Nimekodi gari napeleka mzigo wangu kwa wanyalukolo kutoka dar. Kama kawaida ya magari ya mizigo,dar tumetoka usiku. Kufika kibaha mizani tukasimamishwa na polisi mmoja(hana sare ya trafic) umri wake ni kama miaka 25,dereva alipomsalimia akamwambia sasa, nipe chochote! Dereva mchaga, akamwambia hali ngumu. Aliangalia gari,akaturuhusu. Tulipofika mikese mida ya saa tisa usiku jumapili tukasimamishwa na polisi mwingine(hana sare ya trafic) umri wake kama miaka 28. Akamwambia dereva nipe kadi ya gari, dereva akajadiliana na kiongozi wake wa msafara,tumpe ngapi? Dogo akasema sina chenji(ule mtindo bado unatumika).dereva akampatia kadi tupu, yule polisi alizunguka gari akiangalia cha kukamata akakosa. Mara akauliza, wapi FIRST AID? Wakatoa ile kit wakampa, maskini kumbe kulikuwa hamna plaster! Akatuambia pakini gari pale.... Tukamsubiri kama dk 10 hakutokea, madogo ikabidi wamalizane naye kiaina na tukaondoka. Hivi kwani lazima kila anayepita akupe hela? Au mnapewa kiwango cha kukusanya? Pambaf sana.!