Polisi wakorogana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wakorogana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 8, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Polisi wakorogana
  • Anayetuhumiwa kuua mwandishi akwama kufikishwa mahakamani

  na Abdallah Khamis
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]WINGU jeusi limeendelea kutanda ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Iringa baada ya baadhi ya askari mkoani humo kunyoosheana vidole kuhusu tukio la polisi kuua mwandishi, huku baadhi yao wakimlaumu Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Michael Kamuhanda.

  Askari kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa siri jana, walisema kama RPC angesikiliza ushauri wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) kuhusu namna ya kukabiliana na wanachama wa CHADEMA, maafa yasingetokea.

  Walisema Kamuhanda ndiye aliwaamuru askari wake kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano wa ndani wa ufunguzi wa tawi katika Kijiji cha Nyololo, kwa maelezo kuwa hakuwaruhusu kufanya hivyo.

  "Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa," alidokeza mmoja wao.

  Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia. Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

  Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

  Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.

  Baadhi yao walisema hata maneno na vitisho vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, kwamba CHADEMA kina vurugu, ni uonevu na propaganda za kisiasa, kwani vurugu zilitokea pale CHADEMA walipoanza kutawanywa.

  Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka mkoani humo zinadai kuwa baadhi ya askari waliohusika kwenye vurugu hizo si polisi halali wa jeshi hilo, bali ni vijana wa mtaani ambao walivishwa sare kwa lengo la kuwadhibiti CHADEMA, ndiyo maana walikuwa wakibabaika katika matumizi ya silaha.

  Wakati huo huo, jeshi hilo jana lilishindwa kumfikisha mahakamani askari polisi anayetuhumiwa kufyatulia bomu lililomchanachana na kumuua mwandishi wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

  Awali, taarifa za mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani zilizagaa kila kona; gazeti hili likapiga kambi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, lakini mtuhumiwa hakuletwa mahakamani.

  Jana gazeti hili liliripoti taarifa za kukamatwa kwa siri na kuhojiwa kwa askari watano kati ya saba akiwamo yule anayetuhumiwa kumuua marehemu Mwangosi.

  Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi ni wale walioonekana kwenye picha mbalimbali za magazeti na mitandao wakimpiga marehemu huyo kabla ya kumsababishia kifo.

  Habari za ndani zilieleza kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji hakuweza kufikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa kutokana na kuendelea kutoa maelezo mbele ya mlinzi wa amani.

  Chanzo cha taarifa kilidai kuwa utaratibu huo wa kutoa maelezo ulianza juzi na huenda mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Jumatatu.

  "Suala la mauaji ni kubwa, si kama mashitaka ya mwizi wa kuku au karanga. Hivyo, juzi na jana yule bwana alikuwa anaendelea kutoa maelezo yake kwa mlinzi wa amani. Sasa suala la kukiri kuua au kutokuua litabaki katika moyo wake," kilisema chanzo hicho.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni uonevu na propaganda za kisiasa zinazosimamiwa na CCM. Tunajua Polisi waseme ukweli tu.
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,244
  Likes Received: 12,964
  Trophy Points: 280
  Ukiona haya jua mwisho wao u karibu na ipo siku serikali yao.haitakuwa madarakani sijui watakimbilia upande upi maana ni sawa na marafiki zao watakuwa kikaangoni
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Mlinzi wa amani", naona limerudiwarudiwa hilo neno; ni nani huyo?
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hata mie nataka kumjua huyo 'Mlinzi wa amani'!!
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Haya matendo ya RPC yanafanywa na mtu anaekaribia kufa,nafikiri siku zake zimekaribia
   
 7. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hasira zangu bado ziko kwa kamhanda na chago-njaaa tu hamna mwingine.
   
 8. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  inawezekana ndo huyo a.k.a INTELIJENSIA YA POLISI?
   
 9. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kama jeshi limefikia hatua ya kuvisha wahuni uniforms ili tu kuidhibiti chadema basi kazi ipo.
   
 10. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini huyu mlinzi wa amani asimuhoji kamuhanda ambaye kabla hajaja amani ilikuwepo na ikatoweka mara baada ya yeye kuja pia kwanini asimuhoji waziri wa mahusiano na uratibu ndg wasira ambaye anapaswa kujua uhusiano wa polisi na makundi mengine ya kijamii kwamba ni salama kabisa kiasi kwamba waislamu wanaovunja sheria za nchi wanaishika ****** serikali kwa kuandamana tena palepale ikulu na ccm imenyamaza ila chadema ndio nongwa na wzr wa mambo ya ndani ambaye ndiye anayekubali kufanya kazi na shemeji ya kikwete ndg mwema,na pia mwenyekiti wa ccm ambaye wakati sensa inaendelea wao wanafanya uchaguzi bila kuingilia sensa ila chadema ni lazima wavuruge sensa?Pia tendwa ahojiwe kwakuropoka kama kopo la chooni kwamba eti atakifuta chadema na sio kufuta jeshi la polisi?
   
 11. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  View attachment 64381

  Chanzo chenyewe ndicho hiki. Jamaa walikuwa ndani kwenye ofisi ya chama chao (wakifungua TAWI) kama bendera inavyopeperuka. Ili kupisha zoezi la sensa, mikutano ya ndani iliruhusiwa, sasa baada ya RPC (Michael Kamuhanda) kutoa amri ya uvunjifu wa amani wa makusudi ndipo mtafaruku ulipoanza.
   
 12. K

  Konya JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  na nafikiri huu ni mpango ulioratibiwa mahsusi ili ku justify propaganda ya kuwa cdm ni chama cha vurugu thats why hata bwana tendwa aliamua kukurupuka kutoa kauli ya kutaka kuifutia usajili..kumbe kuna tawi la kwanza lilifunguliwa kwa amani na utulivu na tawi la pili ilikuwa hivyo mpaka kamhanda alivyoamua kuanzisha fujo yeye na askari wake
   
 13. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Hakika nimekerwa mno na hili tukio... ngoja tusubiri mwisho wake!
   
 14. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ama kweli nchi yetu imeisha kabisa. Kamhanda huyu anafanya nini huko aliko? Yeye ni mtuhumiwa wa kwanza katika haya mauwaji. Hili jeshi linalovalisha wahuni mavazi ni la wapi? eti wakaidhibiti CDM? Kwani CDM ni nani? Unaweza kumpa mtu silaha ataidhiti umma? Huu ni ukichaa ambao kama hautaangaliwa polisi wote wataingia vitani na wananchi.
  Nimesema mara nyingi watanzania tuamke tuwadhibiti watawala hawa katili na wauwaji. Hizo silaha zinatokana na jasho letu yaani kodi zetu. Huyu kamhanda analipwa na kodi zetu. Je anachoweza kukifanya ndicho hiki? Tuache unafiki tutafute haki tena kwa nguvu zetu zote. Shenzi kabisa Kamhanda. Siku inakuja!
   
 15. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Polisi ndio wanaovuruga amani Tanzania.
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  hii nchi inakoelekea sijui.....tusubiri tutaona tu
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawa wanafuata maagizo ya watu wenye nyadhifa za juu ndani ya magamba. Kinachotia moyo baadhi yao wameshaanza kuongea. Ila hili la kutumia wahuni toka mtaani kwa kuwapa uniforms na silaha za moto ili wakafanye mauaji linatisha sana.

   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  Sijui huo "Ulinzi wa amani" anaufanyia wapi.

   
 19. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu viongozi wa nchi hii wanadhani wanamarefu yenye ncha,kamanda kamuhanda anajiandaa kugombea ubunge baada ya kustaafu polisi,STEVEN WASIRA anaona bila kufuta CDM inachukua dola kiulaini 2015,KATIKA HALI YA KUTUMIA POLISI DHIDI YA CHADEMA,CCM IMEKOSA VIONGOZI WENYE WELEDI KWA NYAKATI HIZI.MBINU ILIYOBAKI DHIDI YA CDM NI KUFUTA TU,SASA WAJARIBU KUFANYA HIVYO KAMA WAMEICHOKA AMANI YA NCHI HII,WENYE UKIMWI NDANI YA CCM WASIWASABABISHIE WENZAO WDNYE AFYA SINTOFAHAMU.
   
 20. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,707
  Likes Received: 8,249
  Trophy Points: 280
  Mlinzi wa amani = Justice of the peace.
  A judicial officer with limited power
  whose duties may include hearing
  cases that involve civil controversies,
  conserving the peace, performing
  judicial acts, hearing minor criminal
  complaints, and committing offenders.
  Justices of the peace are regarded as
  civil public officers, distinct from
  peace or police officers. Depending on
  the region in which they serve,
  justices of the peace are also known
  as magistrates, squires, and police or
  district judges.
   
Loading...