Polisi kutoa maelezo ya kukamatwa kwa Tito Magoti wa LHRC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesho Jumatatu Desemba 23, 2019 watatoa taarifa za Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti.

Magoti alikamatwa na polisi Ijumaa Desemba 20 eneo la Mwenge, Dar es Salaam tukio lililozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ametekwa.

Hata hivyo, siku hiyo jioni polisi walieleza kuwa Magoti (26) hajatekwa na wanamshikilia pamoja na wenzake licha ya kutoweka wazi wapo kituo gani cha polisi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Desemba 22, 2019 Mambosasa amesema, “kituo alipo ni cha polisi hatuonyeshi mtu yoyote, taarifa itatolewa kesho.”
 
Hatimae wasiojulikana wameamua kwa dhati ili wajulikane

Kwa hiyo yale maswali tuliyokuwa tunajiuliza Watanzania naona yanaanza kujibiwa
 
Korea... kaskazini...ni nchi yenye maendeleo sana...
Wananchi wake na viongozi wanafanya kazi kwa pamoja na ushirikiano mkubwa kama wadudu chungu!
Tunaelekea huko ili ... hatimaye tuwe kama wenzetu hao waliopata maendeleo kabla yetu!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom