Polisi FFU wanavyojichukulia rushwa barabarani

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,173
Reaction score
22,772
Kumezuka mtindo askari waliovaa mavazi kama ya FFU combat za kijani kukamata magari kwa visingizio mbalimbali.

Wengi pia hukamata waendesha boda boda na kuwakung'uta mifuko yaani kuwapiga mkwara watoe rushwa. Pichani askari wawili wa aina hiyo wakiwa wanazunguka zunguka kutafuta wateja maungio ya barabara inayotoka Karume na inayotoka Veta Chang'ombe.

Ukivuka tu reli kama umetoka ile barabara inayotoka Ilala, Karume ikapita Machinga Complex kukutana na Nyerere Road.

Ni mara nyingi hawa askari huwa wanapita wakiwa na silaha kutafuta tafuta watu wa kuwapiga mkwara na kupewa rushwa.

Tabia hii naomba niulize kwa mamlaka je hawa FFU pia hufanya kazi za traffic? Maana mara nyingi nimewakuta hata wakisimamisha magari na kukagua. Lakini cha kujiuliza hawana hata zile mashine za kutoa risiti wakilipwa pesa.

Je hawa wamehalalishwa kufanya haya wayafanyayo? Ni nani anapasea kukamata raia kwa makosa ya vyombo vya usafiri au madereva barabarani?

Screenshot_20191108-192610~2.png

Screenshot_20191108-192605~2.png
 
Ungekuwa na akili ungegundua kuwa
1. Hiyo picha imepigwa mbali
2. Imekuwa cropped sana kuondoa some details.

Simu ambayo imepiga hii picha ni moja ya the best simu camera. Sony Ericsson tuulize tulioanza kutumia simu miaka ya 1998. Tunaweza kukueleza kila simu uzuri wake na ubaya wake.

Shida ni hio TEKNO uliyotumia mzee baba.
 
Kwenye mafunzo ya udereva wanafundisha, askari yoyote anaruhusiwa kukusimamisha, kukuhoji, na kukukamata ikibidi.

Hao ni askari wa doria, na wamepangiwa sehemu hiyo na kazi yao kubwa ni kuangalia usalama wa raia na mali zao, katika eneo hilo ikiwemo kukamata magendo.

Tatizo pale wanapofanya kazi ya utrafiki.

Jiulize, huyo polisi akikumata ukamwambia wewe siyo trafiki, akakubali, akakwambia twende kituoni ukaonane na trafiki, na una makosa kibao, je utaenda au utatoa rushwa? Mfano, ukienda kuonana na trafiki utalipa faini elfu 90, huyo jamaa anataka ten! Rushwa ina faida na hasara.
 
Ungekuwa na akili ungegundua kuwa
1. Hiyo picha imepigwa mbali
2. Imekuwa cropped sana kuondoa some details.

Simu ambayo imepiga hii picha ni moja ya the best simu camera. Sony Ericsson tuulize tulioanza kutumia simu miaka ya 1998. Tunaweza kukueleza kila simu uzuri wake na ubaya wake.
Tatizo ni
here-ithink-you-dropped-this-39628760.jpeg
 
Kama kosa lako ni bima imeisha akakukamata ukampa rushwa 10,000 au 5,000 baada ya hapo bima inakuwa valid? Je una hakika gani hutakamatwa tena huko mbele?au utasema nlishakamatwa nikatoa rushwa huko nlikotoka?

Kama kuna kosa mimi hupenda kuandikiwa then ntalipa.sitoi rushwa na siku moja nlijaribu ikanigharimu sababu nlivunja kanuni yangu i paid a lot kwa kosa la kuvunja kanuni ya kutotoa rushwa.

Kwenye mafunzo ya udereva wanafundisha, askari yoyote anaruhusiwa kukusimamisha, kukuhoji, na kukukamata ikibidi.

Hao ni askari wa doria, na wamepangiwa sehemu hiyo na kazi yao kubwa ni kuangalia usalama wa raia na mali zao, katika eneo hilo ikiwemo kukamata magendo.

Tatizo pale wanapofanya kazi ya utrafiki.

Jiulize, huyo polisi akikumata ukamwambia wewe siyo trafiki, akakubali, akakwambia twende kituoni ukaonane na trafiki, na una makosa kibao, je utaenda au utatoa rushwa? Mfano, ukienda kuonana na trafiki utalipa faini elfu 90, huyo jamaa anataka ten! Rushwa ina faida na hasara.
 
Kwenye mafunzo ya udereva wanafundisha, askari yoyote anaruhusiwa kukusimamisha, kukuhoji, na kukukamata ikibidi.

Hao ni askari wa doria, na wamepangiwa sehemu hiyo na kazi yao kubwa ni kuangalia usalama wa raia na mali zao, katika eneo hilo ikiwemo kukamata magendo.

Tatizo pale wanapofanya kazi ya utrafiki.

Jiulize, huyo polisi akikumata ukamwambia wewe siyo trafiki, akakubali, akakwambia twende kituoni ukaonane na trafiki, na una makosa kibao, je utaenda au utatoa rushwa? Mfano, ukienda kuonana na trafiki utalipa faini elfu 90, huyo jamaa anataka ten! Rushwa ina faida na hasara.

Lakini askari anapomsimamisha mtu anatakiwa kumpa sababu za kumzuia,

Lakini wengi ama hawajaelimishwa juu ya hilo, wengine huwa wahawajulishi wananchi sababu za kuwasimamisha au kuwazuia ,
Na mwananchi anapouliza imekuwaje askari anachukia na kumwambia usinihoji

Kwanini kusiwepo na mawasiliano kati ya askari na mwananchi?

Kwani mwananchi ni mtuhumiwa? Hata mtuhumiwa anazo haki zake vivyo hivyo hata mfungwa anazo haki zake!
 
Wote Wanaruhusiwa Kufanya Kazi, Shida Ipo Kwenye Kuomba Kiwi
 
Kumezuka mtindo askari waliovaa mavazi kama ya FFU combat za kijani kukamata magari kwa visingizio mbalimbali.

Wengi pia hukamata waendesha boda boda na kuwakung'uta mifuko yaani kuwapiga mkwara watoe rushwa. Pichani askari wawili wa aina hiyo wakiwa wanazunguka zunguka kutafuta wateja maungio ya barabara inayotoka Karume na inayotoka Veta Chang'ombe.

Ukivuka tu reli kama umetoka ile barabara inayotoka Ilala, Karume ikapita Machinga Complex kukutana na Nyerere Road.

Ni mara nyingi hawa askari huwa wanapita wakiwa na silaha kutafuta tafuta watu wa kuwapiga mkwara na kupewa rushwa.

Tabia hii naomba niulize kwa mamlaka je hawa FFU pia hufanya kazi za traffic? Maana mara nyingi nimewakuta hata wakisimamisha magari na kukagua. Lakini cha kujiuliza hawana hata zile mashine za kutoa risiti wakilipwa pesa.

Je hawa wamehalalishwa kufanya haya wayafanyayo? Ni nani anapasea kukamata raia kwa makosa ya vyombo vya usafiri au madereva barabarani?

View attachment 1257944
View attachment 1257945
Wanakaguwa usalama,nadhani ni jambo jema.
 
Maaskari wote including wanajeshi, wanaamini utrafiki unalipa.... wamejiongeza acha wavune mapesa sio wale wengine kutwa kufyeka bustani pale Lugalo kama wafungwa.
 
Lakini askari anapomsimamisha mtu anatakiwa kumpa sababu za kumzuia,

Lakini wengi ama hawajaelimishwa juu ya hilo, wengine huwa wahawajulishi wananchi sababu za kuwasimamisha au kuwazuia ,
Na mwananchi anapouliza imekuwaje askari anachukia na kumwambia usinihoji

Kwanini kusiwepo na mawasiliano kati ya askari na mwananchi?

Kwani mwananchi ni mtuhumiwa? Hata mtuhumiwa anazo haki zake vivyo hivyo hata mfungwa anazo haki zake!
Wanajua sana na wamefundishwa hivyo, sema ndo mambo yanaenda hovyobovyo tu, na wao wanakukamata ili kupata chochote na ndo mana wanakusimamisha kwa mkwara.

Nenda kule vijijjni ndo utawahurumia wanakijiji wakikamatwa. Unakuta anapigwa mkwara kwanza, " kwa kosa lako hili la bima, wewe ni jela moja kwa moja" Basi mwanakijiji akisikia hivyo, utasikia "nisameheni jamani" hapo tayari kaliwa
 
Lakini askari anapomsimamisha mtu anatakiwa kumpa sababu za kumzuia,

Lakini wengi ama hawajaelimishwa juu ya hilo, wengine huwa wahawajulishi wananchi sababu za kuwasimamisha au kuwazuia ,
Na mwananchi anapouliza imekuwaje askari anachukia na kumwambia usinihoji

Kwanini kusiwepo na mawasiliano kati ya askari na mwananchi?

Kwani mwananchi ni mtuhumiwa? Hata mtuhumiwa anazo haki zake vivyo hivyo hata mfungwa anazo haki zake!
mkuu kama sheria inampa mamlaka askari kukusimamisha na kukuhoji,ni ukichaa kuuliza anakusimamishia kitu gani.ndio maana jibu huja USIHOJI.

kuhoji huzalisha mashaka zaidi kwa askari,na kumuongezea umakini kukukagua ambao utasababisha upotevu zaidi wa muda.

NOTE msikariri kwamba kuna askari wa barabarani,askari polisi yoyote unayemjua,awe FFU au sijui nani,anayo mmlaka ya kukusimamisha kukuhoji na kukukamata.hizo rangi za nguo ni za vitengo vyao vya upolisi,ambavyo havibadili kabisa jukumu lao la msingi(UPOLISI).kifupi mwenye mamlaka ya kuhoji uhalali wa ffu kuwepo barabarani ni askari mwenzie sio mwananchi wa kwaida.wewe tii amri utakayopewa.
 
Lete muongozo unaosema wote wanaruhusiwa kufanya kazi za usalama barabarani tuone.
muongozo upo kwenye katiba yao ya majukumu.huwezi kuikuta kwenye sheria za kwaida maana zinawatambua kama wote ni polisi wa chuo cha polisi moshi,ila kitabu chao cha ndani ndio kinagawa majukumu.

sasa shikwa na FFU jitetee,mwambie wewe sio traffic uone kama utashinda hiyo case.
 
Trafiki pekee ndio wamebaki kwenye rushwa.
 
muongozo upo kwenye katiba yao ya majukumu.huwezi kuikuta kwenye sheria za kwaida maana zinawatambua kama wote ni polisi wa chuo cha polisi moshi,ila kitabu chao cha ndani ndio kinagawa majukumu.

sasa shikwa na FFU jitetee,mwambie wewe sio traffic uone kama utashinda hiyo case.

Mimi najielewa siyo muoga kama wewe!

Akija kwa utaratibu wala haina shida, kuwa askari siyo kwamba ndo kuwa mwamba bali ni mgawanyiko wa majukumu tu

Kwamba yeye kama askari mimi naweza kuwa daktari akiumwa namtibu,

Au mwingine mhasibu anamlipa mshahara n.k

Na mwisho wa siku wanalipwa kodi zetu!

Mimi siyo wa aina yako
 
Back
Top Bottom