Polisi mbaroni kwa mauaji ya raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi mbaroni kwa mauaji ya raia

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,204
  Likes Received: 3,996
  Trophy Points: 280
  Askari polisi wa Kituo cha Negezi wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga, Koplo Gidman Kanyinuzi, anashikiliwa na jeshi hilo kwa madai ya kumuua raia, wakati akishiriki ulinzi shirikishi unaojulikana kama polisi jamii.
  Inadaiwa kuwa siku ya tukio, Koplo Kanyinuzi alifyatua risasi iliyompiga Aziz Abraham (40) na kumsababishia kifo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Daud Siasi, alisema Koplo Kanyinuzi, anatuhumiwa kutenda kosa hilo Juni 2, mwaka huu, saa 7:00 usiku, katika kijiji cha Mawemawili, kando kando ya barabara ya inayotoka Kishapu kwenda Mhunze. Kamanda Siasi alisema awali wakazi wa eneo hilo waliitaarifu polisi kuhusu kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na ndipo askari polisi akiwemo Koplo Kanyinuzi, walipokwenda eneo hilo.
  Alisema polisi hao walipofika kijijini hapo, walipata ushirikiano mzuri kutoka kwa raia akiwemo Aziz, hivyo kurahisisha kazi ya kuwatafuta majambazi hao. Hata hivyo, Kamanda Siasi alisema wakati wakishirikiana kutafuta majambazi hao, Aziz (marehemu) aliyekuwa ameshika tochi, alikwenda eneo la mbali kutoka walipokuwa wengine.
  Alisema wakati Aziz akirejea kuungana na wenzake, Koplo Kanyinuzi anadaiwa kumfyatulia risasi, akidhani kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa wanatafutwa.
  “Kutokana na tukio hilo, askari huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ingawa inaonyesha kuwa tukio hilo halikuwa la kukusudia,” alisema.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...