisi au JWTZ ni yule anayeaminika kuwa amepitia na kufuzu mafunzo ya kutumia silaha hizo.
 
Last edited by a moderator:

Kwa polisi wetu wa kifo cha Daudi Mwangosi, ukiona tuu kesi inapandishwa mahakamani basi ujue polisi hao watafanywa mbuzi wa kafara kwa kushitakiwa tuu ili kutuliza hasira za wananchi kwa kuonyeshea kuwa waliyatenda waliyoyatenda bila kupokea amri kutoka juu, ili kuwangikia kifua wauwaji halisi!.

Huyo polisi aliyefyatua bomu, yeye ni mtekelezaji tuu, muuaji halisi ni
aliyetoa amri ya mabomu yavurumushwe!.

Pasco.


kwenye red hapo mkuu kwani hauwezi ukafanyika uchunguzi akakamatwa aliyetoa amri ya kuvurumisha mabomu? na huyo mlinzi wa amani ni nani katika vurugu za Nyororo? nimeuliza baada ya kuona umetoa maelezo mazuri juu ya mlinzi wa amani.....
 
Pasco hiyo statement imenishangaza sana na ndio sababu nikasema kama jeshi limefikia hatua hiyo basi kazi ipo. Maana ni ngumu kuamini kama kitu kama hicho kinaweza kufanyika. Mtu anayekabidhiwa silaha za jeshi iwe polisi au JWTZ ni yule anayeaminika kuwa amepitia na kufuzu mafunzo ya kutumia silaha hizo.

hao Polisi kama waliwavalisha vijana wa mitaani uniform wali apply quote ya Albert Enstein "Anyone who has never made a mistake has never tried anything new
 
hata raia wa kawaida asiye askari ni "mlinzi wa amani"....kwa kauli hii ni sawa na kusema " marehemu alipatwa na umauti kutokana na "flying object"
 
This is an "invitation of criminal acts in a pieceful country". Na inasemekana hata mafunzo hawakupata.Kama habari hizi ni za kweli, wa kwanza kujiuzulu ili kupisha tume huru itakayomfikisha kwa pilato ni IGP, wa pili ni RPC kwa kukiuka taratibu , sheria na kanuni za jeshi hilo linalopaswa "kulinda raia na mali zao" Ingawa kwa kawaida(si mimi ni sheria za kimataifa) Askari mmoja anapaswa kulinda raia kati ya 450 hadi mia 500. Ila kwa Tanzania (Nchi ya 23 barani Afrika kwa bajeti kubwa kupelekwa jeshini-Majeshi yote) askari mmoja anawajibika kulinda raia kati ya 1200 hadi 1400(kinyume na sheria za kimataifa.

Wakati huohuo wako vijana mtaani ambao wana uwezo wa kulitumikia jeshi hilo ambao hawapewi mafunzo ili wawe askari na kuzijba pengo kubwa la raia kati ya 700 na 800 ambao badala ya kulindwa, wanawindwa na hao "walinzi wa amani" kwa mabomu bila hatia yeyote, tena kwa amri ya mtu ambaye hana uwezo kisheria kuzuia matakwa yao bali kuyakubali( RPC).

Haya yote (kukosa ajira kwa hao vijana) ni Uzembe na Upuuzi wa CCM na kaulimbiu zembe kama "Maisha bora kwa kila, narudia kusema "kwa kila" Mtanzania, na ahadi hewa ya "Nitatengeneza ajira mpya kwa vijana milioni moja (1,000,000) kila mwaka".

CCM iondolewe madarakani haraka iwezekanavyo, na iundwe tume huru na UN kuichunguza kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa UN. Ndugu zangu CCM ni janga la taifa.
 
Halafu eti yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama (Ingawa hakupaswa kuitwa Amiri Jeshi Mkuu Wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, huwa ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi-(Commander -In-Chief) as per Former Lt Col, then Col. (RTD) Benjamin Msuya ambaye katika vita vya Uganda 1978, batalion yake ndio ilikuwa ya kwanza kuingia Ikulu ya Uganda na kama sheria za kimataifa zingekuwa zinamruhusu, alipaswa kujitangaza kuwa yeye ndiye rais wa Uganda.

Kwa kufanya hivyo angeekuwa amepoteza maana halisi ya vita hivyo kwani Tanzania ndiyo ingeonekana imeivamia Uganda.
 
kwenye red hapo mkuu kwani hauwezi ukafanyika uchunguzi akakamatwa aliyetoa amri ya kuvurumisha mabomu? na huyo mlinzi wa amani ni nani katika vurugu za Nyororo? nimeuliza baada ya kuona umetoa maelezo mazuri juu ya mlinzi wa amani.....
Mkuu Manyanza, uchunguzi wa nini?, mtoa anajulikana, amri haikusema fyatua bomu tomboni kwa mwandishi but ilikuwa too general, vurumisha mabomu kuwatawanya Chadema!, ni katika vurumisha hiyo, bomu moja likafyatuka na kumtawanya mwandishi!.

Mlinzi wa amani ni mtu tuu wa kawaida mwenye hadhi fulani katika jamii, usually kiongozi, ambaye atakuwepo, wakati askari aliyefyatua bomu lililosababisha kifo, atakapokuwa anahojiwa na kutoa maelezo yake yatakayotumika kama ushahidi mahakamani.
 

Polisi wakorogana
• Anayetuhumiwa kuua mwandishi akwama kufikishwa mahakamani

na Abdallah Khamis
Tanzania Daima


WINGU jeusi limeendelea kutanda ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Iringa baada ya baadhi ya askari mkoani humo kunyoosheana vidole kuhusu tukio la polisi kuua mwandishi, huku baadhi yao wakimlaumu Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Michael Kamuhanda.

Askari kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa siri jana, walisema kama RPC angesikiliza ushauri wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) kuhusu namna ya kukabiliana na wanachama wa CHADEMA, maafa yasingetokea.

Walisema Kamuhanda ndiye aliwaamuru askari wake kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano wa ndani wa ufunguzi wa tawi katika Kijiji cha Nyololo, kwa maelezo kuwa hakuwaruhusu kufanya hivyo.

“Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa,” alidokeza mmoja wao.

Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia. Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.

Baadhi yao walisema hata maneno na vitisho vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, kwamba CHADEMA kina vurugu, ni uonevu na propaganda za kisiasa, kwani vurugu zilitokea pale CHADEMA walipoanza kutawanywa.

Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka mkoani humo zinadai kuwa baadhi ya askari waliohusika kwenye vurugu hizo si polisi halali wa jeshi hilo, bali ni vijana wa mtaani ambao walivishwa sare kwa lengo la kuwadhibiti CHADEMA, ndiyo maana walikuwa wakibabaika katika matumizi ya silaha.

Wakati huo huo, jeshi hilo jana lilishindwa kumfikisha mahakamani askari polisi anayetuhumiwa kufyatulia bomu lililomchanachana na kumuua mwandishi wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Awali, taarifa za mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani zilizagaa kila kona; gazeti hili likapiga kambi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, lakini mtuhumiwa hakuletwa mahakamani.

Jana gazeti hili liliripoti taarifa za kukamatwa kwa siri na kuhojiwa kwa askari watano kati ya saba akiwamo yule anayetuhumiwa kumuua marehemu Mwangosi.

Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi ni wale walioonekana kwenye picha mbalimbali za magazeti na mitandao wakimpiga marehemu huyo kabla ya kumsababishia kifo.

Habari za ndani zilieleza kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji hakuweza kufikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa kutokana na kuendelea kutoa maelezo mbele ya mlinzi wa amani.

Chanzo cha taarifa kilidai kuwa utaratibu huo wa kutoa maelezo ulianza juzi na huenda mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Jumatatu.

“Suala la mauaji ni kubwa, si kama mashitaka ya mwizi wa kuku au karanga. Hivyo, juzi na jana yule bwana alikuwa anaendelea kutoa maelezo yake kwa mlinzi wa amani. Sasa suala la kukiri kuua au kutokuua litabaki katika moyo wake,” kilisema chanzo hicho.


Hili la askari anayetuhumiwa kumua Mwangosi kuwa siyo Askari wa jeshi la polisi bali ni mamluki nimenistua sana.
 
Back
Top Bottom