Polisi kutumia magari yao binafsi katika kufanya kazi hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kutumia magari yao binafsi katika kufanya kazi hii imekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, Oct 11, 2012.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jamani naomba mnisaidie kupata uelewa wa jambo hili.
  Kwa siku za karibuni nimekuwa nikishuhudia askari polisi wengi wakimiliki magari ya bei mbaya na si hivyo tu bali wamekuwa wakiyatumia kazini (yaani wakati wafanyapo majukumu ya kiofisi) kama vile ni magari ya kazi.
  Nimeshuhudia matrafiki wakiendesha magari yao binafsi kwenda porini kutegeshea magari, na wale wengine wakienda na magari yao kukamata magendo na kadhalika.
  Naomba nieleweshwe hii imekaaje? ni ruksa kisheria???? Je ka si ruksa mbona wanayatumia wakati wakubwa wao wakifahamu??
   
 2. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo magari ya kifahari Hawa jamaa kwanza tujuwe wameyapata kwa njia ya kuwazulumu wafanyabishara hapa mjini, kila kona unayopita sasa wamefanya Ndio kazi kubwa kwao lya kutafuta magendo, Leo hii katika pita pita zangu nimewaona mtaa wa kongo walikua 5 wawili walikua wamevaa uniform za ffu na silaha na 3 kikawaida wamekikuta kisuzuk kinashusha misumar tena kipo dukani Kabisa wakadai risit, wakapewa, wakadai risit ya deliver wakapewa, baadae wameliza huu mzigo una thamani ya sh.ngapi? Wakaambiwa angalieni risit, kilichoendelea yakazuka mabishano hapa ya kulipia kodi je mimi napenda kuuliza Hawa Askari kazi zao ni zipi hash ncni hii,na wameikusudia nini, wamewakusudia nini alalahoi, wazalendo,Ivi udhalilishaji wa Askari Hawa utakwisha lini? Mtanzania ndani ya nchi yako huna Uhuru hata wakufanya Mimi ningependa kujua
   
 3. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Kwanza sidhani kama kumiliki gari ya thamani kubwa ni dhambi au ni kosa,suala kubwa ni je ulilipata vp? Labda hapo unaposema wanatumia kazini ninashindwa kuelewa. Je wanatumia kuendea ofisini? au wanatumia kukamata na kubabea wahalifu?
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni dalili kwamba nchi HAITAWALIKI na kila mtu na lwake!!
   
 5. m

  mpunumpunyenye Senior Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  wewe ulikuwa hujui kuwa hii ni miradi tena ni mikubwa kuliko migodi, kama unapata zaidi ya laki mbili kwa siku kwa nini nisiende na prado??
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hayo magari ya bei mbaya ni Vogue au Aston Martin,kama Toyota bhaaaasiiii.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  NEW NOEL Sijui kama umesoma vizuri hoja yangu. Najua kwamba wanamiliki magari ya bei mbaya isivyo halali wala hilo halina ubishi hata ungekuja na utetezi upi!! Lakini hoja kuu niliyokuwa nayo si kuyatumia kwenda nayo ofisini, bali ni kuyatumia kama magari ya ofisi kwa kwenda nayo doria n.k. Hapa ndipo nilipotaka mwongozo.
  Suala la waliyapata vipi wote tunaelewa kuwa nchi hii kila mtu anamiliki kitu ambacho anadai sio kosa kuwa nacho ingawa hawezi kukuambia kama kakipata kihalali. Na hapa ndipo tatizo la ufisadi na wizi ulipoanzia kushamiri. Tuache hoja hii kwanza turudi kwenye hoja ya msingi! Je kuyatumia kama magari ya kazi hii imekaa vipi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Naona wamekuwa wabunifu "in themselves" maana ule wimbo wa "hatuna gari,hatuna mafuta" kwenye defender za polisi umekuwa kawaida.
   
 9. nyaunyau

  nyaunyau Senior Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  askari wetu siku hizi wanapewa mikopo na mabenki mbalimbali Nchini,ni dhambi kujadili mambo ambayo hayana ushahidi.wakati mwingine tusiwatwishe mizigo ya lawama bila sababu za msingi,ukiona hali ni shwari wapo kazini.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,383
  Likes Received: 22,259
  Trophy Points: 280
  Jiulize, ni nani anayeweka mafuta ili kulifikisha gari kwenye shughuli za kufukuza wezi??
  Jibu, ni wezi ndio wanaweka hela kwenye magari ya polisi.
  Mwizi akishindwa kuweka mafuta anafunguliwa kesi ya mauaji.
   
 11. M

  Mundu JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Askari huwa tunawapa sisi hela wanapotukamata kwa makosa mbalimbali (hususan wale wa usalama njiani).

  Sasa wakaona isiwe taabu...nao wakaamua kuwekeza kwenye mikoko na piki piki.

  Hakuna ubaya kufika kunako kazi na mausafiri yao...Ila kungekuwa na utendaji wa uwajibikaji...wangewajibika kueleza wamepata kwa njia gani vitendea kazi hivi. Labda wangepunguza kidogo makosa wanaayotubambikia. Mathalan mie walinikuta sinanhatia yeyote wakaniuliza ..."Arooooo, inaonekana hujajiandikisha kuhesabiwa wewe...paki pembeni..."
   
 12. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hii ya Magari Binafsi ni hatarii...mi binafsi ilishwah nikuta ile njia ya Sea cliff sa nane usiku iv.....nilikuwa natembea kama 20km/hr ..nikakunja kushoto kama naenda Tanesco ..ghafra Gx100 ya maroon ikani block kwa mbele...nikajuaa doo nshaibiwa Gari ...ndio kushuka wakashuka askari FFU wa 3 na mmoja akiwa na bunduki (bila shaka ni walinzi nyumba za waheshimiwa maeneo yale)...
  wakaanza kuniambia kwa nini natembea mwendo ule na eneo lile ni hatari,mara washa taa za ndani ya tuwaone,mara fungua iyo hash tray>>nkawaambia kwa iyo naonekana mi mvuta bange ama nimekosa sehemu ya kupigwa BJ hadi nipigwe on the move,Hakika hawakuwa na la maana la kuniuliza washazoea kuwatisha watoto wakihindi>> ni upuuzi mtupu sikusita kuweka gear D na kupotea zangu
   
 13. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  unajua gari la bei mbaya wewe ? kamuulize david mosha maana ya gari la bei mbaya
  anyway gari la bei mbaya kama hilo hapo

  lamborghini.jpg
   
 14. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  polisi ni wezi tu,ukiwafuatilia mambo yao!unaweza fikili nchi haina mwenyewe,na wanawaonea sana raia! enzi za mwlm,polisi hata akinywa bia kuna watu walikua wana hesabu vizibo,na mwisho wa mwezi unaulizwa "eeeh mwenzetu umekunywa bia tisa 9,mshahara wako tunaujua umepata wapi pesa ya bia" usipotoa majibu ya kueleweka unatupwa ndani, leo hii POLISI NI WIZI MTUPU! huku kwetu wanaongoza kwa kumiliki daladala!
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa unafikiri wasipotumia magari yao kutafuta hela barabarani au kukamata magendo wataishije? hela ya mafuta ya hayo magari watayatoa wapi? inabidi waingie nayo mitaani hivo hivo
   
 16. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yaani tunapojadili hapa ni kama hatujui maaskari wa Tanzania. Hawahawa ndiyo waliomlipua Mwangosi kwa amri ya Kamuhanda. Hawahawa ndiyo walioua wale wafanyabiashara ma Ulanga. Hawahawa ndiyo waliomwua Munishi kule bomang'ombe na kutangaza kuwa wameua jambazi. Hawahawa ndiyo waliomtesa Dr. Ulimboka. Hawahawa ndiyo waliorusha kitu kizito kilichomwua kijana maskini Ally. Je kumiliki magari ya kifahari, kuwabambikizia watu makesi na kuwatupa rumande, kuwanyanyapaa watu wasio na hatia ni kitu kwao? Tanzania haina mwelekeo kuanzia raisi, maMPs, na wengine. Je askari atapata wapi uadilifu na uaminifu kama hajui hata wajibu wake? Askari anasimama barabarani kuomba rushwa, kuwaachia wahamiaji haramu waingie na kutoka wanavyota kisha tu rushwa. Ataachaje kupoteza mwelekeo?
  Hatuna nchi kwa sasa. Kilichobaki ni himaya ya JK na shemeji Mwema wakifanya vitu vyao. Sisi tuvumilie na kuomba Mungu ili ifikapo 2015 tupigane mapanga kama wakenya. Tukishauana karibu nusu yetu wale watakaobaki wataketi chini na kujichagulia viongozi wenye maadili. Then, nchi itatawalika na askari watashika angalau adabu na kutimiza wajibu wao ambao ni kulinda 'raia na mali zao"!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sio wewe tu. Mie alinisimamisha traffic kule mwanza akaniuliza kila kitu kipo. Akakagua gari kila kitu murua maana ni jipya, akaishia kuniambia mbona gari halina maji ya kunywa? ahahahahaaaa nikamuangalia kwa mshangao sana. Kisha akaniambia unajua gari yako imefanana kabisa na ya kwangu kisha kaniambia haya bwana unaweza kwenda maana aliona sina deal.......... kumbe inawakuta wengi sio? Nikuomba wasiishie kukupiga risasi kwa sababu your useless to them kisha wakasema alikuwa ni jambazi huku wakikupandikizia siraha!
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Matokeo ya rushwa hayooo!
   
 19. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Magwanda bana! askari walipokuwa wanalala ktk mabanda na maisha duni,mliwaita majina mengi ya ajabu,mara askari njaa,hawana ellimu! n.k,sasa wakiishi vema maneno! yani hamna jema kabisaa!
   
 20. S

  SASTONI Member

  #20
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mkuu kwa bahati mbaya unapenda ujibiwe jibu ulilo lipanga ukweli ni kwamba hakuna sheria inayozuia mtu yeyote kujitolea
   
Loading...