Polisi ni wezi

kimpe

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
911
861
wana jf naomba kuliwasilisha hili jambo ambalo linanikera sana moyon mwangu kiukweli kwan nimeshaliona zaidi ya mara tano kwa sasa. polisi ni vibaka, polisi ni wezi, polisi ni majambazi.Nitatolea mfano kwa hawa polisi wa mbeya. Ninapooona polisi ni vibaka ni pale ambapo wanakukamata huchukua ht vitu vidogo vidogo tena vidogo sana nilishangaa pale polisi alipochukua key holder (kibeba funguo) tena kina Tangazo la mtandao mmoja wa simu pale aliponikamata...... Polisi ni wezi pindi zilipotokea vurugu za machinga hapa Mbeya polisi walikuwa wakikukamata mwananchi wanakusachi na kuchukua kila kitu ulichonacho mfukoni simu, wallet n.k............. wakati wa kutoka polisi ukidai hvo vitu mkuu wao anasema fungua kesi kama unamjua huyo ofisa wakati anajua kipindi walipokuwa wanakamata walivaa mikofia yao mikubwa usoni kiasi kwamba huwez mtambua......... Polisi ni majambazi ni kawaida kusikia polisi hutumia silaha zao kuwauwa wananchi makusud kabisa na kuwa bambikia kesi kuwa walikuwa wezi mwanzoni mwezi uliopita polisi hp mbeya waliingia sehemu moja ya starehe hapa mjini Mbeya na kumuua mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo hapa Mbeya kwa madai kuwa ni jambaz wakati walimkuta katika starehe baadae taarifa zikavuja kuwa kulikuwa na ugomvi wa kimapenzi kati mmoja wa polisi na mwanafunzi huyo..... hivyo ofisa alikwenda lipa kisasi. Hali hii inatisha je na maeneo mengine hali ipo hivi...........tuungane kupinga udhalimu huuuuu.
 
kaunajua kusnipe we snipe maana walishanitoka kitambo sana..

pole sana kwa maswahibu mkuu..
 
kwel polisi ni wahalifu #1,inakuwaje polisi amkamate mhalifu mfano muuza mihadarati tena kamkuta na kielelezo then anamweka rumande zaidi ya saa72 bila dhaman wala kumpeleka mahakaman mwishowe anatoa dhamana kwa pesa zaidi ya laki hlf anamwambia pablo huyo kesho njoo na laki kadhaa 2malize hapa polisi.je siku hzi jinai pia inapigwa fain polisi km trafic case?saidien wasingida wanamalizwa polisi
 
polisi ni wezi tena sana, nshatoa sana rushwa kipindi kile cha difenda za polis zenye plate number za kiraia (TZR) jamaa walikuwa kila wiki lazma waibuke skani
 
Generalisation is very dangerous.Ni kweli polisi wote hutenda mabaya?
 
polisi ni wezi tena sana, nshatoa sana rushwa kipindi kile cha difenda za polis zenye plate number za kiraia (TZR) jamaa walikuwa kila wiki lazma waibuke skani

Na wewe pia ni muhalifu...kwanini ulikuwa unatoa rushwa??? ni kwanini walikuwa wanaibukia maskani kwenu kila mara
KUMBUKA siku zote nzi hufuata uchafu/kinyesi...Polisi ni sawa na Nzi...hufuata kinyesi ndiyo maana nao huchafuka...
wale wanaohusika kusaka majambazi baadaye huzoweana na kisha nao hushiriki ujambazi,...wale wa matapeli vivyohivyo!!
Lakini hili ni tatizo kubwa zaidi kuliko kuliangalia Jeshi la Polisi pekee...Tujiulize ni kwanini mmomonyoko wa maadili unashikla kasi katika jamii yetu...?? Hawa polisi wetu hawajatokea sayari nyingine...ni watoto wetu, dada/kaka zetu...baba zetu...tatizo hili lipo mahospitalini, mahakamani, kwenye mawizara, makanisani/misikitini na michezoni...kote huko lipo tatizo kubwa la mmomonyoko wa maadili...GREAT THINKERS TUFIKIRI ZAIDI YA KULITAZAMA JESHI LA POLISI PEKEE...
 
mtoa mada uko sahihi kabisa,polisi ni watu wa kuogopwa kuliko inavyofikiriwa na wengi,walinikamata mwezi wa 12 mwaka jana wakazama mfukoni wakanichukulia elfu 70,nilipojaribu kuwakomalia waliniweka ndani wakanipa kesi,nilipogundua kesi waliyonipa ni kubwa na ngumu niliwaomba radhi wakaniachia.mpaka hii leo nawaogopa polisi ni majambazi na wauaji.
 
Kwani hujalisoma hili lililotokea ndani ya hifadhi ya Serengeti ila 40 zao zilikuwa zimefika pitia humuhumu utaukuta uzi huo kwenye jukwaa hilihili
 
Back
Top Bottom