Polisi kijana alivyoniharibia usiku wangu jana

Makuzamkumbo

JF-Expert Member
Mar 8, 2023
501
512
Salaam,

Moja kwa moja kwenye kisa hiki cha kipuuzi, kwa kifupi tu mimi sio muajiriwa na sina mpango huo. Nafanya shughuli zangu binafsi ambazo bila kutarajia nimejikuta nikipata connection na watu wazito kiasi na kuzunguka karibia nusu ya nchi yetu hii pendwa ya maziwa na asali

Yapata wiki mbili sasa niko mkoa fulani hivi kishughuli na kulingana na kazi yangu hii muda mwingi nipo mzigoni isipokua jumapili tu, hivyo siku ya jumamosi ndio siku yangu ya kupata mambo yetu haya na kama kawaida jana nilikuwa sehemu napata huku naperuzi hapa jamvini kwa raha zangu

Huwa nagonga hata kama ni mpaka saa 10 alfajiri kwa kua jumapili sifanyi kazi na ninapenda sehemu yenye night club sio hizi bar za kawaida ikifika saa 6 wanafunga.

Basi imefika muda wa saa 7 hivi naona dogo kanijia mzima mzima kibabe " brother nina mazungumzo na wewe njoo hapa" anamaanisha ninyanyuke nilipokaa nimfuate.

Nikamwambia bwanamdogo huwezi kuniita kibabe hivyo vp unanidai? Kapaniki "Bro unaongea sana eeh, ngoja nikuonyeshe kazi" kanifuata mm nikanyanyuka tayari kwa lolote akaniambia unanijua mimi? Mimi ni askari na kuanzia sasa upo chini ya ulinzi" nikahoji uaskari wako unanihusu nini kwani mimi ni mhalifu? Kazidi kupandisha "Unabishana na mimi" nikamwambia siwezi kubishana na wewe nakuuliza maana ni ustaarabu gani unatumia kunivamia kana kwamba mm ni jambazi?

Wakati tunazozana meneja wa bar kaja kauliza kulikoni askari anajibu eti huyu bwana nimemkamata anatafuna gomba halafu ananiletea jeuri muhudumu aliyekua ananihudumia akapinga mara kanaswa kibao dah! Askari anataka kunikamata eti twende kituoni nikamwambia meneja nitaenda ila sitaki huyo bwana anisogelee, meneja akaafiki na akamwambia wewe nenda huyu nakuja nae, ila askari kakataa kata kata anataka anikusanye.

Akili ikacheza haraka nikaona nikizubaa tu anaweza kuniwekea hivyo vitu so nikatoa simu chap nikampigia boss wangu nikamweleza kaniambia subiri hapohapo, baada ya kama dk 5 kaja mtu hata simjui na kutokana na huo mzozo akabaini ndio wenyewe kauliza bwana mkumbo ni yupi hapo nikamwambia ni mimi akaniuliza kulikoni askari akataka kudakia kapigwa stop nikaeleza kila kitu.

Basi huyo bwana ambaye baadaye nikaja kufahamu ni afisa wa kitengo fulani cha halmashauri ya manispaa akapiga simu baada ya salaam kampa bwana afande simu baada ya afande kuongea na ile simu kaanza kunyongonyea naskia anajitetea niko tu naangalia usalama mkuu hamna tatizo mara boss kanipigia nikamweleza kinachoendelea mpaka muda huo

Basi bwana baada ya mazungumzo dogo kawa mpole na samahani nyingi mpaka nikamsikia huruma tena nikamwambia afisa huyu mm sina shida nae aondoke zake tu akaruhusiwa mara mhudumu aliyechapwa kibao naye kalianzisha ila meneja wake akaweka mambo sawa na mzozo ukaisha.

Mimi toka kuzaliwa mpaka umri huu 35+ sijawahi hata kufika mlango wa kituo cha polisi ila jana ilikua nibambikiwe kesi jamani dah nyie polisi baadhi yenu mungu anawaona
 
Kwahiyo Uchawa ulikusaidia....
Hehehe.

Binafsi huwa sibishani nao hao jamaa natii sheria bila Shuruti nikifika Huko kituoni huwa nawapa angalizo tu.

Kuna siku walinisweka ndani nikakubali wakati wa kutoka nikapiga simu (Kwa Mutu ya Kazi) nikaongea nae huku nalia kinafkinafki na mambo mengine ya uongo nikaongezea. Dk 10 si nyingi wakaja (Wanaume).. Yaliyoendelea sijui ila na uhakika walikiona chamoto.

Nikarudi home (Mutu ya kazi) akaja kunipa pole mwanae wanamlaza kwenye kunguni kweli?!!
 
tatizo unakaabaa kinyonge wahuni wanakulia timing wanaona helahii hapa

wanaamua kukupelekesha watakavyo.acha uzoba ukiingia sehemu vimba chukua hata mademu wawili watatu vimba nao wanyweshe

wahuni watakaa mbali nawewe.sasa lafkyangu unaenda sehem kukesha unafika unakaa mwenyewe?🤣🤣🤣🤣
lazima watu wakuchalenji tuu kivyovyote.

Mana sehem zastareh na ugonvi damdam
 
Kwahiyo Uchawa ulikusaidia....
Hehehe.

Binafsi huwa sibishani nao hao jamaa natii sheria bila Shuruti nikifika Huko kituoni huwa nawapa angalizo tu...
Hahahahaha ila mm sio chawa nitake radhi nafanya kazi halali na nina connection za kutosha tu, Kwa mfano nikiwa hapa nimeshapata dili so nikimaliza shughuli ya huyu mnene hapa Moja Kwa Moja naelekea Songwe baada ya pasaka
 
Mimi ningekwisha mtoa meno huyo polisi

Hua nina hasira sna za karibu mtu akitaka tuoneshane ukenge ( in mkojani's voice ) sekunde tu
Ila tatizo ni kwamba utafanya mambo yazidi kuwa magumu na ujue Hawa jamaa huwa wanalindana unaweza kuuziwa kesi mbaya ukabaki kujishangaa, Kuna msemo kule kwetu hua tunasema ukishindana na mjinga atakutoboa macho
 
tatizo unakaabaa kinyonge wahuni wanakulia timing wanaona helahii hapa

wanaamua kukupelekesha watakavyo.acha uzoba ukiingia sehemu vimba chukua hata mademu wawili watatu vimba nao wanyweshe....
Bahati mbaya au nzuri ni kwamba mm na hao mademu ni mbali mbali na hua sitaki bugudha na mtu ndio maana natafuta chamber iliyotulia nagonga vitu vyangu ila nichokoze sasa ndio utajua hujui Kwa taarifa yako muda afande haamini kama Nina connection na watu wazito hapa town japo kimuonekano unaweza kufkiri mm ni bwege
 
Bahati mbaya au nzuri ni kwamba mm na hao mademu ni mbali mbali na hua sitaki bugudha na mtu ndio maana natafuta chamber iliyotulia nagonga vitu vyangu ila nichokoze sasa ndio utajua hujui Kwa taarifa yako muda afande haamini kama Nina connection na watu wazito hapa town japo kimuonekano unaweza kufkiri mm ni bwege
🤣🤣🤣Kwani mtu bwege huwa yukoje?
 
Bahati mbaya au nzuri ni kwamba mm na hao mademu ni mbali mbali na hua sitaki bugudha na mtu ndio maana natafuta chamber iliyotulia nagonga vitu vyangu ila nichokoze sasa ndio utajua hujui Kwa taarifa yako muda afande haamini kama Nina connection na watu wazito hapa town japo kimuonekano unaweza kufkiri mm ni bwege
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom