Polisi wa usalama barabarani msitugombanishe na serikali

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Nalazimika kuja na post hii kutokana na matukio kadhaa ya hivi karibuni ambayo yanayojitokeza tukiwa barabarani tunakimbizana na mkate wetu wa kila siku. Nashindwa kuelewa kama matukio haya yanatokana na uwezo mdogo wa polisi wa usalama barabarani kuongoza magari au ni maelekezo maalumu ya serikali kwa jeshi hili ili kujiongezea makusanyo, mimi sijui. Lakini nalazimika kusimulia visa viwili vilivyojitokeza kati ya jumatatu hadi hii leo. Mojawapo lililonipata mimi mwenyewe ni la polisi wa pale mataa ya chang'ombe kuruhusu magari ya kutoka keko, mjini, na ya tazara, huku akiacha kuruhusu yale ya kutoka karume. Alirudia tendo hilo zaidi ya mara tatu, Nikaamua kumpigia honi ili kumkumbusha kwamba ametusahau. Kitendo hicho kikamkera akanambia namfundisha kazi na kuwaita wenzake ambao walinilazimisha nilipe faini kwa kushindwa kuheshimu ishara na maelekezo ya polisi. Cha kushangaza, ni kwamba mara tu baada ya mimi kulazimishwa kusogeza gari langu pembeni ili nipigwe faini, polisi huyu aliruhusu magari ya kutoka karume ambayo aliyasimamisha kwa muda mrefu.

Tukio la hivi juzi ambalo nililishuhudia pale mataa ya aghakan ni la polisi mwenye namba E7815 ambaye alimanusura asababishe ajali baada ya kujisahau na kuanza kuruhusu magari ya kutokea Aghakan hospital kabla ya kusimamisha yale ya kutokea salenda bridge ambayo ndiyo alikuwa anaendelea kuyaruhusu. Nilichoshuhudia ni dereva aliyekuwa mbele yangu kunusurika kugonga gari nyingine baada ya polisi kushindwa kuonyesha ishara sahihi. Cha kushangaza, badala ya polisi huyu kuomba radhi kwa kushindwa kuonyesha ishara sahihi, alimpiga faini huyu dereva aliyekuwa mbele yangu. Hata sijui alimwandikia kosa gani, lakini hata mimi niliyekuwa nyuma yake sikuona kabisa huyu polisi akitusimamisha.

Haya ni matukio ambayo nimeyashuhudia ndani ya wiki moja. Najiuliza hii ni mbinu mpya ya jeshi la polisi kuongeza makusanyo, au ni polisi mmojammoja anatafuta kiki ya kupandia cheo au hawa polisi ni wapya ambao wameingia kwenye idara ya usalama barabarani bila kupata mafunzo? Ni vizuri polisi mjaribu kutengeneza mahusiano mazuri na wananchi vinginevyo sisi hatutawachukia ninyi, tutaichukia serikali pamoja na chama tawala, kwa kudhani hayo ni maelekezo yao kwenu.
 
Tukio la hivi juzi ambalo nililishuhudia pale mataa ya aghakan ni la polisi mwenye namba E7815 ambaye alimanusura asababishe ajali baada ya kujisahau na kuanza kuruhusu magari ya kutokea Aghakan hospital kabla ya kusimamisha yale ya kutokea salenda bridge ambayo ndiyo alikuwa anaendelea kuyaruhusu. Nilichoshuhudia ni dereva aliyekuwa mbele yangu kunusurika kugonga gari nyingine baada ya polisi kushindwa kuonyesha ishara sahihi.



Ipo haja kufikiria kuongeza kifaa cha ku control speed ya hizo taa, kwa maana kwamba human error ni nyingi kuliko za machine, kukiwa na kifaa cha kuongera au kupunguza mpishano wa taa itasaidia kuondoa kabisa makosa ya kibinadamu ambayo yaweza kusababisha ajali mbaya. Polisi wenyewe kwa sasa ni kama wapo frustrated, tunasikia kasi ya kuongezeka kujipiga risasi ilivyo.
 
Muda mwingine na wao wana frustration zao.....kwa hiyo muwavumilie tu
Nakubaliana kabisa na wewe, kuna wakati kwa kweli hawa watu wanakuwa frustrated, na ukizingatia hilo agizo la kukamata na kutoza faini angalau magari kumi kwa siku naona kama limewachanganya kabisa, kwa hiyo wanakomaa tu hata kama wanajua kosa siyo la msingi. Kuna mmoja aliwahi kunikomalia nilipe faini eti kisa, tangu asubuhi hajapata gari hata moja la kulipiga faini, atarudije ofisini?? Sasa kauli kama hizi za polisi, unajiuliza mara mbilimbili kama hawa wapo kwa ajili ya kulinda usalama au kukusanya mapato. Kama huyo wa Aghakan kwa hakika, hakuwa na lingine isipokuwa kukusanya mapato tu, maana lile kosa ni dhahiri kwamba lilisababishwa na yeye mwenyewe.
 
Ipo haja kufikiria kuongeza kifaa cha ku control speed ya hizo taa, kwa maana kwamba human error ni nyingi kuliko za machine, kukiwa na kifaa cha kuongera au kupunguza mpishano wa taa itasaidia kuondoa kabisa makosa ya kibinadamu ambayo yaweza kusababisha ajali mbaya. Polisi wenyewe kwa sasa ni kama wapo frustrated, tunasikia kasi ya kuongezeka kujipiga risasi ilivyo.
Upo sahihi nchini nyingi sana za wenzetu, tayari wana huu mfumo wa taa zenye sensor, zinaweza kujua upande upi una magari mengi Zaidi kuliko upande mwingine. Sisi bado tunatumia analogue.
 
Upo sahihi nchini nyingi sana za wenzetu, tayari wana huu mfumo wa taa zenye sensor, zinaweza kujua upande upi una magari mengi Zaidi kuliko upande mwingine. Sisi bado tunatumia analogue.


Bado tunalilia manual
 
Back
Top Bottom