Polisi: Chadema ruksa kupiga kambi kulinda kura

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi Taifa wamesema kuwa wananchi wanaruhusiwa 'kupiga kambi' katika kituo cha kuhesabia kura lakini wakiwa umbali wa mita 200.

Tamko hilo limetolewa katika kikao cha wadau mbalimbali wanaoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Arumeru ambacho kiliwashirikisha viongozi wa NEC taifa, akiwemo Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Damian Lubuva, na Mkurugenzi Julius Mallaba pamoja na mkuu wa operesheni wa jeshi la polisi katika uchaguzi huo, Issaya Mungulu.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Polisi, Issaya Mungulu, alitoa msimamo huo akisema kisheria watu wako huru kusubiri shughuli ya kuhesabu kura na matokeo wakiwa maeneo ya vituo vya kupigia kura lakini wanapaswa kuwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka kituo cha kupigia na kujumlishia matokeo.

"Sasa kama wanavyodai watapiga kambi kulinda kura wakiwa umbali wa mita 200, sisi tutasimamia sheria inayoelekeza wawe umbali huo na watakaosimama sehemu isiyovunja sheria hatutakuwa na shida nao," alisema Mungulu.

Gazeti la Tanzania Daima.
 
  • Thanks
Reactions: kmk
Kupiga kambi mita zaidi ya mia mbili? Sheria ya uchaguzi inasemaje? Jeshi la polisi lina nia ya dhati kweli ktk kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki!?
 
Mita 200 sawasawa na viwanja viwili vya mpira wa miguu hapo mtu unakuwa unalinda kura gani!!kama hiyo sheria ipo ivyo basi tume iwagawie wananchi miwani yakuona mbali ili wana Arumeru waone kinachoendelea kwenye majumuisho kuondoa uchakachuzi wa magamba.
 
Back
Top Bottom