Polisi Tanzania Vs Simba SC (0-1) | VPL | CCM Kirumba

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,409
2,000
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara VPL Kuendelea kupigwa leo Juni 19, 2021 ambapo Polisi Tanzania wanawakabili Mabingwa wa Nchi, Simba SC, Mnyama Mkali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jiji Mwanza.

Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania George Mketo, amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi licha ya ubora wa wapinzani wao.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi Suleiman Matola, amesema Maandalizi mazuri na wachezaji wapo tayari kufanya vizuri dhidi ya Polisi Tanzania.

Polisi Tanzania wanawakaribisha Simba SC huku wakiwa na takwinu mbaya kwani hawajawahi kupata matokeo ya ushindi mbele ya Mnyama Makali Simba SC.

Je katika mchezo wa leo Polisi Tanzania anajitetea ama kichapo kitaendelea kumuhusu? Kumbuka mchezo huu ni kuanzia saa 10:00 Jioni. Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


============

00' Kipyenga kimepulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo huu VPL.

10' Simba SC wamepata Free Kick amabayo golikipa wa Polisi amedaka bila wasiwasi huku Makame akionyeshwa Kadi ya Njano.

Mpira unachezwa zaidi eneo la katikati ya Uwanja. Kila timu inasaka ushindi ili kuweza kujiweka sawa

20' Mchezo ni mkali sana, milango bado ni migumu katika safari hii ya kusaka alama tatu muhimu |Polisi Tanzania 0-0 Simba SC.

27' Ni Free Kick kuelekea Polisi Tanzania anakwenda kupiga Miquissone

Goooooooooaaal Goooooooaaal

Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa Free Kick amabayo ilienda moja kwa moja | Polisi Tanzania 0-1 Simba SC

39' Hassan Nassor anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumchezea Madhambi Miquissone.

40' Simba SC wamewashika Polisi na kumiliki zaidi mpira huku Polisi wakijaribu kutafuta bao la kusawazisha.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa CCM Kirumba, mpira anao Yondan kwake Pato anapiga mbele, lakini anafika Wawa, kwake Onyango.

VPL, HT; Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele kwa bao moja dhidi ya Polisi Tanzania | Polisi Tanzania 0-1 Simba SC.

Kipindi cha pili kimeanza huku Polisi Tanzania wakifanya mabadiliko Ametoka Seif na ameingia Mdamu

50' Ametoka Mugalu na ameingia Kagere upande wa Simba SC huku free kick ikipigwa kuelekea Polisi Tanzania.

58' Polisi Tanzania wanapata free kick, eneo nzuri kuweza kusawazisha, Inapigwaa lakini golikipa Manula anadaka bila wasiwasi.

59' Ametoka Bwalya na ameingia Nyoni upande wa Simba SC huku Simba wakifanya mashambulizi kadhaa lengo la Polisi.

Kadi ya Njano kwa Taddeo baada ya kuchezea madhambi ni free kick kuelekea Simba SC.

75' Almanusura Polisi wapate bao kama si umahiri wa golikipa Manula anapangua hatari ile huku Kagere akikosa nafasi nzuri ya kufunga bao Simba SC, yeye na Wavu.

86' Free Kick amabayo Ikipigwa na Miquissone inatolewa na golikipa wa Polisi na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa VPL huku Polisi wakiwa hawana matumaini ya kusawazisha

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Polisi Tanzania na kuzidi kujikita kileleni msimamo huku harufu ya ubingwa kinukia.

FT, VPL | Polisi Tanzania 0-1 Simba SC.
....... Ghazwat.........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom