illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Maeneo ya mbagala wilaya ya temeke yamepakana na mkoa wa pwani ambao siku za hivi karibuni kumetokea matukio mengi ya uhalifu, binafsi ndipo napoishi, changamoto moja ni kwamba huwa nafika usiku sana napotoka kwenye vibarua leo nimeshuka kwenye daladala nasubiri kuchukua pikipiki mida ya saa tano unusu usiku nikawaona "jamaa" watano wamevaa kiraia huku wamebeba silaha nzito za moto mmoja wao alikuwa na radio call walikuwa wanaamuru maduka na biashara zingine zifungwe wakanikaribia maongezi yangu na yao yslikuwa kama ifuatavyo
Wao: wewe unafanya nini hapo usiku huu
Mimi:nimesimama
Wao:afande piga pingu huyo analeta dharau
Mimi:Naomba niwatambue
Wao:sisi ni askari tuko doria
Mimioleni kwa kazi ila ingekuwa ni vyema mngekuwa na sare kwani kwa muonekano huu inakuwa ngumu kuwatofautisha na wahalifu wenye silaha.
Nimefurahi kuona hii kitu inaitwa gorilla patrol yaani mtaa kwa mtaa nchi zote za Africa mashariki zinafanya huu mtindo ila wao wanavaa sare siku nyingine wakija watu wabaya wenye silaha itakuwa ngumu kung'amua kama hao ni walinda au wavunja sheria