Polisi Dar, yawahoji kundi la Orijino Komedi, walazwa Kolokoloni

waambie hata USA kuvaa mavazi ya kijeshi kwa ajili ya filamu ni kibali
hata Nchi yoyote unayotumia magari au vifaa vya kijeshi kwa kuchezea filamu au tamthiliya ni kwa kibali maalum.
Huwezi vaa nguo hizo km ww si mhusika eti ukatolee mahari au ukamkamate mgoni wako halafu utarudisha,
nimeamini kweli kina Joti na Masanja ELIMU ELIMU elimu hakuna
Amen.
 
Mimi ni hiyo picha ndo imeniacha hoi. Wafupi taabu. Check walivyorusha miguu, hakuna mfanano. Mfupi zaidi karusha juu sana,akifuata anayefuatia kwa ufupi,baadaye mngongoti wao.
 
Wewe bakia Na Elimu Elimu yako wenzio wana sheherekea UJANA
Aluekuambia ujana unasheherekewa ni nani? ukifanya sensa karibu wote watasema tunataka turejee kwenye hali ya Utoto na sio ukijana ambo wengi hufanya mistake mbaya
 
Hakuna nchi inaruhusu uniform zake za jeshi, polisi, na kadha wa kadha zidhalilishwe kwahiyo hii ilikuwa kabla Magu hajachaguliwa na itaendelea, ukifanya nchini Kenya haya ama huko mbele adhabu itabakia pale pale
Usidanganye umma. Nguo za jeshi lolote zinaruhusiwa kuigizia maigizo ya maonesho kwa waigizaji kufuata taratibu za kuomba kibali. Wakiruhusiwa,hubidi "kukochiwa",ili vitendo vyao visilidhalilishe jeshi husika kwa maigizo watakayoyafanya,kisha wakimaliza huzirejesha sehemu inayohusika.
 
[URL][URL][/URL][/URL]

Pathetic.
Jeshi la polisi hovyo kabisa. Kosa gani ambalo watu hawa wamefanya. Jeshi la polisi tumieni weledi. mbona mnashindwa kuwakamata wanaotorosha nyara za serikali na majambazi au mafisadi? Nguo zinazoshabiana na uniform zenu ni vazi tu na hakuna sheria yoyote inayosema ni kosa mtu kuvaa nguo zinazoshabia rangi na uniform zenu. Bado jeshi la polisi linafanya kazi kwa misingi ya kikoloni kabisa. Kwani hao waigizaji walivaa hizo uniform na kwenda kufanya uharifu?
Watu wanavaa Vazi linaloshabihiana na vazi la kifalme au la kiongozi mkuu wa dini la kini hawakamatwi, sembuse hizo zinazoshabihiana na uniform zenu!! kwa mtindo huu itafika mahala mtakama watu wanavaa suti inayoshabihiana na suti ya Rais sasa. SIjawahi kuona katika ulimwengu huu jeshi la hovyo kama jeshi la polisi Tanzania. Bado mnaishi enzi za ujima??

Sema baba sema
 
usi ongee kishabiki wewe bila kushirikisha akili....angalia hiyo mikanda viunoni mwao ni typical Tz police belt, hiyo ni kosa kisheria kubali kataa kuvaa/kumiliki nguo za askar wa Tanzania bila kibali maalumu ni kosa kisheria....msizoee kufanta mambo kiholela...
Kufanta?
 
View attachment 383345
Jeshi la Polisi limewahoji wachekeshaji wa Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa nguo zinazoshabihiana na sare za Polisi.

Jeshi la Polisi Dar leo limewahoji wasanii wa Orijino Komedi makosa ya kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii mwenzao Emanuel Mgaya “Masanja”.

Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti, Alex John “Mac Reagan” na Isaya Gideon “Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba na meneja wa kundi hilo, Sekioni David.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Dar zinaeleza kuwa wasanii hao walikamatwa tangu jana jioni na kulala kituo cha Polisi hadi walipohojiwa juu ya tukio hilo.
Kitu kidogo kilichokosa fikra kitawagharimu sana! Kama hawana vipindi walivyotayarisha kabla....litakuwa pigo
 
Back
Top Bottom