Jeshi la polisi Dar lakusanya milioni 840 kwa faini ya makosa mbalimbali ya barabarani kwa wiki moja

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 840 za faini ya makosa mbalimbali ya barabarani kwa kipindi cha wiki moja ya oparesheni iliyofanywa na jeshi hilo.

IMG_9374-1.jpg


Akiongea na waandishi wa habari, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kiwango cha mapato hayo ni kidogo na inaashiria kupungua kwa makosa yanayofanywa na madereva.

“Kwa upande wa barabarani tunakwenda vizuri kati ya tarehe 1 mwezi 3 mwaka 2017 mpaka tarehe 9 mwezi wa 3 mwaka 2017 takribani siku hizo 8 tumeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 840 kwahiyo niseme tu kwamba mapato yanapungua hii tu ni kwasababu watu wameanza kutii tu sheria ya usalama barabarani,” Alisema Kamanda Sirro.
 
Hizi sifa zitatutokea ....


Badala ya kuhimiza elimu ya usalama barabaran mnahimiza askari KUKUSANYA MAPATO

Tunaichelewesha Tanzania!


Ushauri huu hapa wa haraka

kama mapato ya faini ni makubwa kiasi hiko kwa wiki
Ni alama tosha kwamba usalama barabarani ni Gwajima (zero)

Sasa futeni lesemi zote,

Wenye magari turudi shule kwanza


Maana haya magari huchukua roho zetu BILA HURUMA hata mbele ya hao askari wenu!


Ni ushauri tu!
 
Yan hizo hela zingekuwa wanagewa police wenyewe, wangekuwa na mishahara mikubwa sana hawa jamaa na wasingelialia njaa km saivi.
 
Hiyo watu wanaweza kutafsiri kama ni mafanikio kumbe upande wa pili kazi tunayo kuhusu matumizi sahihi ya barabara
 
Mmmmmh haya bana kumbe Dar tunaifaidisha hivo serikali

Madereva tuungane tuache kufanya makosa barabarani ili wakose hayo mapato
 
Hiyo milioni 840 ni kwa mda gani, wiki, mwezi, miezi au?Anyway, hizo pesa zikarekebishe taa za barabarani, alama za barabarani na miundo mbinu ya barabara
 
Ila kwa Madereva wa Dar discipline imerudi sana na hasa kwa taa za barabarani.Wameanza na "vitochi vya 50KPH" kwenye barabara kadhaa kadhaa za jiji.Kwa ufupi hawa yange yange kwa sasa ni balaa.
 
Back
Top Bottom