Polisi dar waua tena

Jamani huyo kijana namjua sana alikuwa fundi wangu pia, ni aina ya vijana wanaopenda kuwa close na watoto wa wakubwa siwezi kukubali kirahisi kama mtu akinimbia kuwa alikuwa mtekaji nyara. Na pia mimi story yote naijua toka usiku ule ule namtoa story hajakosea japo kuna additions kidogo ambazo nadhani hajakosea maana vitu vingine vyooote viko sahihi. Ule ugomvi haukuwa wa yula kijana hata kidogo. Na kama polisi walikuwa right kwa nini walipelekwa polisi usiku ule ule maana vijana wengine waliibroke gari ya polisi muuaji wakapiga simu polisi wakaja kumchukua polisi muuaji hapo unapaelezaje? watekaji ndo walipiga simu polisi? Kama hamjui msimbishie mtoa hoja.
 

Mkuu Tizo,

Nakushukuru kwa maelezo yako mazuri juu ya hili tukio. Lakini naomba nitofautiane na wewe kitu kimoja kwamba polisi hawana haki ya kumuua mtu hata kama alitaka kuwapora silaha. Kwa nini polisi huyo akumpiga risasi mguu ili kumpunguza nguvu badala ya kumuua? Hakuna sheria inayoruhusu polisi kuua lakini kwa Tanzania hii sasa imekuwa ni kawaida na hakuna anayeona kwamba hapa kuna tatizo. Kesho utapigwa risasi wewe ufe kwa kuwa umeonekana unasalimiana na nyumba ndogo ya mzito mmoja na polisi watatwambia ulikuwa jambazi. Mwalifu akamatwe na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria sio kuuwawa na polisi bwana!!!!!!! Utawala wa sheria huko wapi hapa?

Tiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…