Polisi Dar wamhoji Londa

Polisi Dar wamhoji Londa

AK-47

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2009
Posts
1,373
Reaction score
202
[FONT=Comic Sans MS, cursive]Jeshi la Polisi limethibitisha kumhoji Meya wa Manispaa ya Kinodoni Bw. Salum Londa kwa tuhuma za kuhusika kwake na uuzwaji wa maeneo ya wazi pasipo utaratibu.[/FONT]


[FONT=Comic Sans MS, cursive]Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amethibitisha hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo mbali na Bw. Londa, jeshi hilo pia limewaita na kuwahoji watu wengine 30 wakiwemo diwani wa Manzese na Sinza.[/FONT]


[FONT=Comic Sans MS, cursive]Kamanda Kova amesema zoezi la kuwahoji limeanza tangu Jumapili na kwamba ofisi yake inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na kuahidi kuwa watafikishwa mahakamani punde uchunguzi utakamilika na kuonyesha kuwa wana kesi ya kujibu.[/FONT]


[FONT=Comic Sans MS, cursive]Hatua ya kuhojiwa Bw. Londa na wenzake imekuja siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. William Lukuvi kufunga ofisi za ardhi katika manispaa zote za jiji na kwa madai ya kuuza maeneo ya wazi. [/FONT]
 
Si ajabu watakaopata 'kibano' ni watu wadogo kabisa, vigogo wakapona.
 
Back
Top Bottom