Kuna baadhi ya askari wa jeshi la polisi wanashiriki uhalifu

canular

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
858
813
Lazima ukweli usemwe, wakuu uhalifu wa mitaani huko una connection kubwa na Baraka kutoka kwa Polisi wenye njaa na umasikini wa kutupwa. Polisi hawa wapo kwenye jeshi la polisi kutimiza wizi, ujambazi, uchomozi, na vitu kama hivyo kwa kushirikiana na raia wa mtaani. Iko hivi mwaka juzi nimeibiwa Mali zangu nyingi tu za thamani nilipokuwa hotelini.

Ilikua ni Dar maeneo ya Kunduchi nilikua hotel ya mjamaa mmoja wa usalama nikajiaminisha itakua salaama hotel iko saafi kuna CCTV Camera kila kona geti kubwa ulinzi wa kutosha kumbe humohumo kuna vipanga wahudumu wa humo wana connection na wezi kuwapa taarifa za wateja ambao wako vizuri.

Wahudumu wa mahotel wanajua siri zote za wateja wao yupi ana Mali yupi hana kitu sasa ikasukwa njama na walinzi wakaungana na wezi wao wezi pia wakaungana na vikosi vyao vya kiwizi vilivyomo kwenye jeshi la polisi sasa picha linaanza nilikua nimetoka kwenda kubadili dollar maeneo ya Kibo pale kuna Bank halafu nikapitia sehemu kula msosi maeneo hayo kuna bar zilikua hot sana.

Muda ule nimekaa pale kwa muda kama masaa manne sasa nikaamua kurudi hotelini halooo nilicho kikuta sikua mini kama kweli uhalifu wa vile kuvunja Mlango wa chumba nilichokua nimelipia Mali zote niliziacha humo nakuta kumevunjwa wamebeba malapto 2, WiFi 2 Pete 2 silva na gold mix gold wamechukua ela yote zaidi 3 million na laki saba na 35800 mpaka silva zilikuepo Machenchichenchi sikujua zilikua kama ngapi wakachukua nguo za ndani pia wakabeba fasta.

Nikaripoti polisi wakaja kumbe walio kuja ni wa kituo cha hapo hapo mtaani michezo yao wanashiriki pamoja na wahalifu mbaya zaidi mwenye michezo hiyo alikua ni mkuu wa kituo hicho kidogo walivyo fika badala ya kusaidia upatikanaji wa Mali zangu wakanishika mimi kwa sababu eti nimewafanyia fujo hao wahudumu wa hapo hotel ni kapelekwa polisi kituo kidogo hapo mtongani walianza kunitisha na kuniomba ela na kunisakizia kesi mimi kwamba nimekula njama na wezi ili waniibie kwamba Hotel inilipe Daah nyie hii dunia ina uonevu yaani chako kinachukuliwa kwa nguvu na bado wanataka wakutoe pia na ulicho baki nacho.

Wakuu nita endelea nikipata muda tena nitaweka wazi hiyo hotel pia na mengine mengi Leo nimeona nifunguke kwa sababu ya hao panya Road wanao wasumbua wa Tanzania humu mitaani hao panya wana muunganiko na hao polisi wasio waaminifu polisi wezi punguzeni njaa na uonevu na rushwa mnakera huyo polisi alio fanya huo mchongo nilipewa detail zake na subilia tu siku nikaamua nimtawanye nitakavyo weza
 
Back
Top Bottom