Jeshi la polisi lawahoji na kuwashikilia wasanii wa Orijino Komedi

Rogart Ngaillo

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
899
1,887
Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Dar leo
limewahoji wasanii wa Orijino Komedi kwa
makosa ya kuvaa sare za polisi kwenye
harusi ya msanii mwenzao Emanuel Mgaya
“Masanja”. Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti,
Alex John “Mac Reagan” na Isaya Gideon
“Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba
na meneja wa kundi hilo, Sekioni David. Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Dar zinaeleza
kuwa wasanii hao walikamatwa tangu jana
jioni na kulala kituo cha Polisi hadi
walipohojiwa juu ya tukio hilo. Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya
kijamii zinawaonesha wasanii hao wakiwa
wamevalia sare zinazofanana na zile za
Jeshi la Polisi wakiwa wanafanya gwaride,
kama ishara ya kumpa heshima mwenzao,
Emmanuel Mgaya “Masanja” aliyeachana na ukapera.
Source: Mwananchi
 
Mbona bongo movie wamevaa sana.
Ila hata siwatetei sababu ndio chama chao wacha wasomeshwe number japo kidogo.
 
Ngoja waisome number maana ndio walikuwa wanampigia debe CCM.wamuombe Lizaboni akawatoe.na hawana wanasheria makini kama chadema.

swissme
 
Mbona hawa jamaa ling time walikua wanavaa haya magwanda? Walikua hawawaoni.
Wamezidi offside kwa hili tukio sasa kwani walitengeneza mkanda wenye rangi za bendera ya taifa ambao ni exclusive right ya mapolisi sasa wasipothibitiwa kesho watakwenda na A.K. 47 ni lazima vitu vya kijeshi au vinavyofanana na vya jeshi sisi raia tuwaachie jeshi wenyewe kama tumeishiwa ubunifu wa kufanya watu wacheke tuache usanii lanini sio kugusa au kuiga yasio igika.
 
At last mpango wao wa kutafuta kick umekubali....shukran Pastor Emmanuel Mgaya kwa kuja na idea hiyo.
 
Back
Top Bottom