kimpe
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 911
- 861
wana jf naomba kuliwasilisha hili jambo ambalo linanikera sana moyon mwangu kiukweli kwan nimeshaliona zaidi ya mara tano kwa sasa. polisi ni vibaka, polisi ni wezi, polisi ni majambazi.Nitatolea mfano kwa hawa polisi wa mbeya. Ninapooona polisi ni vibaka ni pale ambapo wanakukamata huchukua ht vitu vidogo vidogo tena vidogo sana nilishangaa pale polisi alipochukua key holder (kibeba funguo) tena kina Tangazo la mtandao mmoja wa simu pale aliponikamata...... Polisi ni wezi pindi zilipotokea vurugu za machinga hapa Mbeya polisi walikuwa wakikukamata mwananchi wanakusachi na kuchukua kila kitu ulichonacho mfukoni simu, wallet n.k............. wakati wa kutoka polisi ukidai hvo vitu mkuu wao anasema fungua kesi kama unamjua huyo ofisa wakati anajua kipindi walipokuwa wanakamata walivaa mikofia yao mikubwa usoni kiasi kwamba huwez mtambua......... Polisi ni majambazi ni kawaida kusikia polisi hutumia silaha zao kuwauwa wananchi makusud kabisa na kuwa bambikia kesi kuwa walikuwa wezi mwanzoni mwezi uliopita polisi hp mbeya waliingia sehemu moja ya starehe hapa mjini Mbeya na kumuua mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo hapa Mbeya kwa madai kuwa ni jambaz wakati walimkuta katika starehe baadae taarifa zikavuja kuwa kulikuwa na ugomvi wa kimapenzi kati mmoja wa polisi na mwanafunzi huyo..... hivyo ofisa alikwenda lipa kisasi. Hali hii inatisha je na maeneo mengine hali ipo hivi...........tuungane kupinga udhalimu huuuuu.