Polisi na tahadhari za ajari barabarani

Polisi na tahadhari za ajari barabarani

Olmo

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2026
Posts
1,048
Reaction score
1,911
Wakuu ndugu zangu polisi najua na nina uhakika kabisa nyinyi ni watanganyika wenzetu tena hata majina mnatumia kama ya kwetu ya kina Mongera kama mimi hapa richa ya kuijita olmo lakini kiukoo ni mongera! Najiuliza kwanini mnachukiwa ivi jamani ? Wengine tunaenda mbali tunasema hii ni kwa sababu nyinyi ni mali ya ccm! Lakini ukiangalia tena kama vitu vingine havihusiani kabisa na mabwana zenu! Ok any way twende kwenye point!
Leo nimeshudia mkasa mmoja hapa makete mwakavutwa. Madogo wa miaka kama sita nane hivi wamepakizana kwenye baiskeli yao wakiifuatilia land cruser kwa nyuma, ikipunguza mwendo na wao wanapunguza ikiongeza wanaongeza! Akashuka polisi mmoja akawahoji maswali mawili matatu madogo wakaanza kulia! Hapo jamaa akaanza kufungua baiskeli ikaitoa upepo na kuwaacha madogo wanatembea kwa miguu. Hapo hajui wanaelekea wapi na wanatoka wapi na umbali wanaoenda na wanakotoka! Maana mahojiano yao nilisikia hakuwauliza habari hizo!
Sasa jamani tuulizane kulikuwa na sababu ya kutoa upepo baiskeli? hawa watoto utawaaminisha vipi kuwa polisi ni mwema na anarinda raia?
Karibu sana!
 
Back
Top Bottom