Polisi Msijisahau Tanzania ni yenu pia

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Ndugu zetu polisi wanatabia ya kuwanyanyasa wananchi, hata sasa hivi watu wanapokufa muhimbili, wao wanazuia maandamano. Sijui ni kwa maanufaa ya nani wakati ni ndugu zao pia wanaokufa mahospitalini. Kwanza maisha mnayoishi ni ya kusikitisha. Fikirieni Tanzania mtakayowaachia watoto wenu. Msikubali kutumika kwa kuwaua ndugu zenu wanatafuta haki kwa wote. Hao viongozi ni wa muda tu, Tanzania itabaki pale pale
Muigeni Mama Hellen Kijo- Bisimba aliyewaonyesheeni Njia kwa kuwa tayari kufa kwa ajili ya nchi yake. Badilikeni, siku yenu ya kufa ikifika hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM atakaye kuja kwenye mazishi yenu. Hacheni mambo ya unyanyasaji, Wakumbukeni wana libya, Misri pamoja na Tunisia.......
5.jpg

10.jpg
 
Kati ya watu ambao nawashangaa sana ni hawa Polisi, wana maisha duni mnoo lkn kila kukicha hawaachi kumtumikia huyu kafir anayeitwa serikali ya CCM
 
Labda wameridhika na maisha yao ya kuishi kwenye nyumba za bati full suti, kuanzia chini mpaka juu,na vimishahara vidogo.
 
Hao mnawaonea tu! Tatizo ni system nzima ya utawala! Wao wanawajibika kwa serikali iliopo madarakani,na wamekula kiapo cha utii kwa amiri jeshi na mkuu wa nchi. Wanatekeleza wajibu wao,kwa maelekezo ya watawala! Eleweni.
 
Ujumbe mzuri kwa askari wetu. Maisha yao ni duni, wanaishi kwa kuwadhurumu raia wema. Maisha ya waTZ wote wakiwemo polisi na koo zao yanazidi kuwa duni. Ni wakati muafaka kwa polisi wetu kusimama imara kukataa amri za kikandamizaji wapewazo na viongozi wao. Polisi wasipobadilika mwisho wao utakuwa mbaya sana.
 
yaani serikali inawaweka kwenye nyumba za bati ambazo naamini hata mabanda yetu ya kuku yana unafuu na bado wamekaa kimya????
 
Hao mnawaonea tu! Tatizo ni system nzima ya utawala! Wao wanawajibika kwa serikali iliopo madarakani,na wamekula kiapo cha utii kwa amiri jeshi na mkuu wa nchi. Wanatekeleza wajibu wao,kwa maelekezo ya watawala! Eleweni.
Umenena Mkuu...tunahitaji Great Thinkers kama wewe...wengine humu wanayaona mambo kijuujuu...Polisi siyo
ma-dr hawawezi kugoma...maana kiapo chao kinawakataza...endapo wakigoma madhara yatakuwa makubwa
kupita maelezo...huu wa ma-dr ni cha mtoto...tusilaumu tulipoangukia bali tulipojikwaa...
 
HAWA POLISI MNAWAONEA BURE, WANAVOFANYA NDIVYO MAADILI YA JESHI LETU YANAWATAKA KUFANYA, MFUMO WA JESHI LETU TULIORITHI KUTOKA KWA WAKOLONI NDIO UNAHARIBU MUONEKANO WA POLISI, siku zote wamefundishwa kutii oda bila kuhoji, na kijeshi aliye kuzidi cheo ndie mwenye akili na kila kitu kinafuata trend hiyo, na hakuna kazi ngumu km inayodil na binadamu maana kila kinachomgusa bnadamu huwa kitamu ama kichungu. TATIZO NI VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI WANAOTOA MAAGIZO KUJA CHINI AMBAYO HAYAWEZI KUHOJIWA NA HAWA POLISI, bt ipo siku haya yatabadilka.
 
kwanza unapoandika kuhusu polisi ndani JF kweli kuna polisi anasoma humu?kwa sababu mtu hata kama amestarabika vipi akiingia upolisi tu kwanza anaaminin yupo juu ya sheria,hivyo humpelekea kuwa mjinga kabisa,yaani polisi ni wanafiki wanajifanya matatizo ya nchi hayahusu ndiyo maana wanazidi kubabuka kesi za bangi,ndiyo wanaouwa taifa hili ipo siku watalipa tu
 
Umenena Mkuu...tunahitaji Great Thinkers kama wewe...wengine humu wanayaona mambo kijuujuu...Polisi si
ma-dr hawawezi kugoma...maana kiapo chao kinawakataza...endapo wakigoma madhara yatakuwa makubwa
kupita maelezo...huu wa ma-dr ni cha mtoto...tusilaumu tulipoangukia bali tulipojikwaa...

kwa hiyo ma dr kiapo chao kinawaruhusu kugoma? wakati mwingine inafumika kitu inaitwa common sense sio kola kitu kukariri mazee.
 
Back
Top Bottom