Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,690
- 26,568
Ukifuatilia vizuri matukio mengi yanayoendelea nchini ambayo, utagundua Polisi ndiyo chanzo kikuu cha vurugu.
Kauli za viongozi wa Polisi wanapokuwa wakionya na kukataza jambo fulani kutokea, huwa unaona kabisa kwamba kama luna vurugu yoyote ile, basi vurugu hiyo ndiyo wanakuwa wanaitangaza hapo kupitia hayo maonyo yao.
Vurugu za Polisi huwa zinaandaliwa na kuratibiwa chini ya Kamandi ya Opareshini na Mafunzo ya Jeshi la Polisi. Mkuu wa Kamandi hii siku zote ni lazima awe 'Kada hasa' aliyeandaliwa. Lawama zinaweza zikatupwa kwa IGP, RPC na wengineo, ni sababu wengi hawafahamu nguvu ya Kamanda wa hii Kamandi.
Unaweza ukawa na IGP mzuri kweli, ila kaangalie atakayeongoza hii Kamandi, unaweza ukajiuliza inakuwaje akamuweka pale mtu kama yule.
Mfano katika kesi ya Tundu Lissu, watu walewale wanaop8gwa na kuumizwa na Polisi nje ya Mahakama, ndiyo haohao wanaoingia Mahakamani kusikiliza kesi, lak8n8 haikuwahi hata siku moja kusikika wak8wa wamefanya vurugu Mahakamani, haikuwahi kuonekana au kusikika askari Magereza wakiwatumia risasi, marungu au mabomu ya machozi kutuliza vurugu ndani ya Mahakama na viunga vyake. Mambo hayo huwa tunayaona barabarani wakati watu wakielekea mahakamani.
Kama watanzania wangekuwa na angalau robo ya vurugu ambazo huwa wanatuhumiwa nazo kwenye siasa, basi viwanja vya mipira vingezuiwa watu kuingia kuangalia mechi.
Kwa Tanzania, Polisi ndiyo hutumika kuamua nani apewe sifa ya uvunj8fu wa amani.
Ushauri wangu kwa Chama Cha Mapinduzi ni kwamba, acheni kulitumikisha Jeshi la Polisi katika ukandamizaji, haya mambo msiyaangalie kwa historia, yaangalieni kwa hali ya sasa, tulipofika yanaenda kupasua chombo, matokeo yake yaliyomo yamwagike...mmekimbia sana na sasa mpo ukingoni mwa sakafu. Jitahidini muwe kama yule Wakili 'Mwelevu', Injili ya Luka 10:25-37.