Polisi: Tunachunguza sakata la Dada yake Polepole

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,398
Reaction score
14,521

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa za kutekwa na kurejeshwa kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole alidai kuwa dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

Soma, Pia: Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

“Dada huyo alifika katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa zinazohusiana na yeye kuchukuliwa na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyohiyo”, ameeleza Muliro.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.
 
ina maana hao watekaji walikurupuka kwenda kuteka bila amri ya boss wao..ila baada ya boss kutaarifiwa ndio akaamuru wamrudishe haraka..au watekaji lengo lao ni kumtisha polepole kwamba akiendelea kuleta fyoko kugusa wakubwa na kujificha mbali watadili na wanafamilia wake.! nimewaza nhe ya box
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa za kutekwa na kurejeshwa kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole alidai kuwa dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

“Dada huyo alifika katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa zinazohusiana na yeye kuchukuliwa na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyohiyo”, ameeleza Muliro.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.
Jaman tumefika huku tenaa aiseee

So bad
 
M Natacha kuweka bundle sasa maana kila nikifungua humu naona comedy za AJABU loh
 
Back
Top Bottom