Polisi kushiriki ualifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kushiriki ualifu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Daudi Mchambuzi, Feb 26, 2012.

 1. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,789
  Likes Received: 36,800
  Trophy Points: 280
  Hili ni moja kati ya matukio 1000 yanayofanywa na askari wa jeshi la polisi.
  Iko hivi, kuna jamaa nilipata kusoma naye kitambo na sasa ni polisi kitengo cha FFU.
  Juzi polisi huyu kaniambia kuwa, huwa anakodisha silaha yake kwa majambazi wakati wa lindo usiku (hasa akipangwa bank) na asubuhi hurejeshewa silaha yake na kitita cha laki mbili mpaka tatu kutoka kwa majambazi hayo.
  Hakuishia hapo, polisi huyo alizidi kunidokeza kuwa wanapoishiwa na pesa za matumizi huwa wanachukua silaha wakati wa lindo mida ya jioni na kuvaa makoti makubwa kama raia na kuvamia maduka makubwa ya biashara za jumla wakati wa kufunga na kutishia kwa silaha hizo za jamuhuri na kupora fedha kutoka ktk duka husika.

  MY TAKE:
  Polisi wetu wakiwa huko mafunzoni hufundishwa utii wa uwoga na wanapewa treatment mbaya sana kiasi cha kuwafanya kuwa na roho mbaya na ya kikatili badala ya kuwa waaminifu na watii wa sheria.
  Mafunzo ya ukatili wanayofundishwa askari wetu yanawafanya walinzi hawa wa usalama wa raia na mali zao kukengeuka na kuwa majambazi kwa kujaribu kujikwamua kwenye umaskini kwa kutumia ukatili uleule waliofunzwa huko CCP.
  Swala la mafunzo ya askari na malipo yao litazamwe upya.
  Askari anayelipwa laki mbili unusu kwa kazi ya kulinda bank yenye billions of money lazima awe mwizi.
  Kwa kifupi polisi ndo wezi hapa tanzania.
   
 2. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  naunga mkono mkuu. me pia kuna jamaa yangu mmoja nilisoma naye a level tabora kwa bahati mbaya akafukuzwa kwa uvutaji wa sigara na bangi. baada ya hapo alijiunga na jeshi la polisi,nikiwa chuo dar nilikutana naye akiwa cid wa kwenye ma tzr. duuuh,huyu jamaa ni soo kwani story alizonipigia ni hatari sana. wanaua raia na kuwanyang'anya pesa kisha wanasema ni jambazi,wanakodisha silaha ile mbaya,wanasindikiza mizigo ya wizi kwa kutumia defenders zao,wanakamata madawa ya kulevya then wanayauza tena kwa wauzaji wengine,wanawajua vizuri sana majambazi na wauza madawa na ndio washirika wao wakubwa! askari wa bongo ni kama askari wa kwenye movie za kihindi miaka ile,mchana askari lakini usiku jambazi.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Haya yote ni kwa sababu ya serikali ya jk legelege.

  Lawama yote ni yao yote!
  Watatumaliza hawa majambazi police.
   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kabisa, mi nimeshashuhudia matukio matatu ya wizi wa magari na kwa asilimia kubwa polisi ndio wanahusika na wizi huo moja kwa moja.
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,531
  Likes Received: 10,444
  Trophy Points: 280
  ni kweli mkuu kakaangu siku moja usiku alivamiwa na majambazi wakampora vitu kadhaa vya thaman. Akaripoti polisi lakini kila akipojaribu kufatilia upelelezi polis walimjibu bado.siku ya tatu ndipo askari mmoja bila aibu akamwambi atoe posho vitu vinaweza kupatikana.ikabidi atoe lakini huku akiwa amekata tamaa cha kushangaza asubui wakampigia sim na kumwambia aje atambue vitu vyake kufika pale akakuta ndo vilevile japo vingine walikua wameshaanza kuviuza lakini mwizi hakumuona hata mmoja. Na inasamekana wezi wote polis wanawafaham awe mdokoz mwizi au jambazi kwa hiyo wizi ukifanyika wenyewe hawahangaiki ni kunyosha kwenye kundi ambalo watahis limehusika au wanawapigia sim .kweli tz ni zaidi ya ujuavyo
   
Loading...