Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Jamani naomba mnisaidie kupata uelewa wa jambo hili.
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikishuhudia askari polisi wengi wakimiliki magari ya bei mbaya na si hivyo tu bali wamekuwa wakiyatumia kazini (yaani wakati wafanyapo majukumu ya kiofisi) kama vile ni magari ya kazi.
Nimeshuhudia matrafiki wakiendesha magari yao binafsi kwenda porini kutegeshea magari, na wale wengine wakienda na magari yao kukamata magendo na kadhalika.
Naomba nieleweshwe hii imekaaje? ni ruksa kisheria???? Je ka si ruksa mbona wanayatumia wakati wakubwa wao wakifahamu??
NEW NOEL Sijui kama umesoma vizuri hoja yangu. Najua kwamba wanamiliki magari ya bei mbaya isivyo halali wala hilo halina ubishi hata ungekuja na utetezi upi!! Lakini hoja kuu niliyokuwa nayo si kuyatumia kwenda nayo ofisini, bali ni kuyatumia kama magari ya ofisi kwa kwenda nayo doria n.k. Hapa ndipo nilipotaka mwongozo.Kwanza sidhani kama kumiliki gari ya thamani kubwa ni dhambi au ni kosa,suala kubwa ni je ulilipata vp? Labda hapo unaposema wanatumia kazini ninashindwa kuelewa. Je wanatumia kuendea ofisini? au wanatumia kukamata na kubabea wahalifu?
NEW NOEL Sijui kama umesoma vizuri hoja yangu. Najua kwamba wanamiliki magari ya bei mbaya isivyo halali wala hilo halina ubishi hata ungekuja na utetezi upi!! Lakini hoja kuu niliyokuwa nayo si kuyatumia kwenda nayo ofisini, bali ni kuyatumia kama magari ya ofisi kwa kwenda nayo doria n.k. Hapa ndipo nilipotaka mwongozo.
Suala la waliyapata vipi wote tunaelewa kuwa nchi hii kila mtu anamiliki kitu ambacho anadai sio kosa kuwa nacho ingawa hawezi kukuambia kama kakipata kihalali. Na hapa ndipo tatizo la ufisadi na wizi ulipoanzia kushamiri. Tuache hoja hii kwanza turudi kwenye hoja ya msingi! Je kuyatumia kama magari ya kazi hii imekaa vipi?
Hii ya Magari Binafsi ni hatarii...mi binafsi ilishwah nikuta ile njia ya Sea cliff sa nane usiku iv.....nilikuwa natembea kama 20km/hr ..nikakunja kushoto kama naenda Tanesco ..ghafra Gx100 ya maroon ikani block kwa mbele...nikajuaa doo nshaibiwa Gari ...ndio kushuka wakashuka askari FFU wa 3 na mmoja akiwa na bunduki (bila shaka ni walinzi nyumba za waheshimiwa maeneo yale)...
wakaanza kuniambia kwa nini natembea mwendo ule na eneo lile ni hatari,mara washa taa za ndani ya tuwaone,mara fungua iyo hash tray>>nkawaambia kwa iyo naonekana mi mvuta bange ama nimekosa sehemu ya kupigwa BJ hadi nipigwe on the move,Hakika hawakuwa na la maana la kuniuliza washazoea kuwatisha watoto wakihindi>> ni upuuzi mtupu sikusita kuweka gear D na kupotea zangu
Hiyo ni dalili kwamba nchi HAITAWALIKI na kila mtu na lwake!!