Polisi na usalama wa raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na usalama wa raia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Nov 10, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160


  [​IMG]
  Polisi nchini Marekani wiki hii akiwa kazini kutuliza mtafaruku
  uliotokea chuo cha Penn State huko Penslivania, USA


  [​IMG]
  Polisi wa Tanzania akiwa katika kujiandaa kusambaratisha maandamano Jijini Dar leo
  akiwa na silaha mkononi tayari kana kwamba anawinda jambazi lenye silaha mkononi
  tayari kuwashambulia wananchi ambao ana dhamana ya kuwalinda.  Katika pichi hizi mbili tunaweza kuona tofauti kati ya hawa polisi na wote wako katika ulinzi, lakini yule wa Marekani alikuwa katika kutuliza ghasia ambazo zilileta madhara, lakini hakutumia nguvu na vitisho vya silaha kama anavyoonekana askari wa pili wa kikosi cha polisi Tanzania.

  Polisi wa Marekani ni wa jamii inayowazunguka na wanachi wana maamuzi na kuinyooshea kidole polisi muda wo wote inapofanya kazi kinyume cha sheria na kwa mantiki hiyo wako makini sana. Kosa lo lote likitokea kuuawa mtu au kujeruhiwa ni kwa hakika polisi huwa hakuwa na jinsi nyingine ya kufanya ila kutetea uhai wake na ni jambo nadra mno kutokea. Ndio maana unamwona polisi huyo wa marekani licha ya kuwa na silaha hajaishika vinginevyo ingekuwa tishio na kukosa ushirikiano na raia wema.

  Askari wa Tanzania yuko vitani licha ya kutokuwepo aina ye yote ya hatari, ni vita tu, hakuna akili na hakuna dalili za kuonyesha polisi kuwa na taaluma ya kazi zao. Inaonyesha wamafunzwa kutisha wananchi kwa kwa utaratibu huu si rahisi kupata ushirikiano ambao unaweza kuwasaidia katika kazi zao. Na kwa mfumo wa polisi Tanzania, wananchi hawana haki ya kuwanyooshea kidole ukiukwaji wa taratibu na sheria juu ya utendaji wao. Wako juu ya sheria.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Hiki ndicho kikosi cha polisi Tanzania kikiwa vitani na vitisho vya silaha hatari kwa wananchi badala ya kuwalinda raia hao.
   
Loading...