Polisi bado kuna uozo, Polisi wanaofanya makosa wafukuzwe badala ya kupangiwa kazi nyingine

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Mh Rais, salamu nyingi zikufikie.

Najua wewe sio member ila huwa unasoma sana JamiiForums na mengi umeyapata kupitia humu na kuyafanyia kazi.

Kuna jambo moja nataka uniondoe wasi wasi, hivi msimamo ni kutumbua majipu au kuyaondoa usoni na kuyaweka kwapani?

Kashfa nyingi zinazohusu jeshi la polisi mbali na uthibitisho usio na shaka,bado majipu yamehamishwa, kwanini yasiondolewe kabisa mwilini?

Kuhamisha jipu mara nyingi hugeuka kansa,jipu ni jipu dead cells zake hazifufuki.

Najua kuna watu wameondolewa nafasi za juu polisi sasa wapo mikoani,kuna watu wameondolewa mikoani wapo makao makuu ya jeshi,wengine wamehamishwa wilaya zao.

Naomba kama unatumbua tumbua kama unahamisha msamiati wa kutumbua achana nao kabisa maana utakupa umaarufu wa muda mfupi tu na dharau ya kudumu.

Najua mkuu wao anatumbua kwa huruma,uswahiba wake unamponza na amedangnywa sana na wawakilishi wake, hebu mwambie awe serious na jeshi letu. Kama polisi anakuwa mbadhirifu nani atakuwa muungwana?

Wapo waliopewa magari,fedha na nyumba wakati wa chaguzi,fukuza wote maana wamepoteza imani kwa askari wadogo.

Ipo siku utakumbuka ninachosema kama utatenda au itaacha.

Karibu Tanga utumalizie mgogoro wa Meya kama ilivyokuwa huko Dar.
 
Unamaanisha Mtweve, Magayane, Chagonja na wengine. Kuna kubwa lao lililostaafu linaitwa Mwema, huyo na mkwewe Said Lugumi ni hatari sana kwa taifa hili.
 
Mh Rais, salamu nyingi zikufikie.

Najua wewe sio member ila huwa unasoma sana JamiiForums na mengi umeyapata kupitia humu na kuyafanyia kazi.

Kuna jambo moja nataka uniondoe wasi wasi, hivi msimamo ni kutumbua majipu au kuyaondoa usoni na kuyaweka kwapani?

Kashfa nyingi zinazohusu jeshi la polisi mbali na uthibitisho usio na shaka,bado majipu yamehamishwa, kwanini yasiondolewe kabisa mwilini?

Kuhamisha jipu mara nyingi hugeuka kansa,jipu ni jipu dead cells zake hazifufuki.

Najua kuna watu wameondolewa nafasi za juu polisi sasa wapo mikoani,kuna watu wameondolewa mikoani wapo makao makuu ya jeshi,wengine wamehamishwa wilaya zao.

Naomba kama unatumbua tumbua kama unahamisha msamiati wa kutumbua achana nao kabisa maana utakupa umaarufu wa muda mfupi tu na dharau ya kudumu.

Najua mkuu wao anatumbua kwa huruma,uswahiba wake unamponza na amedangnywa sana na wawakilishi wake, hebu mwambie awe serious na jeshi letu. Kama polisi anakuwa mbadhirifu nani atakuwa muungwana?

Wapo waliopewa magari,fedha na nyumba wakati wa chaguzi,fukuza wote maana wamepoteza imani kwa askari wadogo.

Ipo siku utakumbuka ninachosema kama utatenda au itaacha.

Karibu Tanga utumalizie mgogoro wa Meya kama ilivyokuwa huko Dar.

Siyo kila mtu anaweza kufukuzwa tu hivi hivi ni lazima uangalie pia na mazingira ya mtu, Askari ni wa usalama na hii iko kwenye mafunzo yao, na ukiwa mwana usalama siku zote utakuwa mwana usalama!
Nafikiri haya mambo tuwaachie wenyewe wana usalama wanajua jinsi ya kuwaadhibu wanaokwenda kinyume na taratibu, maadamu tatizo wameshaliona!
 
Nyie si mnawadharau kuwa wana mishahara midogo????? acha na wao wale kwa urefu wao.
 
Hali mbaya hakuna kibaka hakuna polisi wote wale wale,kweli ccm ni ile ile
 
Back
Top Bottom