Polisi: Mabasi kutoka Dar kwenda Kagera, Kigoma, Katavi marufuku kutembea Usiku saa 24

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Liberatus Sabas amesema mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Kagera, Kigoma, Katavi hayataruhusiwa kutembea saa 24 kutokana na sababu za kiusalama.

Kamishna Sabas amesema zuio hilo litahusu pia mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea wilaya mbalimbali za mkoani Tabora ambayo yatalazimika kusimama Tabora Mjini na baadaye kuendelea na safari wilayani.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 2, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa polisi, hali ya usalama.

Amesema mabasi yanayotoka mikoa ya Kagera, Katavi, Kigoma kwenda Dar es Salaam yataruhusiwa kutembea saa 24 kama kawaida kutokana na eneo la Morogoro na Dar es Salaam kuwa salama wakati wote.

"Mabasi haya yalikuwa yakitoka kwenye mikoa hiyo yalikuwa yanalala Morogoro, lakini kutokana na hali nzuri ya kiusalama yataendelea na safari hadi Dar es Salaam," amesema Kamishna Sabas.

Amesema mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa hiyo yatalazimika kulala wilayani Kahama kisha kuendelea na safari.
 
Aisee! Kwa hiyo interijensia ya polisi hadi sasa imeshindwa kuwabaini hao wahatarisha usalama!?
 
Kukurupuka kwa kila jambo
Mara ruksa mara marufuku
Mnatusumbua
Tuliwaambia mkaona hatujui kitu
Ujambazi utashamiri kwa hizi safari za ucku
Naona unawahi sana lawama na kujihakikishia ubingwa wa kukosoa.
 
Ujinga mwingine huu. Kwa nini wasipange mida tofauti ya safari? Kwani lazima kuanza safari 1200 asubuhi na gari kulala Kahama? Kwa nini mabasi yasitoke DSM saa mbili usiku kukikucha wawe wanakaribia Singida waingie Kigoma au Bukoba jioni?
 
Ujinga mwingine huu. Kwa nini wasipange mida tofauti ya safari? Kwani lazima kuanza safari 1200 asubuhi na gari kulala Kahama? Kwa nini mabasi yasitoke DSM saa mbili usiku kukikucha wawe wanakaribia Singida waingie Kigoma au Bukoba jioni?
Nakumbuka miaaka ya nyuma mabasi yalikuwa yanatoka Dodoma saa 2 usiku yanaingia Dar saa 12 asubuhi unaenda zako kazini.
 
Kwa hilo tamko halina makosa maana mikoa hiyo ni hatari sana ila Lugola sijui alilala vibaya
 
Back
Top Bottom